Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi mji wa Kigamboni wa
jijini Dar es salaam kuwa Wilaya kamili inayojitegemea, na kufanya mkoa wa Dar
es salaam kuwa na Wilaya nne
Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam,
Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya makazi Prof. Anna Tibaijuka amesema kuanzia
sasa mji wa Kigamboni utatoka na chini ya manispaa ya uongozi wa manispaa ya
Temeke.
“ Kigamboni itajitegemea kama Wilaya
kuanzia leo, na utakuwa chini ya Kigamboni Development Agency (KDA)”. Alisema
Prof. Tibaijuka
Kutengwa kwa Mji mpya wa Kigamboni kuwa Wilaya, kumekuja
baada ya kuundwa kwa chombo kijulikanacho kama Wakala wa Uendelezaji wa Mji
Mpya wa Kigamboni inayojulikana kwa Lugha ya Kiingereza kama Kigamboni
Development Agency (KDA), Alisema Prof. Tibaijuka
KDA, itakuwa na jukumu la kuendeleza Kigamboni kuwa mji wa
Kisasa, na kufafanua kuwa shuguli zote za kiserikali zitasimamiwa na chombo
hicho kwa kushirikiana na baraza la ushauri la mji wa Kigamboni. Alisema Prof.
Tibaijuka
Hatahivyo, Baraza la ushauri wa Wilaya ya Kigamboni utaundwa
kwa kushirikisha wawakilishi wa wananchi pamoja na Madiwani na Wabunge wa eneo
hilo.
EmoticonEmoticon