IDADI YA VIJANA WALIOJIUNGA NA ELIMU YA JUU YAONGEZEKA



IDADI ya vijana wanaojiunga na mafunzo ya elimu ya juu nchini Tanzania imeongezeka na kufikia laki moja na elfu ishirini na tano, baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi katika mikoa mine nchini

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa, amesem Hayo wakati wa ziara ya naibu spika wa Bunge la Korea Kusini Park Byeong-Seug, ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi

Kwa mujibu wa Waziri Kawambwa, Ujenzi wa vyuo hivyo umetokana na mkopo wa Dola za Marekani Millioni 8, zaidi ya shilingi Billioni 10 za Tanzania ilioupata kutoka Serikali ya Korea Kusini

Waziri Kawambwa ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika Ujenzi wake, vyuo hivyo vimefanikiwa kudahili Wanafunzi 1160,sawa na ongezeko la asilimia 1 ya uwezo wa vyuo vyote nchini. Alisema Waziri


EmoticonEmoticon