WANAFUNZI IFM WAANDAMANA KISA KULAWITIWA KWA WENZAO WAWILI NA WIZI WA LAPTOP 100


WANAFUNZI chuo cha usimamizi wa fedha IFM cha jijini Dar es Salaam leo, wameandamana kutoka chuoni kwao mpaka makao makuu ya Jeshi la Polisi (Wizara ya mambo ya ndani) wakilalamiki kulawitiwa kwa wenzao wawili katika Hostel zao zilizopo kigamboni pamoja na wizi wa Laptop zaidi ya 1000




Wanafunzi hao ambao walikuwa wakipiga kelele za kumtaka Kamanda wa kanda maalum wa Dar es Salaam Suleiman Kova kufika eneo hilo ilikusikiliza madai yao ambayo wamedai kutoa yamekuwa yakitokea kwa muda mrefu sasa



" Kitakachofuata ni tarifa ya vifo vya wanafunzi, kulingana na matukio ambao yanazidi kuendelea kwani wanafunzi waliolawitiwa nikwakuwa walikuwa hawana Laptop kabisa na mpaka sasa wanafunzi wengi wameibiwa Laptop zaidi ya 100" Alisema kijana mmoja katiya wanafunzi waliokuwa wakikimbia kwa maandamano

Hatahivyo kamanda Suleiman Kova aliwasili eneo la tukio mda mfupi badaae na kuwaahidi kufuatilia tukio hilo, huku akiwaomba majina yawahalifu wa matukio hayo



 "Mbona hamkusema mapema, mimi na pambana na watu wenye silaha kali itakuwa hawa vibaka, nipeni listi ya majina ya hao watu alafu muone, muda mfupi tu hakunatena tatizo hili" Alisema Kamanda Kova







Wamafunzi wa IFM, wameomba kupewa ulinzi hasa katika Hostel za chuo hicho zilizopo Kigamboni kufuatia wenzao wawili kulawitiwa na vitendo vya ubakaji pamoja na kunyang'anywa Laptop zaidi ya 100.


EmoticonEmoticon