Gharama
za kupiga simu kutoka mtandao wa kampuni moja ya simu ya mkononi
kwenda mwingine nchini, kuanzia Machi Mosi mwaka huu zitashuka kutoka
sh.115 hadi sh.34.9 kwa dakika moja.
Uamuzi
huo umefanywa na mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya
kufanya mapitio ya gharama za mwingiliano kwa kampuni za simu nchini
kwa mwaka 2013. Pia kuanzia Januari Mosi mwakani gharama hizo
zitapungua hadi sh.32.4.
Vilevile
Januari 2015 gharama hizo zitashuka na kufikia sh. 30.6, Januari 2016
gharama hizo zitadhuka mpaka sh. 28.6, Januari 2017 zitashuka mpaka
sh.26.9 kwa dakika moja.
Akitangaza
bei uamuzi huo jijini Dsm jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John
Nkoma alisema umetolewa kwa mujibu wa sheria ya TCRA ya mwaka 2003
sura 172. Profesa Nkoma alisema viwango hivyo ni vya kikomo cha juu
na pia ni bei elekezi lakini akasema kampuni za simu zina uhuru wa
kukubaliana kibiashara ili mradi makubaliano yao yasizidi gharama
zilizoelekezwa na TCRA.
- Kumpa mtumiaji uhuru wa kuongea bila kubadilisha badilisha laini
- Kumpunguzia mtumiaji mzigo wa kubeba simu na laini nyingi
- Gharama za simu nchini Tanzania ziko juu ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika
- Kudhibiti ukiritimba wa gharama zinazotozwa haswa mtu ananapopigia mtandao mwingine
Baadhi
ya sababu ya mabadiliko ya gharama za kupiga simu:
EmoticonEmoticon