Raisi wa wanafunzi- Michael Charles aliyovaa skafu, pamoja na wanafunzi wengine wa IFM |
Raisi wa Serikali ya Wanafunzi IFM
(IFMSO) Michael Charles amekanusha wanafunzi wa IFM kutembea na wake
za watu huko Kigamboni na kuahidi kulifanyia uchunguzi jambo hilo
ilikubaini ukweli wa shutuma hizo kama zinahusiana na tukio la
kulawitiwa kwa wenzao wawili pamoja na kuporwa kwa vifaa vyao
“Nimara yangu ya kwanza kusikia
tuhuma hizi, na tunafanya uchunguzi ilikujua undani wa tukio hili.
Tayari tumeweka watu ambao wataleta majibu iwapo kama kuna wanafunzi
wanaovuta Bangi, Wanaojiusisha na Ulevi na iwapo kuna yeyote yuko
kwenye makundi ya uhalifu, na ripoti hiyo itatolewa kwenye Bunge la
Wanafunzi” Alisema Charles
Akiongea na Blog hii, Michael Charles
amesema, hakuwai kusikia tuhuma hizo kabla ya tukio lililotokea Taree
10. January 2013, lakulawitiwa na kuporwa mali kwa wenzao wawili
ambao wanaishi katika Hostel Binafsi (Off Campas) huko maeneo ya
Uwanja wa Machavi- Kigamboni.
Tukio hilo lilisababisha Wanafunzi wa
chuo hicho kuandamana ilikushunikiza vyombo vya usalama kuingilia
kati na kuchukua hatua juu ya matukio ambao yamekuwa yakihatarisha
usalama wao katika Hostel wanazo panga huko maeneo ya Kigamboni.
Wanafunzi hao wamedai kuibiwa Laptop zaidi ya 100 pamoja na
kulawitiwa kwa wenzao wawili
Wanafunzi wa chuo cha IFM juzi
waliandamana hadi makao makuu ya Jeshi la Polisi (WIZARA YA MAMBO YA
NDANI) wakimtaka Kamanda wa Kanda maalum ya Mkoa wa Dar es salaam
bwana Suleiman Kova kujitokeza na kusikiliza madai yao, ambapo
Waliahidiwa uhakika wa usalama wao na malizao
EmoticonEmoticon