WALIO ONJA JOTO YA JIWE 2012, NA WATANZANIA KUWAOMBEA SANA KWA MUNGU ILI AWALINDE NA KUWAEPUSHA NA MABAYA ZAIDI HAWA HAPA

STEVEN ULIMBOKA
Huyu alikuwa Raisi wa Madaktari nchini, alijeruhiwa vibaya na nusura kuuwawa na watu wasio julikana taree 
************************************************************************************
ELIZABETH MICHAEL A.K.A LULU 

Msanii Lulu ni miongoni mwa watu walio onja joto la jiwe na kuombewa sana na watanzania wote iliaweze kuepuka mkosi wa kwenda jela kwa kosa la kuua bila kukusudia msanii mwenzake mareemu Steven Kanumba.


***********************************************************************************
     Wengine ni Sajuki, Vengu na Kajala hawapo pichani.. hawa wote ni wasanii wa kibongo ambao nao watanzania waliwatupia macho na kutoa msaada wao kwa namna moja au nyingine
WALIO TUTOKA MWAKA 2012 NA KUACHA HISTORIA AMBAYO AITASAAULIKA KWENYE VICHWA VYA WATANZANIA WENGI, KWANI VIFO VYAO VILISHTUA WATU WENGI SANA NA KUACHA MAJOZI MAKUBWA 

                    DAVID MWANGOSI MWANDIHI WA HABARI 

DAVID MWANGOSI, aliuwawa na polisi katika kijiji cha nyololo mkoani Iringa, alipokuwa anachukua Habari katika mkutano wa chama cha Democrasia na Maendeleo Chadema, ilikuwa September 2. 2012
HAPO POLISI WAKITEKELEZA MAUAJI YA DAVID MWANGOSI

****************************************************************************

STEVEN KANUMBA ALIYE KUWA MSANII WAMAIGIZO, BONGO MOVIE

STEVEN KANUMBA, alifariki gafla April 7.2012 nyumbani kwake Sinza jijini Dar es salaam na mazishi yake kuudhuriwa na watu zaidi ya elfu 30,000. Kifo cha msanii huyo kiliusishwa na msanii mwenzake LULU kwa kisa cha wivu wa mapenzi

Picha ikuonyesha jeneza la mareemu Kanumba na umati mkubwa wa watu wlioudhuria mazishi hayo Kinondoni

**************************************************************************
 SHARO MILIONEA


MSANII wa maigizo ya vichekesho Sharo Milionea alifariki Nov. 27 2012 kwa ajali ya gari. Mareemu alikuwa akielekea mkoani Tanga na alipofika Muheza alipata ajali na kufariki papo hapo

Hao ni miongoni mwa watu walio make headline baada ya vifo vyao kutokea, kutokana na mapenzi na ushabiki mkubwa kwenye jamii ya watanzania.

Nimiongoni mwa vifo vilivyo jaza vichwa vya habari na magazeti nchini







ANALOGIA KUZIMWA DAR ES SALAAM, TCRA WASISITIZA MASAA MACHACHE YALIYO BAKI, WAKAZI WA DAR NAO WAHAHA KWENYE FOLENI NDEFU KUSUBIRI HUDUMA HIYO

KAMA inavyoonekana pichani, kwenye vituo vyote ambako huduma ya ving'amuzi hupatikana kumekuwa na foleni kubwa tangu asubuhi yaleo kufuatia zoezi la kuzima mitambo ya ANALOGIA ilikuamia DIGITALI kutarajiwa kufanyika hii leo usiku saa sita kamili

Mkoa ambao utaanza kuzimwa ni JIJI LA DAR ES SALAA, Ikifuatiwa na mikoa mingine nchini. Msemaji wa TCRA Inocent Mungi amesema zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kusisitiza kuzima mitambo hiyo ifikapo saa 12.00 kamili usiku

Aidha, amesema kuusu ubora wa huduma itakayo patika ni ya uhakika na kuwaomba wananchi wanao ishi maeneo ya mabonde kuhakikisha wana Antena mbili ya ndani na yanje ilikuweza kupata stasheni bila chenga

WATANZANIA WAKO MILLIONI 44.9, JK ATANGAZA LEO UWANJA WA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM



RAIS Jakaya Kikwete ametangaza idadi ya watanzania ambapo amesema kwamba jumla ya watanzania 44929002 ambao ni sawa na (44.9)milioni, huku akisema kwamba idadi ya watanzania wote wanaoishi Tanzania Bara ni 43625434 na visiwa vya Zanzibar na Unguja ni 1303568.

Idadi ya Watanzania wote ni Millioni 44 929 002, ambayo ni sawa na milioni 44.9, matokeo hayo yametajwa na RAISI wa Jamuuri ya muungano wa Tanzania JAKAYA KIKWETE, katika uzindizi wa matokeo ya Sensa 2012. 

Aidha Tanzania bara inajumla ya watu Milioni 43.625.434, huku Tanzania Visiwani Zanzibar kuna watu Milioni 1.303.568. Idadi ya watanzani ainaongezeka kwa kasi ndani ya miaka 10 ambayo watu huesabiwa

Sensa ya Kwanza Tanzania ilianza mwaka 1967 mara baada ya Uhuru, ikifuatiwa na mwaka 1978, 1988, 2002 na 2012, Zoezi la Kuesabu watu nchini hufanyika kila baada ya Miaka 10

IDADI YA WATANZANIA KUJULIKANA LEO


RAISI wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo atatoa matokea ya Idadi ya Watu nchini, uliofanyika kwenye SENSA 2012 tangu August 26 mwaka huu. Mkutano unaofanyika katika viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam

Idadi ya awali ya watu Tanzania ilikuwa Milioni 42 baada ya sensa iliyofanyika mwaka 2002. matokeo mapya kutajwa leo ilikujua kama watanzania wameongezeka au laa kutoka kwenye idadi iliyo pita

DIAMOND AUKANA U FREEMASON, AWASHANGAA WANAOENEZA KUWA KABADILI DINI



Msanii anaye Ng'ara katika Tasnia ya Muziki wa Bongo Fleva hivi sasa, Diamond Plantum amekana kushiriki wala kujihusisha na imani inayousishwa na nguvu za giza ya "Freemason", na kusikitishwa sana na watu wanao sambaza maneno ya kuwa yeye amebadili dini.

"Mimi sijawahi kujiusisha na imani ya Freemason na wala sijui juu ya hilo kabisaa, Nimelelewa katika imani ya Kiislamu na ninacho juwa nikuwa Mungu ni mmoja....Siwezi Kuwa Freemason Hata siku moja"Alisema Diamond.

Akiongea na Campasvision Diamond, alisema Zaidi ameumizwa sana na kusikitishwa sana na habari zinazo zagaa kuwa yeye kabadili dini, kitu ambacho sio kweli..alisisitiza kuwa awezi kuiacha dini yake na kuwa na imani tofauti na aliyo lelelwa na kudai kuumizwa na watu wanao eneza habari hizo, Alisema Diamond

Vijana wanaoiga na Kukopi kazi zangu, kimsingi nafrahishwa sana tena inanipa nguvu yakuwa kazi zangu zinakubaliwa  hata nawasanii wenzangu, Swala ambali linanifanya niongeze juhudi zaidi katika kuboresha kazi yangu. Alisema Diamond

Akiongelea juu ya Video Mpya ya Kesho Diamond alisema, amefurahishwa sana na Wimbo huo kwani ni miongoni mwa nyimbo ambazo Mashahiri yake hayakumpa shida kutunga kabisa kwa ilikuwa kama masihara lakini kilichotoka nikitu ambacho kimesimama. Alimalizia Diamond

MAPYA YA IBUKA KIFO CHA MTU ALIYE TAKA KUCHOMA NYUMBA YA CHAMELEONE, MSALA WA MGEUKIA YEYE

 
 
Baba mzazi wa mtu aliyejulikana kama Robert Karamagi ambaye alifariki kutokana na majeraha ya kuungua kwa moto baada ya kujaribu kuchoma nyumba ya msanii Jose Chameleone wa Uganda, yameibuka mapya baada ya Familia ya mtu huyo judai kuwa Marehemu alichomwa na moto wa Petroli

Karamagi aliyekuwa na umri wa miaka 27 alifariki katika hospitali ya Mulago, baada ya kujeruhiwa vibaya na moto nyumbani kwa Chameleone, Huku mke wa msanii huyo akisisitiza kuwa mareemu alijiunguza mwenyewe kwa moto

Baba wa marehemu  Robert, Meja Benedict Kyamanywa amepingana na ripoti kuwa mwanawe alijichoma moto mwenyewe. na kuongeza kuwa mwanae anajulikana katika kijiji kizima kuwa ni kichaa huku akisisitiza kuwa swala hilo Msanii Jose Chameleone analijua

SUKARI YA TANZANIA KUCHUNGUZWA NCHINI KENYA


Bodi ya sukari nchini Kenya (KSB) imeanza mchakato wa kuchunguza sukari kutoka nchini Tanzania na Uganda baada ya takwimu kuonyesha kwamba uingizaji wa sukari kutoka nchizi  hizo mbili kuongezeka sana kwa miezi michache iliyopita 

Mapema mwezi huu KSB iliyapiga makampuni mbalimbali ya Tanzania na Uganda kuingiza sukari nchini humo, Hatahivyo bodi hiyo ililegeza msimamo wake ilikupisha sikukuu za Christmas kupita, huku wakifanya uchunguzi wasiku chache na mamlaka za Tanzania na Uganda.

Kwa mujibu wa Jarida la Daily Nation la Kenya, Mkurugenzi wa bodi ya KSB Bi Rosemary M'kok amesema kwamba Bodi yake ina mamlaka ya kuchunguza ubora na uingizwaji holela wa sukari nchini humo, nakudai kuamini kuwa wafanyabiashara wa Kenya na Uganda wengi awana uaminifu

Kwamujibu wa takwimu, uingizaji wa sukari toka Uganda umeongezeka toka Tani 73 mpaka tani 30elfu kwa miezi 11 mwaka huu. Huku Tanzania ikiwa imesafirisha tani 504 kwa miezi 11 kuwenda nchini Kenya. alisema Bi. Rosemary

JOSEPH CHAMELEONE ANUSURIKA KIFO SIKU YA BOXING DAY 2012


Joseph Chamilione na mkewe Daniella
Msanii maarufu wa nchini Uganda Joseph Chameleone na mkewe Daniela, jana walinusurika kufa baada ya mtu mmoja kuvamia nyumba hiyo akiwa na Petroli kwa lengo la kumuua msanii huyo, lakini akiwa kwenye hazma ya kutekeleza tukio hilo moto wa Petroli aliotaka kuwachoma na ndani ya nyumba ya msanii huyo uli muunguza vibaya mtu aliyetaka kufanya tukio hilo

ALIYE JARIBU KUMUUA MSAANI WA UGANDA JOSEPH CHAMELEONE AFARIKI DUNIA

Mtu huyo aliye fariki masaa mawili yaliyo pita, Akipatiwa matibabu amefaamika kwa jina la Robert Kalamagi mwenye umri wa miaka 27, mkazi wa Seguku Kampala Uganda, amefikwa na umauti baada ya kujeruhiwa vibaya na moto wa petroli ambao alikuwa akijaribu kumwagia mke wa msanii huyo,

Daniela ambaye ni mke wa Chameleone, aliwaambia wa andishi wa Habari kuwa, Asubuhi ya Boxing Day alisikia vishindo sebuleni, wakati akiwa chumbani na alipojaribu kujua ninani, aligundua ni nani alimkuta marehemu na akajaribu kumuuliza anataka nini lakini akumjibu chochote, Alisema Daniela.

Aidha mke wa Msanii huyo alimuita Chameleone, ndipo mtu huyo alichukua geleni la lita tano kwa lengo la kumwagia Daniela, kinyume na matarajio yake petroli ilimwagikia yeye na alipo washa moto, aliungua kiasi cha kufanya mtu huyo kujeruhiwa vibaya na moto huo, Daniela anasema mtu huyo aliomba msaada alipokuwa anaungua na moto huo.

Kilicho washangaza watu wengi wa nchini Uganda ni baada ya mtuhumiwa kuwaeleza Polisi alipofanyiwa Mahojiano akiwa Hospitali kuwa, yeye ni shabiki mkubwa wa msanii huyo, na kilichotokea kwake alitumwa na mtu ilikumuua msanii huyo


Hatahivyo Polisi wa nchini humo wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo kubaini kama hilo nitukio la ujambazi au alitumwa na mtu kutekeleza tukio hilo

PICHA YA SIKU


KUTOKA KUSHOTO NI NOAH LALTAIKA MTANGAZAJI WA KURASA (EATV) KATIKATI NI WILBROD SLAAA KATIBU MKUU WA CHAMA CHA CHADEMA, KULIA NI CEO WA CAMPASVISION BLOG LOYCE JOSEPH

Picha ya siku, ambayo inamuonyesha Katibu Mkuu wa chama cha Demokrasia na maendeleo Mheshimiwa Dk.Wilbrod Slaa pamoja na Mtangazaji wa kipindi cha KURASA kinachorushwa na Televisheni ya EATV, pamoja na Reseacher wa EATV na CEO wa Blog ya CAMPASVISION Miss Loyce Akoth Joseph. 

Wanahabari tukiwa mzigoni kusaka habari, kuna muda tunakutana na kufanya kazi kwa karibu sana na viongozi wetu

picha zaidi ingia
Link ya Photo 

RABA ZENYE NEMBO YA CCM HIVI HAPA

Watu na itkadi na chama chao- kiatu chenye nembo ya CCM

Kiongozi mmoja wa chama cha Mapinduzi CCM, anayesadikiwa kuwa ni Mhe. Godfrey Zambi Mbunge wa Mbozi Mashariki na M/Kiti wa CCM Mkoani wa Mbeya. Akiwa amevaliya Raba zenye chata au Nembo ya Chama cha CCM ambayo pia utumika kwenye Bendera ya Chama hicho

Picha hii kwa hisani ya~~~
www.mbeyayetu.blogspot.com

BAR 248 ZINAZO PATIKANA ENEO LA SINZA AZINA VYUMBA VYA KUIFADHI WALIOLEWA KUPINDUKIA

Barabara ya Shekilango mpaka Bamaga, eneo la Sinza, imebainika kuwa na Bar zinazo fika 250, baada ya mtandao wa kuzuia matumizi mabaya ya Pombe (Tanzania Network Against Alcohol- TANETS) kufanya utafiti katika kata 18 za jiji la Dar es Salaam.

Utafiti huo ulifanywa kwa muda wa wiki tatu, na miongoni mwa kata hizo ni Tandale, Mabibo, Mwenge, Kawe, Manzese, Ubungo, na Shekilango, umebaini kuwa eneo la Sinza ndilo linaloongoza kuwa na Bar nyingi zaidi, huku kukiwa na usalama mdogo wa kuwaifadhi waliolewa kupindukia

Tarifa hiyo imetolewa na Katibu Muoenezi wa TANETS, bwana Mathias Kimario, baada ya taasisi hiyo kutaka kujua juu ya kuzagaa na unywaji holela wa pombe katika jiji la Dar es Salaam

Bwana, Mathias alisema, miongoni mwa bar zote 250 zilizo fanyiwa utafiti katika eneo la Sinza bara bara ya Shekilango mpaka Bamaga, ni Bar Mbili tu Ndio zina vyumba maalumu kwaajili ya kuifadhi watu waliolewa kupindukia, na zilizo baki Walevi hutolewa nje bila kusaidiwa mahali pa kupumzikia 

" Bar mbili tu ndio zina vyumba maalum kwa ajili ya walevi kupindukia na kuwajali wateja wao wanapokuwa awajitambui kwaajili ya Pombe yani, 'Responsible Beverage Services', lakini zilizo baki azina huduma hiyo kitu ambacho uhatarisha maisha ya yule aliye lewa" alisema Mathias

Mwanamke anatakiwa kunywa pombe mbili tu, kutokana na kuwa na mafuta mengi mwilini, na kwa wanaume ni pombe 3 tu, kwakuwa wana maji mengi mwilini hivyo uwezo wakuchuja pombe ni mkubwa kuliko wanawake wenye mafuta mengi,  Alisema Mathias kutokana na tafiti mbalimbali zlizo fanywa nchi za Marekani.

Alisema, Kiwango cha watumiaji wa Pombe ni kikubwa sana, kwani utafiti unaonyesha watu 90 ambao wanatumia Pombe kila siku hunywa pombe zaidi ya 5 mpaka 6, kiwango ambacho nikikubwa sana na kusisitiza Watanzania kuacha kutumia Pombe kali. Alisema Mathias

Nivyema watu wakanywa Pombe maenoe ya nyumbani hasa katika siku za sikukuu na kusisitiza kuwa kutumia Pombe kali ni maswala yanayo ondoa usalama wa mtumiaji, kama ataendesha uku amelewa. Alisema Mathias
PICHA YA SIKUU

IKIMUNYESHA MWANAJESHI AKIWA PAMOJA NA WANACHAMA WA CHADEMA, GODBLESS LEMA NA NASARI WAKIWA WANASHANGILIA

PICHA HII INAKUFUNDISHA NINI, KAMA WANAJESHI HAWARUUSIWI KUWA WAFUASI WA KISIASA.. JE NIPOZI LA PICHA TU AU TUSAIDIANE WADAU

Picha hii imepigwa na kuchapishwa na Gazeti la Mwananchi leo

Mtu aliyejitambulisha kuwa askari wa Jeshi la wananchi wa Tanzania (JWTZ),kambi ya Monduli,Arusha akiwa na wabunge wa Chadema,Godbless Lema (Arusha Mjini) na Joshua Nassari (Arumeru Mashariki) baada ya kumalizika kwa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na wabunge hao katika Mji mdogo Mererani,Simanjiro mkoani Manyara jana.

LEMA KURUDI TENA BUNGENI, TUNDU LISU APONGEZA MAHAKAMA KUTOA UAMUZI HUO


Mahakama ya Rufaa nchini Tanzania leo, imemrudishia ubunge  Godless Lema aliyekuwa Mbunge wa Arusha mjini kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), aliyo vuliwa na Mahakama kwa tuhuma ya kukiuka taratibu za Uchaguzi


Jopo la majaji watatu waliotoa hukumu hiyo, wakiongozwa na Jaji Natalia Kimaro, Wamesema kimsingi watu waliopinga Ubunge wa Bw.Lema hawakuwa na haki kisheria kufungua shauri hilo


Apiril mwaka Huu, Mahakama kuu kanda ya Arusha ilimvua Ubunge Bw. lema kufuatia kesi iliyofunguliwa na makada watatu wa chama cha Mapinduzi CCM, Kwa madai kuwa Mhe. Lema alikiuka taratibu za uchaguzi ikiwa nipamoja na kutoa Lunga za kashfa didhi ya aliyekuwa mgombea kupitia CCM. Badilda Buriani
 

Aidha katika maelezo yake, wakili wa Mhe. Lema Mbunge wa Singida Mashariki Mhe. Tundu Lisi amepongeza maamuzi ya Mahakama rufaa kwa kutoa  hukumu ya haki


KESI YA LULU YAAMISHIWA MAHAKAMA KUU BAADA YA UPANDE WA JAMUHURI KUSOMA USHAHIDI WAKE LEO

 
Kesi ya Kuua bila Kukusudia inayomkabili Msanii wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu kama LULU, imehamishiwa katika Mahakama Kuu, NA Lulu amerudishwa tena Maabusu. Lakini taree ya kusimamishwa katika mahaka kuu aikuweza kutwaja.


Lulu anakabiliwa na kesi ya Kuuwa bila kukusudia, Msanii mwenzake Mareemu Steven Kanumba, ambaye alifariki April 7, 2012 nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam, 


Upande wa jamuhuri leo, Ulisoma taarifa ya ushahidi wa Kesi hiyo, ambayo imechukuliwa kwa watu 9, Akiwemo Seth Bosco mdogo wake mareemu Steven Kanumba, Madaktari walio kuwepo kwenye uchunguzi wa mwili wa mareemu kanumba ambao waliwakilisha familia ya Mareemu, mapolisi waliofanya Upelelezi na walio andika maelezo ya awali ya Msanii LULU.


Katika Ushahidi huo, Jamuhuri ilitoa vitibitisho ambavyo ni ramani ya eneo la tukio, Ripoti ya kitaalamu ya uchunguzi wa kifo hicho, Ambayo imedhibitisha Kanumba liuwawa na mtikisiko wa ubongo yani Brain Concution. Pamoja na maelezo ya mshatakiwa yani LULU


Lulu alipopewa nafasi yakujielezea iwapo ananeno la kuongezea iliviambatanishwe kwenye ushahidi utakao tolewa katika mahakama Kuu., Lulu alisema Hana la Kuongezea.


Hii imekuwa kinyume na watu wengi walivyo sambaza kwenye mitandao ya Kijamii kuwa msanii huyo ameachiwa kwa Dhamana.

NASA YAKANUSHA MWISHO WA DUNIA NA KUWEPO KWA GIZA KWA SIKU TATU


MWISHO WA DUNIA NI LEO, KWA MUJIBU WA MAYAN

"THE MAYAN   CALENDER END'S 21.2012"

PICHA INAONYESHA JINSI DUNIA ITAKAVYO ARIBIWA

Mamia ya watu wametahamaki, wakisubiri kuona mwisho wa Dunia, ambao utatokea hii leo kwa mujibu wa Kalenda ya waumino wa Mayan, ambao wanapatikana nchini ya Mecxico 
 
Picha inaonyesha waumini wa Mayan
Waumini wa Dini ya Mayan ndio wanaamini juu ya taree hii, kuwa taree ya mwisho imefika kwamujibu wa kalenda yao ambayo imeishia leo taree 21, Dec 2012.

Nawame kuwa wakiita kwa majina mengi,  kama yafuatayo "This time now has many names "The Time of Trial on Earth," "Judgement Day," "The Time of Great Purification," "The End of this Creation," "The Quickening," "The End of Time as We Know It," "The Shift of the Ages," "The Apocalypse" and "Armageddon". hao ni Mayans

Kwa mujibu wa NASA(National Aeronautics and Space Administration), ambayo ipochini ya Taifa la Marekani, ambao wanahusika na maswala ya utafiti wa Anga, wamepinga kutokuwepo kwa mwisho wa Dunia na kuelezea kuwa tetesi za kuwepo kwa giza kwa siku tatu pia ni uvumi na imani tu

Kuna uvumi, wa dunia kukumbwa na giza kwa siku tatu kuanzia taree 23 Dec.2012 mpaka 25 Dec.2012, kitu ambacho pia siyo kweli.

Hatahivyo umoja wa wanajimu Duniani, bado aujasema chochote juu ya imani ya Mayani, kama kweli leo itakuwa ni mwisho wa Dunia ama sio mwisho wa Dunia

 soma zaidi:  2012apocalypse.net/
                https://www.nasa.gov/topics/earth/features/2012.htm#mayan

DIAMOND - SIWEZI KUMROGA TANZANITE
Star wa Bongo Fleva, Diamond Platinum, amefunguka juu ya sakata linalo endelea kati yake na msanii mwenzake Tanzanite, baada ya Tanzanite kusema kuwa anarogwa na Diamond, kiasi cha kuwa na maradhi yasiyo eleweka.

Akiongea na CampasVision Diamond amesema, Awezi kumroga Tanzanite "Nimroge iliiweje wakati nimemzidi vitu vingi sana, kama ni kuroga basi ninge waroga wale wenye mafanikio kimuziki na sio Tanzanite, hana kitu ambacho naweza kujifunza kutoka kwake, istoshe na mzidi kwa vitu vingi sana" alisema Diamond

Diamond alisema, malipo huwa ni hapahapa Duniani, yanayo mtokea yeye nimambo aliyo nifanyia mimi lakini mimi sijamfanyia chochote, pengine ni maradhi yake tu Mungu alipanga aumwe, sasa kutokana na  mambo yake binafsi anaisi ni mimi, aliongeza kuwa mimi nimtu wa Mungu sana siwezi kumfanya chochote" Alisema Diamond

Sasa hivi anaomba msamaa kwenye vyombo vya Habari, wakati alifanya watu wakanilaumu na kuniona mbaya kuwa nimeiba wimbo wake, kitu ambacho anajua siyo kweli, Mimi nimemsamee sana wala sina kinyongo naye, alisema Diamond

Hatahivyo, Tanzanite alisema anahisi kurogwa na Diamond kwani anaumwa maradhi yasiyo eleweka, kwani Diamond alimwambia atamfanyia kitu ambacho awezi kusaau maishani mwake , Nakumuomba sana Msamaa msani Diamond iliaweze kupona maradhi yanayo msumbua.


Pichani ni Tanzanite anaye dai kurogwa
" Namuomba Diamond msamaa sana, alisema sitasahau atakacho nifanyia, nandio sababu naamini pengine ni yeye atakuwa anahusika na maradhi yasiyo eleweka yanayo nisumbua, anisamee tu" alisema Tanzanite


MTOTO WA AJABU ALIYE ZALIWA JUZI MKOANI MBEYA AFARIKI DUNIA


Mtoto aliye zaliwa bila pua, huku macho yakiwa juu ya paji la uso amefariki dunia, Mungu ailaze roo ya mtoto huyo mahali pema peponi
RAISI WA MAREKANI BARACK OBAMA, AMEIBUKA KUWA, PERSON OF THE YEAR 2012

Barack Obama, amekuwa Person of the year, Nafasi ambayo hutolewa na TIME ya nchini marekani, huku picha yeke aliyopiga na Mke wake Mishell Obama wakati wa kampeni za uchaguzi wa marekani ikiwa picha bora ya muda wote

Kwamujibu wa Jarida hilo 
vigezo zilivyotumika ni hivi hapa chini 

We are in the midst of historic cultural and demographic changes, and Barack Obama is both the symbol and in some ways the architect of this new America. In 2012, he found and forged a new majority, turned weakness into opportunity and sought, amid great adversity, to create a more perfect union.

Read more: http://poy.time.com#ixzz2FW2DnaaC







CHADEMA WALIA NAMCHAKATO WA MAONI YA KATIBA MPYA


Chama cha Democrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kimemtaka Rais akumbushwe kujibu barua ya Mwendelezo wa Operesheni ya Vuguvugu la Mabadiliko M4C, ili itumike kushinikiza Serikali kuchukua hatua stahiki juu ya mambo mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Mwenyekiti wa chama hicho Bw.Freeman Mbowe, amesema kuwa chama hicho kimechukua fursa hiyo kueleza baadhi ya masuala yaliyojiri kwenye mkutano wa kamati kuu ya chama hicho ambao ulifanyika kwa siku mbili ya taree 15 na 16, Dec 2012.

"Mazungumzo yaliyofanyika kati ya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na  Rais Jakaya Kikwete, juu ya hoja ya kuundwa kwa Tume ya kimahakama kuchunguza mauaji na haja ya Rais kuchukua hatua na muendelezo wa M4C", ni muimu kuwa Raisi akumbushwe, alisema Mbowe

Mbowe amesema, tarifa ya hali ya siasa, Mapendekezo ya mwendelezo wa operasheni za vurugu la mabadiliko M4C, pamoja na mchakato wa mabadiliko ya katiba nimiongoni mwa vitu vilivyopewa kipaumbele

Aidha, Kamati hiyo imeitaka Tume ya mabadiliko ya katiba kuwasilisha mapendekezo ya Chadema juu ya katiba mpya na mapendekezo kwa serikali juu ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba awamu ya pili na tatu kwa pamoja, lengo nikupata katiba mpya na bora kwa taifa, alisema Mbowe

Kamati hiyo imeazimia, Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni kutoa mapendekezo ya kurekebisha katiba mpito kuhakikisha tume huru ya uchaguzi na marekebisho ya sheria zinazo simamia uchaguzi yanafanyika kabla ya katiba mpya, Alisema Mbowe

WITNEY HUSTON, TOP GOOGLE SEARCH OF THE YEAR 2012


Bado nakuletea mfululizo wa matokeo ya mtandao maarufu wa Google, Ambapo leo ni tarifa kuusu Marehemu Witney Houston.

Kwa mujibu wa mtandao huo, marehemu Witney Houston ndiye Mtu aliyezunja recodi ya kutafutwa au kuuliziwa Zaidi Dunia, lakini kwa Africa Mashariki Ripoti ineongelea nchi ya Kenya na Uganda,

Ambapo Witney aliongoza kutafutwa zaidi kuliko watu wote ndani ya nchi hizo, za Kenya na Uganda.

Witney alifariki February 2012. Lakini bado watu wengi Duniani hupenda kujua kuusu habari zake




Kategori

Kategori