WANAFUNZI 450 HUFARIKI KILA KWAKA NCHINI KISA, UKOSEFU WA VYOO MASHULENI






NAIBU Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt Seif Rashid amekiri kuwepo kwa upungufu wa Vyoo katika Shule za msingi nchini, na kwamba tayari wanafunzi zaidi ya 450 wamefariki dunia kutokana na magonjwa ya homa ya matumbo kutokana na vyoo hivyo kuwa vichafu kinyume cha utaratibu wa kiafya

Akiongea na Waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Naibu waziri huyo amesema kuwa miongoni mwa wagonjwa wanaohudhuria hosibitali kwaajili ya kupata matibabu ya magonjwa ya Tumbo na kuhara ni wanafunzi, ambapo kila mwaka ni wanafunzi 45o hufariki dunia kwa maradhi hayo. Alisema Drkt Seif

“ Hali ya kukosekana kwa vyoo vyenye mazingira salama kiafya, imesababisha daadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya uambukizo yakiwemo magonjwa hatari kama homa ya matumbo, kuhara damu na hata ugonjwa wa kipindupindu” Alisema Dkt. Seif

Hatahivyo, Asilimia 86 ya shule zilizopo nchini Tanzania, hazina mazingira na miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ukiwemo wa viungo, kwani ni alisimia 4 tu ya shule nchi nzima ndio zina niundombinu ya choo kwa watu wenye ulemavu.

“Bado hatuna miundombinu ambayo ni rafiki kwa watu wenye ulemavu kutokana na asilimia ndogo sana ya shule zetu ndio zenye miundombinu hiyo, ambayo ni asilimia 4 tu kwa nchi nzima” alisema Dkt. Seif

Mojawapo katiya malengo ya Serikali ndani ya Sekta ya Elimu, ni kufanikisha matumizi ya Tundu  moja la choo kutumiwa na wanafunzi 20 kwa watoto wakike huku wakiume wakitumia tundu moja wanafunzi 25, mpango ambao haujafanikiwa hadi hivi sasa. Na kwa mkoa wa Dar es salaam ni shule 6 tu ndizo zina miundombinu ya choo kwa uwiano wa idadi ya wanafunzi.


EmoticonEmoticon