IGP MWEMA KUKABILIANA NA UHALIFU, AKABIDHI PIKIPIKI 571


JESHI la Polisi nchini Tanzania limepanga kutoa mkakati wa kuwashirikisha wakaguzi wa tarafa kata katika kuelimisha jamii juu ya namna ya kukabiliana na ongezeko la Vitendo vya uhalifu

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Saidi Mwema amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akikabidhi pikipiki 571 zilizotolewa na ofisi ya Raisi Ikulu, kwa ajili ya kuzisambaza katika tarafa mbalimbali nchini.

Kwa mujibu wa IGP Mwema, Jeshi la Polisi litashirikiana na wadau katika ngazi zote za utawala kuanzia ngazi ya kata, serikali za mitaa na katika taraf, katika kutoa elimu kwa wananchi kuhusu mpango huo unaoenda sambamba na kupunguza wimbi la ajali za barabarani


EmoticonEmoticon