PICHA TANO ZIKIONYESHA MADUKA YAKITEKETEA KWA MOTO TEGETA

Masaa machache yaliyopita Maduka kadhaa yameteketea kwa moto katika eneo la kibaoni jijini Dar es salaam kwa kile kilichodaiwa kuwa ni hitilafu ya umeme, mali zenye mamillioni ya shilingi yameteketea kwa moto


 Hii si mara ya kwanza kwa eneo hilo kuzukwa kwa moto na kuteketeza mali, Mwaka jana kanisa la Pendecoste katika eneo hilo liliteketea kwa moto na mali nyingi kuaribiwa huku chanzo kikiwa ni itilafu ya umeme
 

Octobar 26 mwaka jana maeneo hayohayo ya Tegeta by Night kulizuka moto na kuteketeza kabisa Duka la vifaa mbalimbali (Hurdware) huku chanzo kikiwa ni itilafu ya umeme
 

Kwa muda wa Mwezi sasa tatizo la moto kuteketeza maduka yamefululiza. Katika soko la Mwenge mpaka hivi sasa Maduka yaliyoteketea hayaja funguliwa hadi hivi sasa

Aliyejuza Blog hii kwa taarifa hizi amesema Zimamoto walifika eneo la tukio lakini kwa kuchelewa nakukuta tayari moto huo umeenea huku wananchi wakijikusanya kwa wingi kutazama moto huo

Hatahivyo bado haijajulikana mara moja nikiasi gani cha fedha kilicho haribiwa na kama kuna mtu yeyote amefariki katika tukio hilo

HABARI NA BENJAMIN
PICHA KWA HISANI YA STEVEN SANDU

WANAWAKE ELFU 4300 HUFARIKI KILA MWAKA KUTOKANA NA SARATANI YA KIZAZI



Miongoni mwa wanawake Elfu 6200 ambao hugundulika kuwa na Saratani, katiyao wanawake Elfu 4300 ufariki kila mwaka kwa ugonjwa huo. Wengi wawana wake hao niwenye umri kati ya miaka 15 na 44 ambao usumbuliwa na Saratani shingo ya kizazi

Akiongea le jijini Dar es salaam katika uzinduzi wa mpango wa pamoja wenye lengo la kudhibiti tatizo hilo, Waziri wa Afya na Ustawi wa jamii Mhe. Dkt Hussein Mwinyi amesema, Serikali pamoja na wadau wenye nia ya kusaidia taifa watashirikiana juu ya ugonjwa huo

"Niwanawake Elfu 4300 ndio wanao fariki kutokana na saratani ya shingo ya kizazi kila mwaka, miongoni mwa wale Elfu 6200 ambao hugundulika kuwa na ugonjwa huo hapa nchini" Alisema Dkt Mwinyi 

Aidha Waziri aliwataja Wadau hao kuwa ni Chama cha Wazazi na Malezi (UMATI), Marie stopes international pamoja na PSI, Ambao kwa pamoja wametangaza nia yakuungana na serikali katika kudhibiti tatizo la kansa ya shingo ya kizazi

Hatahivyo, Waziri amewataka wanawake na watu wengine kwa ujumla kujijengea tabia ya kwenda kucheki Afya yao ilitatizo liweke kudhibitiwa mapema

Kwa mujibu wa tafiti za Afya Duniani, hivi sasa ugonjwa wa Saratani (Cancer) ndio ugonjwa unaoongoza kwa kuuwa watu wengi zaidi ikifuatiwa na Maleria na Ukimwi

MWANZA KUHAMIA DIGITALI USIKU WA LEO


Leo usiku Wakazi wa mkoa wa Mwanza watahamia mfumo mpya wa kurushia matangazo wa dijiti, Kama ilivyo pangwa na TCRA

Akiongea na Blog hii akiwa Jijini Mwanza, Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Bw. Innocent Mungi amesema kwamba, wakazi wa Jiji la Mwanza wamejiandaa na wako tayari kwenda kwenye mfumo mpya wa dijiti.

Bwana Inocent amesema, Jiji la Mwanza na vitongoji vyake leo usiku saa 5 Dakika 59 na Sekunde 59 wanahama rasmi kwenda mfumo mpya wa dijiti, huku akieleza kuwa wakazi waeneo hilo tayari walijiandaa mapema

Mwanza ni mkoa wa Nne kuhamia katika mfumo mpya wa kurushia matangazo wa dijiti baada ya Dsm, Tanga na Dodoma.

Kwa mujibu wa ratiba ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania iliyotolewa Disemba mwaka jana, mikoa ambayo itafuata katika awamu ya kwanza ya uzimaji mitambo ya Analojia ni Kilimanjaro na Arusha mwezi wa 3 pamoja na Mbeya mwezi wa 4.
TANESCO: LIPENI DENI LENU ACHENI KULALAMIKA

TANESCO: LIPENI DENI LENU ACHENI KULALAMIKA


Stop grumbling and pay your debts, Tanesco told

By Mkinga Mkinga
The Citizen Reporter
SOURCE: The Citizen News Paper

Dar es Salaam. Tanesco should honour its contract with power supplier Songas and pay its debts, the government declared yesterday.

Speaking on the phone from Britain, Energy and Minerals Minister Sospeter Muhongo expressed surprise that Tanesco had failed to live up to its obligations. “I know Tanesco has a contract with Songas,” Prof Muhongo told The Citizen. “It should stick to it.”

Tanesco owes Songas Sh80 billion ($51 million) in outstanding bills covering the past six months. Songas has threatened to switch off Tanesco’s power supply if the state-owned firm does not pay up.

Prof Muhongo said the government was not involved in the transaction. “I wonder why the ministry should intervene when the contract is between the two,” he added. “You should go back to Tanesco and they should not escape from their duty…..I do not know how much the public utility owes Songas.”

Songas supplies about a quarter of the electricity Tanesco passes on to its own customers. Should it go ahead with the threat, most of the country will be plunged into darkness. According to Mr Chris Ford, managing director of Songas, the firm needs the money to maintain its facilities and it may have to shut down if it does not receive payment soon.

Tanesco Acting Managing Director Felchismi Mramba admitted that there was an outstanding debt but maintained that some of it had been cleared though he did not have precise figures. He added: “I understand that we have a contract with Songas but it is not proper to talk about the details in the media….we are bound by the contract. It’s true that we owe Songas billions and there is no way we can run away from that fact.”


NANI MKWELI HAPA .........???

NCHI IMEINGIA TENA GIZANI: MNYIKA ALIA NA TATIZO LA UMEME

NCHI IMEINGIA TENA GIZANI: MNYIKA ALIA NA TATIZO LA UMEME

Sikuambayo Blog hii ilitoa chapisho kuwaHAKUNA MGAO WA UMEME TANESCO WAFUNGUKA, HABARI ZA KUZIMWA MITAMBO YA SONGAS, BWAWA LA MTERA YAKANUSHWA,

John Mnyika, Mbuunge wa Ubungo na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini baba na mama wa Shirika la Umeme Tanesco, asema haya,

NCHI IMEINGIA TENA KWENYE MGAWO WA UMEME, SERIKALI IELEZE WANANCHI UKWELI NA HATUA KUHUSU UDHAIFU KWENYE UTEKELEZAJI WA MPANGO WA DHARURA

Nchi imeingia tena katika mgawo wa umeme kinyume na ahadi iliyotolewa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo bungeni tarehe 28 Julai 2012. 

Hali hiyo ni matokeo ya Serikali kutozingatia tahadhari niliyoitoa bungeni tarehe 27 Julai 2012 kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani na kwa nyakati mbalimbali kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini juu ya hali tete iliyotarajiwa kuwepo na hatua zinazopaswa kuchukuliwa katika utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme. 

Ikiwa ni sehemu ya wajibu wa kibunge wa kuisimamia Serikali nawataka viongozi na watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini na Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) kuacha kuficha hali ya mambo na kuwaeleza ukweli wananchi kuhusu mgawo wa umeme uliojitokeza na hatua za haraka zinazochukuliwa kurekebisha hali hiyo. 

Iwapo Wizara na TANESCO hawatatoa matangazo ya ukweli kwa wananchi, kwa nafasi yangu ya Waziri Kivuli wa Nishati na Madini nitaeleza vyanzo vya mgawo wa umeme uliojitokeza ili hatua ziweze kuchukuliwa wakati huu ambapo wajumbe wa kamati ya nishati na madini wenye wajibu wa kuisimamia Serikali kwa niaba ya Bunge katika sekta hizo nyeti hawajateuliwa.


Aidha, pamoja na kutoa maelezo kuhusu mgawo wa umeme, Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO watumie nafasi hiyo pia kueleza hatua zilizochukuliwa kuhusu ukaguzi wa awamu ya pili kuhusu tuhuma za ufisadi katika ununuzi wa vifaa na uzalishaji wa umeme wa dharura ikiwemo kuhusu mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme. 

Ikumbukwe kwamba mwanzoni mwezi Agosti 2012 Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (NAOT) iliunda timu ya wakaguzi kufanya ukaguzi maalum wa hesabu za Shirika la Umeme (TANESCO) kufuatia tuhuma za ubadhirifu wa fedha za umma zilitajwa bungeni na Waziri Kivuli wa Nishati na Madini katika maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani tarehe 27 Julai 2012 na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa majumuisho ya hoja ya Serikali tarehe 28 Julai 2012. 

Wizara ya Nishati na Madini na TANESCO waeleze pia hatua iliyofikiwa kuhusu uchunguzi mwingine uliofanywa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) kuanzia mwezi Agosti 2012 wa mchakato wa ununuzi wa mafuta mazito ya kuendeshea mitambo ya kufua umeme wa dharura kutokana na tuhuma mbalimbali zilizotolewa bungeni kuhusu ununuzi huo suala ambalo Kambi Rasmi ya Upinzani ilitaka pia tarehe 27 Julai 2012 liundiwe kamati teule ya Bunge ili uchunguzi wa kina uweze kufanyika. 

OFFICIAL VIDEO RUFFTONE NA THE GFU INAITWA MUNGU BABA

Wimbo huu ni miongoni mwa nyimbo kadhaa zilizotungwa na wasanii wa Kenya wakiamasihsa amani kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo. Kenya itafanya uchaguzi wake tarehe 4. 03. 2013 

                                      video wa wimbo mpya wa kuombea amani nchi ya kenya
KENYATTA AONA DALILI YA KESI YA ICC KUFUTWA

KENYATTA AONA DALILI YA KESI YA ICC KUFUTWA


Mgombea Urais kwa tiketi ya chama cha Jubilee bwana Uhuru Kenyatta anaye kabiliwa na mashitaka katika mahaka ya kimataifa ya ICC ametanhaza kesi yake haitafika popote na huenda ikafutiliwa mbali

Bwana Kenyatta amesema hayo baada ya mshtakiwa mwenzake katika kesi hiyo bwana Francis Mudhaura kueleza kuwa kesi inayo mkabili huenda ikatupiliwa mbali kwa kukosekana kwa ushahidi baada ya kesi hiyo kupigwa kalenda, kitu ambacho Kenyatta anaamini kwake pia itakuwa vivyo hivyo

"If Muthaura's case is collapsing, is that not an indication even mine will go nowhere? Alisema Bwana Kenyatta

Hatahivyo, Kauli ya Mwendesha mashtaka ya mahakama ya ICC aliosogeza mbele siku ya kusikilizwa kwa kesi hiyo kwa sababu alizo elezea kuwa ni NANUKUU “On Tuesday, Ms Bensouda said the April 10 trial start date could be pushed to August due to lack of courtrooms at The Hague and safety of witnesses.”

An August 2013 start date would therefore provide the defence with several months after receiving the delayed disclosure witnesses’ identities and unredacted materials to review those materials and conduct the associated preparations before trial begins,” she said.



Uhuru Kenyatta na mgombea mwenza Willium Ruto wanakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya kimataifa ya ICC wakihusishwa na mahafuko ya baada ya uchaguzi yaliyotokea nchini Kenya mwaka 2007 ambapo watu zaidi ya Elfu moja walifariki Dunia huku wengine wakikimbia makazi yao.

Kampeni zikiwa zinaendelea miongoni mwa wagombea wa urais nchini Kenya, wapiga kura wa nchi hiyo watamchagua mgombea wamtakaye siku ya Jumatatu March 4th ikiwa imebaki siku 4 tu uchaguzi huo kufanyika

HAKUNA MGAO WA UMEME TANESCO WAFUNGUKA, HABARI ZA KUZIMWA MITAMBO YA SONGAS, BWAWA LA MTERA YAKANUSHWA,



Shirika la umeme Tanesco limewatoa hofu wanachi kwa kukanusha juu ya kuzimwa kwa mitambo ya Songas pamoja na kukauka kwa bwala la Mtera, na kusisitiza kuwa hakuna mgao wa umeme kwa sasa, hayo yamesemwa na Bi Badra Masoud ambaye ni msemaji wa TANESCO

Pia Shirika hilo limewaomba radhi Wananchi wanaofikwa na usumbufu pindi umeme unapo katika kwani shirika hilo linadhamira ya dhati ya kutatua matatizo ya umeme nchini. Alisema Badra

“Mitambo ya Songas haita zimwa, wala Bwawa la Mtera halija kauka kiasi cha kuzima uzalishaji wa umeme katika bwawa hilo japokuwa kiwango cha uzalishaji kimepungua kutoka Megawati 80 mpaka Megawati 40 lakini aiwezi kufanya tukazima mitambo hiyo, tutatumia kiwango cha umeme kinacho patikana na sio kuzima mitambo hiyo” Alisema Bi Badra

Akifafanua zaidi juu ya swala la Kampuni ya Songas kuzima mitambo yake Bi Bibadra amesema, Kampuni hiyo tayari imepewa kiwango cha fedha ya Deni wanalo dai japo kuwa hawajamali kulipa deni hilo. Hatahivyo Bi Badra alisikitishwa na kitendo cha kampuni ya Songasi kusema kwenye vyombo vya habari kuwa inaidai Tanesco na kuwa itazima mitambo yao ilhali njia za mazungumzo kati yao inaendelea

“Sivyema kwa Songas kulalamika kwenye vyombo vya habari, kama Tanesco wameshindwa kuelewana na sisi yupo baba yetu mama yetu Wizara ya Nishati na Madini waende kule na kulalamika na madai yao yatasikilizwa lakini tayari wamelipwa kiasi fulani cha pesa” ...hakuweka wazi kiasi walicholipa.

AIDHA Tatizo lililopo hizi sasa ni marekebisho ya miundombinu ambayo yanaendelea kote nchini kwani kwamuda wa miaka 10 shirika hilo halikuwekeza kwenye miundombinu, hali inayopelekea kuwepo kwa uchakavu wa Nguzo, Nyaya na miundombinu muhimu. Alisema Bi Badra

“Hivi sasa marekebisho ya miundombinu yanaendelea maeneo mbalimbali hali inayopelekea kukatika kwa umeme, marekebisho yatachukua muda lakini tunaomba watanzania wawe wavumilivu' hali hii itaisha, kikubwa nikuweka sawa miundombinu yetu” Alisema

Sabubu ambazo Bi Badra aliziita kuwa ni UN PLANED SHUT DOWN, nimiongoni mwa matatizo yanayopelekea umeme kukatika baadhi ya maeneo akitolea mfano, kuibwa kwa nyaya za umeme, kukatika kwa nguzo za umeme, wizi wa mafuta ya transfoma na mengine mengi kama mvua kali au upepo mkali nimiongoni mwa mambo yanayopelekea umeme kukatika.

Shirka la hilo linasikitishwa na kukatoka kwa umeme hata kwa sekunde moja kwani hali iyo inapotokea uinyima mapato shirika hilo na kuieleza jamii kuwa inania ya dhati ya kuboresha matatizo yaliyopo hivi sasa, ilikuzuia matatizo ya kukatika kwa umeme

Kwa zaidi ya mwezi sasa Umeme umekuwa ukikatika katika maeneo mengi ya Jiji la Dar es Salaam, na maeneo mengine hali iliyopelekea wananchi kuhoji endapo kuna mgao wa umeme lakini Tanesco wamekanusha kuwepo kwa Mgao licha ya umeme kukatwa mara kwa mara
TCRA: WALIOKIUKA MAADILI YA HABARI WAFUNGIWA

TCRA: WALIOKIUKA MAADILI YA HABARI WAFUNGIWA


Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imevifungia Radio mbili pamoja na kipengele kimoja katika kipindi cha radioni kwa kile walichodai ni ukiukwaji wa maadili ya habari

Akizungumza na waandishi wa habari hii leo katika ukumbi wa habari maelezo jijini dar es salaa, Makamu Mwenyekiti wa tume ya maudhui kutoka TCRA Dr. Wolter Bugoya ametangaza maamuzi hayo huku akisisitiza watangazaji na waandishi wa habari kufuata maadili
Tumefungia matangazo kwa muda wa miezi sita kwa vituo viwili vya Radio, kwakukiuka maadili ua utangazaji, na kipengele kimoja tumeamuru kifutwe kabisa kutokana na kuchochea mambo mabaya katika jamii” alisema
Vituo hivyo ni pamoja na KWA NEEMA FM ambayo ipo mkoani Mwanza, ambayo imefungiwa kwa kuendesha mjadala uliokuwa ukihusisha watu wa dini gani wenye haki ya kuchinja wanyama kati ya waislamu na wakristo hali iliyo sababisha mgongano wa kiimani wa dini mpaka kupelekea mauaji na mabishano. Alisema
RADIO IMANI FM ya mkoani Morogoro, imefungiwa kwa kosa la kupnga zoezi la SENSA mwaka jana na kuwashawishi waumini wa dini ya kiislamu wasijiandikishe kwenye zoezi hilo. Alisema Dr.Buya
Aidha Kipindi cha Power Breakfast kinachoruka kila siku asubuhi katika Radio CLODS FM, kimefungiwa kabisa kipengele kinachoitwa JICHO LA NG'OMBE ambacho kinaruka kwenye kipindi hicho, ambapo licha ya kupigwa marufuku ila kimefungiwa kabisa.
Tumefungia kipengele cha jicho la ngo'mbe na kwamba kisianzishwe kingine chenye maudhuhi hayo wala kurusha kipegele kama hicho tena, kama Clouds Radio itarudia basi hatua zingine zitachukuliwa “ Alisema Dr. Buya
Hatahivyo Clouds Radio imetakiwa kulipa kiasi cha Shilingi Milioni 5 za kitanzania kama faini juu ya kile walicho dai ni uchochezi kwa mambo ya kishoga, kulingana na mada waliojadili juu ya Mtoa sala wa Nchini Marekani ambaye aliwaombea mashoga kipindi cha uchaguzi wa marekani” Alisema Dr. Buya
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA kupitia kitengo cha maudhui kimetoa onyo kwa waendesha vipindi kuwadhibiti wasikilizaji wao hasa wanapotoa maoni kwani kutofanya hivyo kutawapa mwanya kutoa maoni yaliyona uchochezi kwa jamii

KUUNDWA TUME YA KUCHUNGUZA MATOKEO MABAYA KIDATO CHA NNE 2012, WAUNGWA MKONI, MPANGO WA SEDEP NAO WAGUSIWA


Kutokana na serikali kuunda tume ya kuchunguza matokeo mabaya ya kidato cha nne 2012, Profesa. Herne Joseph Mosha kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, Amesema kuwa serikali inaumuimu wa kuunda tume kuchunguza matokeo hayo ilikuweza kupata chanzo kimoja ambacho kinazungumzia chanzo cha matokeo hayo na nini chakufanya baada ya matokeo hayo mabaya kwani sivyema kuwatumia wanasiasa katika mambo ya kitaalam

Sivyema kuwatumia wanasiasa sana japo nao wanaumuimu, ilikupata mtummoja ambaye anatoa kiini cha tatizo nilazima tume iundwe kwani serikali aiwezi kutumia maoni yakila mtu, na pia serikali inayo haki ya kuunda tume na kwahilo sioni shida” alisema Prof. Herne Mosha

Jinsi ya kutekeleza mipango ya Elimu ndio bado aijaeleweka, Hakuna ambacho akijulikani na ninaamini hawatapata kitukipya ndani ya hii tume kwani tayari vilisha wekwa kwenye tafiti mbalimbali, sera na dira mbalimbali za elimu zilisema mipango mingi na changamoto nyingi ndani ya sekta ya Elimu, kushindwa kutekeleza ndio maana bado tunarudi nyuma, alisema Prof. Herne Mosha

Aidha Profesa Herne Mosha amesema kuwa kuna haja kwa serikali kuweka Sekta ya Elimu chini ya Wizara ya Elimu tu nasio ilivyo sasa ambapo sekta hiyo ikochini ya wizara ya elimu na tamisemi kituambacho kinapunguza uwajibikaji na kufanya wizara ya elimu kutokuwa na maamuzi yamwisho hasa kwa walimu namengineyo

Hakuna ambaye anaweza kumuwajibisha mwalimu akienda kinyume na mkataba wake, wala kufuatilia kwa umakini zaidi juu ya mambo fulnai kutokana na sekta ya Elimu kuwa ndani ya Tamisemi na wakati huohuo iko Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi” Hapa napo paangaliwe, alisema Prof. Herne Mosha

Prof. Herne alisema kuwa, viashiria vya matokeo mabaya yalianza mwaka 2009 tangu serikali ilipoanza mpango wa maendeleo wa elimu ya secondary yani SEDEP ambao ulitaka kiasi cha ufaulu kianzie dara la I – III ambapo ni kwasilimia 32% mpaka asilimia 50% kwani takwimu zinaonyesha ndipo matokeo ya elimu yalipoanza kushuka. Profesa. Herne Joseph Mosha alisema

Hatahivyo, Prof Abdu Ntajuka Hamisi wa Lunga ya Kiswahili UDSM, amesema kuwa kuundwa kwa tume hiyo nimuhimu kwani tume inatoa matumaini ya kile walichokibaini kutokana na maoni ya watumbalimbali juu ya matokeo haya.

Tume italeta matokeo mazuri na yenye njia ya kufanya baada ya hili janga na kuganga yajayo, kwani nilazima wajue wanaanzia wapi, kwani awawezi kutoa msaada bila kuwa na data ya nini kifanyike” alisema Prof. Abdu Hamisi

Prof. Aliongeza kuwa, kufeli kwa wanafunzi kumanisha kilicho kusudiwa hakikufanikiwa, ama wanafunzi wamesomeshwa tofauti na mitaala, au vitabu walivyo someshwa sivyo na pengine watahiniwa awakuwa waangalifu kulinganisha masomo na mitihani

Kufeli kuna maana nyingi sana, pengine kuoanisha matokeo ya kuleta mafanikio kwenye ufaulu avikufikiwa kwani wameshindwa kufikia walicho kusudia' Alisema Prof. Abdu Hamisi

Naye mwalimu wa shule ya sekondari moja ya hapa jijini ambaye hakupenda jina lake litajwe alisisitiza kuwa serikali itegemee matokeo mabaya mwaka 2013 kwani msingi huu uliopo na ambao umewaangusha hawa waliopita bado upo na njia ya kutatua kwa sasa imechelewa, Alisema mwalimu huyo

UHURU AMPIKU RAILA ODINGA KURA ZA AWALI UCHAGUZI MKUU KENYA

Kulia ni Raila Odinga, kushoto ni Uhuru Kenyatta
Habari zilizotolewa kwenye mtandao wa Daily Nation wa Nchini Kenya masaa machache yaliyopita yanaonyesha kuwa Uhuru Kenyatta amepata kuranyingi hadi hivi sasa kuliko mpinzani wake mkubwa bwana Raila Odinga

Kura hizo zinazopigwa kupitia mtandao na taasisi ya utafiti ya SYNOVATE nchini kenya zinaonyesha kuwa mgombea huyo bwana Uhuru anaongoza kwa muda mchache sasa, tofauti na siku ya jana ambapo na siku zingine Raila Odinga alikuwa anaongoza kwa kura nyingi sana

kura zinaonyesha Uhuru Kenyatta akiwa na kura ya asilimia 44.8 huku Raila odinga akiwa na kura 44.4 ikiwa amemshinda kwa point 4 tu wakifuatiwa na wagombea wengine

NEW SYNOVATE poll shows Uhuru Kenyatta's ratings at 44.8%, higher than Raila Odinga's 44.4%. Mudavadi 5.2%, Kenneth 1.6%, Karua 0.8%.” kama ilivyo andikwa na taasisi hiyo ya utafiti

Liku chache zilizo pita bwana uhuru alitangaza kujitoa kwenye mdahalo wawagombea urais kenya kakile alichodai kuwa niupendeleo wawazi uliofanywa na waandishi wa habari walifanya nao mahojiano katika siku ya kwanza ya ya Feb. 11, ambapo swala la ukabila na kesi ya ICC inayomkabili Bwana Uhuru zilipewa nafasi kubwa.



Mdahalo mwingine unatarajiwa kufanyika tarehe 25.Feb.2013 ambapo kutakuwepo na wagombea 7 tu. Uhuru kenyatta nimiongoni mwa wakenya wanne wanaokabiliwa na kesi katika mahakama ya kivita ya ICC.

NINAHAKIKA HUYU SIMFANYAKAZI WA TANESCO IRINGA


Kwamujibu wa mtandao wa Jamii Forums, Fundi wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma akiwa amenaswa na umeme baada ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati akiendelea na matengenezo katika eneo la Mlandege mkoani humo.

Picha hii inamengi ya kuzungumzia, kama kweli ni fundi umeme basi akujipanga kwani huwezi kupanda huko juu na anajua kiasi cha umeme kinachopita hapo (Volt), bila kuweka mazingira ya thahadhari yoyote

Hajavaa kitu chochote cha kufunika umeme na miguu yake kama anavyoonekana pichani, kuanzia miguuni mikononi mpaka kichwani..... hatakama tutamtafuta mkosaji binafsi sijui ninai kwani yeye tu hakuonyesha nia ya kujisaidia

Hii iliwahi kutokea hapa Dar maeneo ya Jogoo kufuatilia sana kumbe alikuwa ni kibarua sasa TANESCO muwafundishe vibarua wenu kabla ya kuwapa ajira ninauhakika huyu simfanya kazi wa Tanesco na alikuwa kibarua tu.....

Kama nimfanya kazi kweli nina mashaka na uongozi wake pamoja na watu alioongozana nao mpaka anapanda huko juu bila hata Element,

Nakama ilikuwa inajulikana kuwa kunawatu wanafanya matengenezo haja ya kuwasha umeme ilitokana na nini mpaka umauti ukamkumba Selemani Mbuma, Tanesco wafundisheni vibarua na kuweni na mawasiliano nao ilikuepuka vifo vinavyo epukika

TANZANIA WAMFAGILIA MWAI KIBAKI, SASA OLD BAGAMOYO ROAD YAPEWA JINALAKE



 Barabara ya Old Bagamoyo imebadilishwa jina rasmi nakuitwa jina la Raisi wa Kenya anaye karibia kumaliza muda wake, Mwai Kibaki katika Uzinduzi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete akiwa pamoja na Raisi huyo mapema hii leo jijini Dar es salaam


Akiongea katika uzinduzi huo, Rais Mwai Kibaki amesema Tanzania iseme inataka nini kwa nchi hiyo, nakuongeza kuwa majina yanapokuwepo inamaana ya uhusiano mzuri kati ya nchi yetu na nchi hiyo ilikuweka kumbukumbu" Alisema Rais huyo


Barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 10.1., ikitokea makutano ya Barabara ya Rashid Kawawa hadi njia panda ya Africana na kukutana na Bagamoro Road imebadilishwa jina na Raisi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Kikwete

Uzinduzi huo umefanyika Mbeye ya Waziri wa Ujenzi Prof. John Pombe Magufuli, Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Meck Sadic na Meya wamanispaa ya Kinondoni Mstahiki Yusuf Mwenda. Na Jina la barabara hiyo imetolewa kama Eshima kwa raisi huyo anaye karibia kumaliza mda wake

Raisi Mwaikibaki amebakiza muda wa wiki mbili ilikuachia ngazi ya Uraisi wa Kenya mara baada ya Uchaguzi mkuu wa nchi hiyo kufanyika March 4 mwaka huu.

Hatahivyo baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam, walikuwa na maoni tofauti juu ya uzinduzi huo huku wakihoji nikitugani hasa,


Raisi huyo wakenya ameifanyia Tanzania kiasi cha kumpa sifa ya jina la barabara nchini Mwetu

Iddi Abdala, amesema " Bado sijajua kwa nini Raisi nawatu wake wameamua kubadilijina, nikitugani hasa ameifanyia Tanzania kiasi cha kuweka kumbukumbu au kama kuna kitu kimefichwa basi tuambiwe" Alisema Iddi


" Barabara hii inahistoria ya watumwa ambao walikuwa wakipita kupelekwa Bagamoyo enzi hizo, kuiita Mwai Kibabi inafuta historia yake, kimsingi sijaona alichokifanya Rais huyo kwa Tanzania kiasi cha kupewa jina hilo" Alisema Idd

Naye Suza Lyimo. amesema Akuna shida jina lake kuwekwa ndani ya nchi yetu akielezea kwamba sisi ni Afrika Mashariki tukiwa na umoja siombaya japo naye akujua nikwanini imeamriwa hivyo.

Watu wengi amboa Blog hii imefanyanao mahojiano walipinga sana uamuzi huo huku wakijiuliza nikitugani alichokifanya Rais huyo nchini mwetu.

Picha kwa hisani ya Michuz na IPPMedia.com

MATOKEO MABAYA KIDATO CHA NNE 2012, VYUO VYA UALIMU KUKOSA WANAFUNZI ELFU 50,000

Athari za Matokeo ya Kidato cha IV 2012: 
 
vyuo vingi kukosa wanafunzi wakudahili, kwa asilimia 50%,
huku Dira ya maendeleo ya taifa ya 2025 ikuyumba.

Reported by Dr Kitila Mkumbo
Senior Lecturer in Psychology and Education
Dean, Faculty of Education Dar es salaam University (DUCE)

Kama ilivyotarajiwa, idadi kubwa ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne mwaka jana wamefeli. Kati ya wanafunzi 367,750 waliofanya mtihani na ambao matokeo yao hayakuwa na kuzuizi, wanafunzi 240,903 wamefeli kwa kupata daraja la 0 (Tazama umbo Na.1). Hii ni sawa na asilimia 65.5 ya wanafunzi wote waliofanya mtihani wa kidato cha nne.


Aidha wanafunzi 103,327 ‘wamefaulu’ kwa kiwango cha daraja la nne, ambao ni sawa na asilimia 28.1 (Tazama Umbo Na. 2). Kitaaluma, hawa nao wamefeli kwa sababu kwa mfumo wa elimu wa Tanzania kwa sasa ngazi nyingi za elimu baada ya kidato cha nne kinahitaji ufaulu wa kiwango cha chini cha daraja la tatu. Kwa hivyo ukijumlisha idadi ya wanafunzi waliopata daraja la IV na 0 unapata wanafu
 
344,230 waliofeli kwa kiwango cha daraja la IV na 0; idadi hii ni sawa na asilimia 94 (Tazama Umbo Na. 2)!! Kwa hiyo ni asimia sita (6) pekee ya wanafunzi waliopata madaraja ya I, II na III na ambao kimsingi ndio wenye sifa za kujiunga na ngazi mbalimbali za elimu baada ya kidato cha nne.

Pamoja na kwamba watu wengi wameonekana kushtushwa na matokeo haya, akiwemo waziri mwenye dhamana ya elimu nchini, kwa wataalamu na wafuatiliaji makini wa mambo ya elimu matokeo haya hayashangazi. Tatizo moja la sisi

watanzania tumekuwa ni watu wa kusubiri matokeo na kutokujali sana mchakato unaoletekeza matokeo hayo. Sote tunajua kwamba hizi shule zinazoitwa shule za sekondari kimsingi nyingi zao hazina hata sifa ya shule nzuri ya shule ya msingi.

Utafiti wa karibuni unaonyesha kwamba ni asilimia nne tu ya shule zote za sekondari nchini ndio zenye kukidhi vigezo vya chini kabisa vya shule ya sekondari. Sote tunatambua kuwa walimu siku hizi hawana moyo wa kufundisha baada ya kupuuzwa na kudharauliwa kwa muda mrefu. Walipojaribu kugoma mwaka jana wakatishwa na kusimangwa na mwajiri wao.

Wakarudi madarasani wakiwa wamenuna na wakatuwaaambia waziwazi kwamba ‘mtaona’. Baadhi ya walimu wakadiriki hata kusema kwamba watafundisha madudu na mwalimu mmojawapo akatoa mfano ubaoni kuwa watafundisha ‘7+7=77’. Badala ya kuungana na walimu kuibana serikali sote tukanywea, na mitihani ilipokaribia tukaenda madhahabuni kumuomba Mungu ili watoto wetu wafaulu mitihani yao.

 Matokeo ya mwaka huu ni mabaya zaidi kutokea tangu nchi yetu ianze kuwa na mfumo wa elimu wa kidato cha nne. Haijawahi kutokea hata mwaka mmoja wanafunzi wa kidato cha nne wakafeli kwa kiwango hiki. Kiwango kibaya cha kufaulu kilikuwa mwaka 2010 ambapo asilimia 50.4 tu ya wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne ndio waliofaulu, wakati asilimia 49.6 walifeli (Tazama umbo Na. 3). Ukichunguza kwa makini utaona kwamba kiwango cha kufaulu kilianza kushuka zaidi baada ya wanafunzi waliopitia mfumo wa shule za sekondari za kata walipoanza kumaliza, hasa kuanzia mwaka 2010, tulipoanza rasmi kutekeleza sera ya ‘wingi kwanza ubora baadaye’.

ADHARI ZA MUDA MREFU NA MFUPI

Matokeo haya, kama yalivyokuwa ya miaka ya nyuma, yana athari nyingi, za muda mfupi na muda mrefu ujao. Kwa muda mrefu ujao, matokeo haya yanafifisha azima ya taifa ya kuwa na taifa la watu walioelimika ifikapo mwaka 2025 kama ilivyoanishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025.

Kwa matokeo haya na mengine ya miaka mitatu iliyopita, mfumo wetu wa elimu ya sekondari (na hata msingi) unatutengenezea taifa la watu mbumbumbu ambao itakuwa vigumu kuwafanya waamini katika sayansi, achalia mbali wao wenyewe kuibuka kuwa wana sayansi.
  
Lakini pengine athari ambazo zitaanza kuonekana sasa hivi ni shule na vyuo kuanza kukosa wanafunzi wa kudahili. Kwa mfano, idadi ya wanafunzi wanaohitajika kujiunga na mafunzo ya ualimu ngazi ya cheti na kidato cha tano kwa mwaka huu ni zaidi ya 50,000, lakini ni wanafunzi 23,520 tu waliomaiza mwaka jana ndio wenye sifa za kujiunga na taasisi hizi za elimu. 

Hivyo kutakuwa na upungufu wa wanafunzi zaidi ya asilimia 50 wa kujiunga katika vyuo vya ualimu ngazi ya cheti na kidato cha tano ukizingatia kwamba sifa ya chini ya kujiunga na ngazi hizi za elimu ni kidato cha nne na ufaulu wa kiwango cha daraja la tatu. 

Ni wanafunzi hawa waliomaliza mwaka jana wanaotarajiwa kujiunga na vyuo vya elimu ya juu ifikapo mwaka 2015. Kwa upande wa vyuo vikuu pekee, kutakuwa na nafasi zisizopungua 27068 mwaka 2015. 

Hata kama wanafunzi wote waliofaulu kwa kiwango cha daraja la I-III wataenda kidato cha tano na wote hawa wakafaulu mtihani wa kidato cha sita mwaka 2015, bado hawataweza kujaza nafasi za vyuo vikuu zitakazokuwepo mwaka 2015. (tazama maumbo Na. 4 na 5).

Hata hivyo, kwa maoni yangu, hatari kubwa inayotukabiri sio ubaya wa matokeo haya. Hatari kubwa ni kutokujali kwetu. Tena katika hili la elimu ndio kabisa litapita upesi kwa sababu wengi tunaopiga hizi kelele watoto wetu ni miongoni mwa hao asilimia mbili waliopata madaraja ya I na II na ambao wanahudhuria mfumo tofauti kabisa wa elimu! Tutapiga vikelele kidogo kisha tutanyamaza tukisubiri matokeo mengine pengine mabaya zaidi mwakani tusipochukua hatua yeyote ya maana. 

Na hatua ya kwanza ya maana kabisa na ya muda mfupi ni kuwajali walimu. Katika bajeti ijayo serikali iwaongezee walimu mishahara angalau mara mbili ya wanaopata sasa hivi. Tukichukua hatua hii tutaanza kuanza matokeo tofauti. Nimesema mara zote na narudia tena leo kwamba elimu bora ni walimu bora. Hatua za muda mrefu ni kuuangalia upya mfumo wetu wa elimu. Hili litahitaji wataalamu wa elimu waweke vichwa vyao chini. Lakini hili haliwezekani kama serikali yetu itaendelea na sera yake ya ‘wingi kwanza, ubora baadaye’!


Mwandishi wa Makala haya ni Mhadhiri Mwandamizi katika Elimu na Saikolojia
na Mkuu wa Kitivo cha Elimu katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Dar es
Salaam (DUCE).

ASILIMIA 60 WALIOPATA SIFURI WAZIDI KUMLIZA MBATIA, ASISITIZA MITAALA NI TATIZO



Kushoto,Waziri wa Elimu Mhe.Shukuru Kawambwa, Kulia Naibu wake Mhe. Philip Mulugo


Kufuatia matokeo mabaya ya mitihani kidato cha nne 2012, Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi na Mbunge wa kuteuliwa Mhe. James Mbatia amesikitishwa na kiwango hicho na kusema kuwa hali hiyo nikukosa usukani kwa elimu ya Tanzania.

Mbeshimiwa Mbatia amesema hayo hii leo ofisini kwake jiji Dar es salaam, akiongea na waandishi wa habari, ambapo alisisitiza elimu kuporomoka.
 
Elimu ya Tanzania inaporomoka kwa kukosa usukani na mwelekeo, kama maswala haya hayatachukuliwa maanani swala la elimu litaendelea kuwa kikwazo” Amesema Mbatia.

Akiongelea swala la wastani waufaulu ambapo asilimia 60 wamepata ziro (Divisio 0 ), asilimia 20 wamepata daraja la nne (Division IV), asilimia iliyobaki haiwezi kukuza elimya ya Tanzania na kwamba hali hiyo ni msiba kwa Taifa.

Mhe. Mbatia amesema, sababu inayosababisha hali hiyo ni mfumo mbovu usioeleweka wa Elimu pamoja na mitaala ya Elimu nchini ambayo inawaongoza wanafunzi juu ya Elimu yao, alisema.

Hakuna mitaala inayoeleweka ya elimu nchini, pamoja na iliyopo hivi sasa hii ndi inachangia elimu kuyumba, huku akiongea kwa masikitiko makubwa” alisema Mbatia.

James Mbatia kulia
 Aidha, Mbatia amesisitisa sana juu ya mitaala iliyowasilishwa Bungeni kikao kilicho pita na Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa kuwa imechakachuliwa na sio halisi



 
Mitaala hii sio halisi huku akikionyesha kwa wanahabari, aina no. ya ISB, aina Nembo ya Taifa ya adam na hawa pamoja na saini hata ya mmiliki wake” alisema Mbatia

Matokeo ya kidato cha nne yalitangazwa jana na waziri wa elimu, huku wanafunzi Elfu 1641 tu ndio waliopata Division I, Elfu 6453 ndio wenye division II, Elfu 15,426 Division III, huku laki 103,327 wakipata Division IV na Laki 240,903 wakipata Division 0.

AMANI NI HAZINA KUBWA.....UMOJA WETU TUNAMPA NANI TANZANIA?

Tanzania ninchi iliyo shinda ukabila, tusikubali kumpa mtu amani yetu kwa garama ya mauti ya Taifa letu, Uzao wetu na Hazina yetupamoja na utuwetu kupotea, Tumeushinda ukabila kwakishindo kwa nini udini utuvuruge kisha kugawa umoja wetu

Kwa miezi ya hivi karibuni kume kuwa na matukio ya uvunjifu wa amani yakiambatana na mauaji ya watu wasio kuwa na hatia yanayofanywa na watu wanajulikana kama " WAHUNI" ambao wanania yakulipeleka taifa pabaya....inasikitrisha kusema ni matukio ya kiimani au yakidini kutokana na wanaolengwa ni viongozi wa dini

Kila mtu anajua historia ya Taifa letu kwakuwa na amani na utulivu tangu uhuru, Hawa wahuni wachache wanaotaka kugeuza Tanzania kuwa Nigeria au nchinyingine yenye mfano sawa na huu. Kama ni "SIASA" Basi wapande majukwaani nafasi hipo, kama ni Harakati basi zitambulike taasisi iweya huru na haki kwa wote kuliko kuimiza machafuko na mauaji yasio na faida yoyote

Naamini kuwa, wanaotamani amani yetu na utulizu wetu wanatumiwa kutuvuruga, Yanayoendelea Tanzania Visiwani (Zanzibar) yanawengi nyuma yake. hao ni wachache tuliowengi hatuungi mkono vitendo hivi kuanzia Zanzibar hadi Bara kwani hatuna mafungamano nao na hii itawafanya hao wachache wasipate mwanya wakutuvuruga kabisa..tusikubali kupoteza utuwetu

Nijuacho sisi ni kitu kimoja Tanzania ni moja na ni nchi ya amani, tusikubali haya "AMANI'' ni utajiri mkubwa hata kuliko mengi tuliojaliwa ndani ya nchi yetu, kinachoendelea kaa mauaji na kuchoma kanisa sio ukombozi bali ni utumwa wawabaya wetu tuukatae tusishiriki nao bali tuongeze nguvu kukemea na kumaliza mauaji ili amani idumu kwetu

WARAKA WAKUPUUZWA HUU HAPA
Sijambo jema nimepita katika mitandao ya kijamaii nakupata waraka huu ambao siwaheri lakini haya tusiyape nafasi kwani sisi niwalinzi wa nchiyetu na wote tunawajibika..... PINGA ...PINGA DUMISHA AMANI TUSIUZE AMANI KWA ADUI WETU..TANZANIA MOJA (zanzibar and Tanganyika milele)
WIZARA YA ELIMU IAMISHIWE OFISI YA RAISI, WAZIRI WA ELIMU NAYE AWAJIBIKE KISA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012: ZITTO ANENA

WIZARA YA ELIMU IAMISHIWE OFISI YA RAISI, WAZIRI WA ELIMU NAYE AWAJIBIKE KISA MATOKEO KIDATO CHA NNE 2012: ZITTO ANENA


> SIFURI ZA MTISHA ZITTO
> ASISITIZA WIZARA YA ELIMU IAMISHIWE OFISI YA RAISI
> AMTAKA WAZIRI AWAJIBISHWE
> AHOJI JUU YA ELIMU YA VYUO VYA UFUNDI, AKITABIRI TAIFA LA MAMBUMBUMBU
> ASISITIZA BILA ELIMU NIBURE

Taarifa ambayo Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe ameiandika kwenye ukurasa wake wamitandao ya kijamii,kuusiana na matokeo ya kidato cha nne 2012, ambapo mbunge huyo ameitaka wizara ya Elimu kuwajibishwa na kuiamisha kwenda ofisi ya raisi

Tarifa ya Zitto inasema, Matokeo ya Kidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu kupata sifuri) na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne na daraja la sifuri kwa mwaka wa tatu

Zitto amesema kuwa,Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna, Najua kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya mabadiliko. amesema zitto

Aidha amesema, Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu, yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka. kwani kwa kutofanya hivyo mwakani pia haya yatajirudia.

Mhe. Zitto ameendelea kusema, Mwaka jana tulisema mpango wa kujenga vyuo vya ufundi kila Halmashauri ya Wilaya uanze mara moja. Katika Bajeti Kivuli mwaka 2011 tulipiga hesabu kwamba tunahitaji tshs 720 bilioni katika kipindi cha miaka 5 ijayo kujenga vyuo vya ufundi vya VETA kila Wilaya. 

Aliongeza kuwa, Tukawaambia badala ya kukopa kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kulipana posho ni vema tukope kuwekeza kwenye elimu maana Elimu ni Hifadhi ya Jamii. Elimu yetu ya sasa inazalisha matabaka kwenye jamii na ni hatari sana kwa uhai wa Taifa.

Aidha, Tunaweza kujidai kujenga madaraja na miji mipya. Tunaweza kujidai kujenga mabomba ya gesi na kusambaza umeme kila kijiji mpaka kwenye vyoo. Kama hakuna Elimu haya yote ni bure kabisa. Hata kukosa uvumilivu wa kiimani sasa hali itakuwa mbaya zaidi unapokuwa na Taifa la mambumbumbu. Waziri Shukuru Kawambwa na wenzake watoke. Watoke SASAalimalizia Zitto 
 
UBORA NA UFAULU KWA DARAJA KIDATO CHA NNE 2012

DARAJA
(division)
IDADI YA WAVULANA IDADI YA WASICHANA JUMLA
I 1073 568 1641
II 4456 1997 6453
III 10813 4613 15426
IV 64344 38983 103327
0 120664 120239 24090

Idadi ya matokeo kama ilivyo kwenye jedwari nikwamba wanafunzi waliopata Division I ni Elfu 1641 katika taifa zima, waliopata Division II ni Elfu 6453, Division III ni Elfu15,426, Division IV ni Laki103,327 huku Division 0 ni Laki 240,903 matokeo ya kidato cha nne 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YATOKA, WASICHANA WABURUZWA, MATUSI NA UDANGANYIFU VYA JIRUDIA TENA



Matokeo ya kidato cha nne 20012 yametoka hii leo, huku wasichana wakiwa wameburuzwa sana na wavulana kwa kiwango cha ufaulu. Matokeo hayo yametangazwa katika wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi jijini Dar es salaam na waziri wa wizara hiyo Mhe. Shukuru Kawambwa

Octoba mwaka jana, Jumla ya watahiniwa Laki 126, 847 elfu walifanya mtihani huo, waliofaulu ni wanafunzi 397,136 huku wasichana wakiwa ni Elfu 46 na161 na wavulana niElfu 80 na 686. idadi inayofanya wavulana kuwajuu zaidi ya ile ya wasichana

Waziri amesema, Jumla ya watahiniwa Elfu 23, mia 520 wamefaulu katika daraja la I-III ambapo katiyao wasichana ni Elfu 7,178 na wavulana ni Elfu 16,342 ambapo wasichana wameburuzwa kawa kiasi kikubwa pia

Shule 10 zilizofanya vizuri ni, St. Francis Girls iliyopo Mbeya, Marian Boys iliyopo Pwani, Feza Boys iliyopo Dar, Marian Girls iliyopo Pwani, Rosmini iliyopo Tanga, Canosa iliyopo Dar, Jude Moshono iliyopo Arusha, St.Marys mazinde juu iliyopo Tanga, Anwarite Girls iliyopo Kilimanjaro na Kifungilo Girls iliyopo Tanga

Shule 10 zilizofanya vibaya ni Mibuyuni – Lindi, Ndame – Unguja, Mamndimkongo – Pwani, Chitekete – Mtwara, Maendeleo – Dar es salaam, Kwamndolwa – Tanga, Ungulu – Morogoro, Kikale – Pwani, Nkumba – Tanga na Tongoni pia kutoka Tanga

Wanafunzi 24, wamefutiwa mitihani yao kwa sababu ya kuandika matusi katika script zao, “ Waziri amesema kutokana na kosa hilo baraza la mitihani limefuta matokeo yao yote kwa mujibu wa kifungu cha 6 (2)a cha kanuni za mitihani”.

Akitoa tadhmini ya ufaulu wa mitihani hiyo, Waziri amesema shule zilizo fanya vibaya zaidi nizile za vijini ambazo hazina kabisa walimi, miundombinu ni mibovu, hakuna maabara kwaajili ya masomo ya sayansi, kuna ubungufu mkubwa wavitabu na changamoto mbalimbali

“ Shule hizi zilizofanya vibaya zinachanga moto nyingi kama nilivyo taja na Serikali inajitahidi kuzuia changamoto hizo ilikukabiliana nayo, kwa kuajiri walimu wapya Elfu 13,246 ” Alisema Waziri

MWANAFUNZI BORA HAJAWEKWA HADHARANI

Katika hali ya kushangaza Wizara haikuweza kumuweka hadharani mwanafunzi bora wa mwaka 2012 wa kidato cha nne kama inavyo fanya miaka yote, akijibu swali lililo ulizwa na mwandishi wa habari katika mkutano huo waziri amesema

“ Sikuweza kuandaa nimwanafunzi yupi ameshika nafasi ya kwanza kutokana na wengi kugongana kwa alama, lakini niombe samahani kwa hilo na mtajulishwa baadae” Alisema waziri

Aidha aikutolewa tadhmini ya ufaulu kwa mwaka 2011 na hii ya 20012 kwa kidato cha nne ilikujua kama kiwango kimeshuka au laah. TAKWIMU AMBAZO KILA MWAKA HUTOLEWA

PINGAMIZI LINGINE KWA UHURU NA RUTO, UCHAGUZI MKUU KENYA

Kenya Human Rights Commission (KHRC) chairman Makau Mutua (right) and Executive Director Atsango Chesoni (left) during a press conference in Nairobi February 16, 2013. KHRC said it will not relent in ensuring Uhuru Kenyatta and William Ruto do not assume office if elected. ANTHONY OMUYA


HASASI za kiraia zinazo tetea haki za binadamu nchini Kenya, zimewakilisha pingamizi jingine kuwazuia Willium Ruto na Uhuru Kenyata ambao ni washukiwa wa mauaji katika mahakama ya ICC watakaogombea urais wan chi hiyo, kuwa wakishinda hawata kubali waingie ofisini nakufanya kazi za kiserikali
 
Habari zilizoandikwa na vyombo vya habari nchini Humo zinasema, Hasasi hizo zimetoa mapingamizi yao, kwa mara nyingine baada ya Mahakama Kuu ya Kenya kushindwa kutoa uamuzi kama wawili hao wanaruhusiwa kugombea nafasi ya uraisi ama laa, hali inayo wapa nafasi kubwa wagombea hao kitukinacho pingwa vikali na hasasi hizo

Kushoto ni Uhuru Kenyata, kulia ni Willium Ruto

Hasasi hizo zinazojulikana kama The Kenya Human Right Commission (KHRC), na Kenyans For Peace with Trueth and Justice (KPTJ) wamepinga uamuzi wa mahakama kwakile walicho daia inaongoza kinyume na maslahi ya jamii

Uhuru Kenyata na Willium Ruto,ambao niwagombea katika wa uraisi katika uchaguzi mkuu wan chi hiyo ambao unatarajiwa kufanyika wikimbili zijazo tarehe 4. 3. 2013, huku wakiwa wanatuhumiwa katika mahakama ya uhalifu ya ICC kwa kuhusika na gasia zilizoshuhudiwa baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007

Kategori

Kategori