Baada ya uzimaji wa mitambo ya
Analojia katika jiji la Dar es salaam, imebainika kwamba ni wananchi wachache
sana wa Dar es salaam wana uwezo wa kuangalia TV. Hii ni kwa mujibu wa utafiti
uliofanywa na shirika la habari la XHUSA.
Tanzania imekuwa nchi ya
kwanza Afrika Mashariki kuhamia mfumo wa kisasa wa matangazo wa Dijitali baada
ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na teknolojia kutangaza kwamba jiji la Dar es
salaam ndilo la kuanza kuathiriwa na mfumo huo mpya.
Hata hivyo utafiti huo
unaonyesha kwamba, wananchi walio wengi bado hawana ving'amuzi nyumbani kwao na
ni watu watano kati ya 20 ndio hupata huduma ya matangazo humu jijini. Hali hii
inatokana na bei ya ving'amuzi kuwa juu na wananchi walio wengi hawawezi kumudu
bei hizo.
Nchi za Afrika Mashariki
zimeamua kuhamia mfumo mpya wa matangazo miaka mitatu kabla ya muda wa
Shirikisho la Kimataifa la Mawasiliano hapo Juni 2015. Kenya, Uganda, Rwanda na
Burundi hajachukua uamuzi wa kuzima mitambo yao kwa sababu mbalimbali.
Kwa upande mwingine, Msemaji
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy amekanusha madai kwamba ni watu 5 kati ya 20
ndio huwapata matangazo katika mfumo huu mpya jijini Dar es salaam.
Aidha Bw. Mungy amesema
kwamba, ving'amuzi vimenunulika sana kabla na baada ya kuzima mtambo wa
Analojia jijini Dar na kwamba madai ya Shirika la Habari la XINHUA si za kweli.
Hata hivyo Bw. Mungy amesema kwamba tatizo ni kwamba walio wengi bado hawana
ujuzi wa kuunganisha ving'amuzi vyao kwa sababu wanashindwa kusoma na kuelewa
maelekezo yaliyoandikwa.
EmoticonEmoticon