WAKAZI wa Miji ya Tanga na Dodoma wamepokea kwa hamasa kubwa zoezi la kuamia Digitali kuliko ilivyo kuwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaaam, kwani wakazi wengi wa maeneo hayo tayari walisha nunua Vingamuzi
Ikiwa leo ni siku ya kuzimwa kwa Mitambo
ya Analogia ifikapo saa sita usiku, Msemaji wa TCRA bwana Inocent
Mungy ambaye ni msemaji wa TCRA amesema hayo hii leo kwanjia ya simu
akiwa mkoani Dodoma, kuwa leo usiku kwa mikoa hiyo miwili mitambo ya
Analogia itazimwa na kuwashwa ya Digitali
Aidha, amesema kwa mkoa wa Tanga tayari
watu elfu 20 wameamia Digital hatakabla ya mitambo hiyo kuzimwa, Na
mkoani Dodoma hali iko hivyohivyo kwani tayari watu elfu 27
wameshaamia Digitali, huku idadi ndogo ya watu wasio zidi elfu 35
wakiwa ndio bado hawajaamia lakini niwengi sana walio jiandaa kuamia
kwa siku ya leo
Lakini bwana Inocent amesema, kuanzia
leo asubuhi kulikuwa na msururu wa watu wasiozidi 15 wakisubiri
kununua Ving'amuzi kwa mawakala mbali mbali mkoani Dodoma
“Kwa mkoa wa Dodoma tumefanya
majaribio katika maeneo ya Nong'ono nyuma ya chuo cha UDOM, tayari
Digital ikosawa kwa kutumiwa na kufikia muda halali tutazima mitambo
ya Analogy” alisema bwana Mungy
Hatahivyo bwana Mungy, amewataka
wananchi kusema aina ya Tv aliyo nayo, pamoja na eneo analo kaa kama
ni bondeni au eneo la Tambarare ilikuepuka usumbufu unaoweza
kujitokeza, na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kwenda na mtaalamu wa
kuunganisha king'amuzi wakati wa kuunganisha king'amuzi hicho
Kama kuna mtu anamalalamiko yoyote
nimuhimu kuyafikisha mahali aliponunua king'amuzi kwani, tayari
wamepokea malalamiko 180 na kuyafanyia kazi.
Pia bwana mungi amekanusha uvumi
unaoenezwa na vyombo vya habari kuwa kuna ina ya Kinga'amuzi ambacho
kitazimwa ifikapo June mwaka huu kuwa sio za kweli na kuwataka wanao
eneza uvumi huo kuacha maramoja
EmoticonEmoticon