TCRA WATANGAZA NEEMA MATUMIZI YA SIMU, WAFANIKIWA KUDHIBITI MAKAMPUNI NCHINI


Gharama za kupiga simu kutoka mtandao wa kampuni moja ya simu ya mkononi kwenda mwingine nchini, kuanzia Machi Mosi mwaka huu zitashuka kutoka sh.115 hadi sh.34.9 kwa dakika moja.

Uamuzi huo umefanywa na mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kufanya mapitio ya gharama za mwingiliano kwa kampuni za simu nchini kwa mwaka 2013. Pia kuanzia Januari Mosi mwakani gharama hizo zitapungua hadi sh.32.4.

Vilevile Januari 2015 gharama hizo zitashuka na kufikia sh. 30.6, Januari 2016 gharama hizo zitadhuka mpaka sh. 28.6, Januari 2017 zitashuka mpaka sh.26.9 kwa dakika moja.

Akitangaza bei uamuzi huo jijini Dsm jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema umetolewa kwa mujibu wa sheria ya TCRA ya mwaka 2003 sura 172. Profesa Nkoma alisema viwango hivyo ni vya kikomo cha juu na pia ni bei elekezi lakini akasema kampuni za simu zina uhuru wa kukubaliana kibiashara ili mradi makubaliano yao yasizidi gharama zilizoelekezwa na TCRA.

    Baadhi ya sababu ya mabadiliko ya gharama za kupiga simu:
  • Kumpa mtumiaji uhuru wa kuongea bila kubadilisha badilisha laini
  • Kumpunguzia mtumiaji mzigo wa kubeba simu na laini nyingi
  • Gharama za simu nchini Tanzania ziko juu ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika
  • Kudhibiti ukiritimba wa gharama zinazotozwa haswa mtu ananapopigia mtandao mwingine


EmoticonEmoticon