Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo BAVICHA leo wameelezea sababu iliyo pelekea kuwatimua baadhi ya wanachama wake akiwemo makamu mwenye kiti wa BAVICHA Bi. Juliana Shonza kuwa ni kutaka kukiujumu chama hicho.
Akiongea na waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam, Mweyekiti wa Bavicha John Heche na kusema kuwa ni kukiuka taratibu na sheria za chama ndio sababu za kuvuliwa uanachama wa viongozi hao
"Tunanyaraka walizo andaa ikiwa pamoja na mambo waliyo jadili katika vikao viwili, ilikutaka kukihujumu chama" na kuongeza kuwa vikao vyao vilikuwa vyenye nia mbaya kwa chama hicho. alisema Heche
Aidha Heche alisema, Kuna ushahidi wakutosha kuwa walitaka kufungua chama kipya, pamoja na madai ya kumchafua Katibu Mkuu wa Chama hicho Mheshimiwa Wilbroad Slaa kwa madai ya Uongo, Alisema Heche
Hatahivyo imebainika kuwa wanachama hao walipewa nafasi ya kutoa madai yao kwa mujibu wa sheria za chama hicho na katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania lakini Hawakufanya hivyo na Badala yake wameishia kulala mika na kutoa shutuma za uongo
Kusoma Rekodi za
Messi,Ronaldo na Iniest
ingia Ukurasa wa Artical..........
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon