WAFANYAKAZI- RIPOTINI MKINYANYASWA

 

SERIKALI IMEWATAKA WAAJIRI WANAO NYANYASA WAFANYAKAZI KUACHA MARAMOJA, HUKU IKIWASISITIZA WAFANYAKAZI KUZIJUA SHERIA ZINAZO WALINDA NA KURIPOTI KWENYE VYOMBO VYA SHERIA PINDI WANAPOPATWA NA MGOGORO NA WAAJIRIWA WAO

 Habari zaidi


Serikali imetoa onyo kwa waajiri wote hususani wale wawekezaji wanaowanyanyasa wafanyakazi kuacha maramoja kwani itawachukualia hatua stahiki na kuwataka watambue kuwa wamekuja kuleta ajiira stahiki na sio manyanyaso kwa wafanyakazi.

Akiongea leo Bungeni Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi Mhe. Dr Milton Makongoro Mahanga wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mariam Msabaha, ambaye alitaka kujua nihatua zipi serikali inachukua kwa waajiri ambao wanawanyanyasa wafanyakazi wao, Mahanga amesema nilazima waajiri watambue umuhimu wa haki kwa wafanyakazi wao

Aidha, amewaomba wafanyakazi kuelewa sheria zinazowalinda kazini na kuwasisitiza kutoa tarifa pale wanapokosa haki zao

Hatahivyo, tayari waajiri 13 wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la kuwanyanyasa wafanyakazi wao, huku kukiwa na tafiti mbalimbali ambazo zinafanywa na wizara ya kazi ilikuweza kudhibiti hali hiyo, huku elimu ikitolewa kwa waajiri na wafanya kazi kuondoa tatizo hilo. Alisema Dr Milton 


EmoticonEmoticon