WAZIRI MKUU AKIRI MADAWA YA KULEVYA NI TATIZO NCHINI, AHAIDI KULISHUGULIKIA ILI KUKOMESHA ULEMAVU


WATU WENYE ULEMAVU MBALIMBALI WAKIPATA CHAKULA CHA MCHANA KWA PAMOJA

WAZIRI MKUU wa Tanzania, Mhe. Mizengo Pinda ameahidi kushugulikia tatizo la madawa ya kulevya nchini kwani nimiongoni mwa mambo ambayo yanapelekea kuwa na watu wenye ulemavu nchini, Waziri ameyasema hayo jana alipokuwa akihutubia umati mkubwa wa watu wenye ulemalemavu zaidi ya Elfu 4000

"Natambua swala la madawa ya kulevya nivhangamoto kubwa tunayo kabiliana nayo, pia nakiri kuwa nimiongoni mwa sababu zinazopelekea ongezeko la ulemavu, kwani vijana weyu wengi wamatumbukia huko". Alisema Pinda

Aidha Waziri Mkuu amewataka watanzania kuwajali na Kuwadhamini watu wenye ulemavu kwani nao nibinadamu kamawengine hivyo kuwatenga, kuwabagua ikiwa pamoja na kuwatesa aina maana yoyote kwani sote tutakufa, nakuongeza kuwa hakuna maana ya kufanya hayo kwa watu wenye ulemavu. Alisema Pinda

Naye Mwenyekiti Mtendaji wa makampuni ya IPP DK. Reginald Mengi amewasihi watu wasiona ulemavu kutowaacha walemavu kujisaidia wenyewe, Dr. Mengi amesema kuwa nijukumu la watanzania wote kuwakumbuka walemavu na kuwainua kiuchumi

MWENYEKITI MTENDAJI WA IPP DR. REGINALD MENGI AKITOA HUDUMA YA CHAKULA KWA BAADHI YA WALEMAVI- DIAMOND JUBILEE  SIKU YA JANA

" Watu wenyeulemavu wanatutegemea sisi tusio wlemavu ilikuwainua kiuchumi, nijukumu letu kuakikisha kuwa wanakuwa na hali nzuri ya kimaslahi" Alisema reginald Mengi

Dr. Mengi pia aliiomba Serikali kuhakikisha usalama wa Taifa unazidi kuwepo kwani pasipokuwepo na Amani watu wakwanza kuadhirika ni wale wasiojiweza ambao ni walemavu, wazee na watoto. Alisema

" Walemavu niwau ambao wanaitaji amani zaidi, amani ikitoweka wao ndio wengi watakao adhirika nijukumu la serikali kulinda amani ilikuwaweka walemavu katika hali ya Usalama" Alisema Dr. Mengi

Hii ni mara ya 19 Tangu kuazishwa kwa hafla ya chakula cha mchana kwa watu wenye walemavu.. hafla hii hufanyika kila mwaka ambayo huandaliwa na Mwenyekiti Mtendanji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi


EmoticonEmoticon