WALEMAVU WA NGOZI WALILIA USALAMA WAO, WAITAKA SERIKALI KUGUNDUA MBINU MPYA YA MAUAJI DIDHI YAO

Chama cha Walemavu wa ngozi nchini kime lalamikia uendeshwaji wa kesi zawatu wanaokamatwa kwa kuwadhuru, pamoja na kutokamtwa kwa kundi nambalo ndio waagizaji wakubwa wa viungo vya walemavu kitu ambacho kinawapa mashaka juu ya usalama wao

Akiongea leo na waadnishi wa habari maelezo jijini Dar es salaa, Afisa Mahusiano na utetezi wa Chama cha Albino Nchini bwana. Joseph Torner amesema kwa uchungu kuwa, Kutokamatwa kwa kundi la tatu ambao ndio wanunuzi au waagizaji wa viungo vya Albono ni ishara kwamba tatizo hilo halitokaa limalizike nchini

"Kesi ambazo ziko mahakamani mpaka sasa ni tano tu, wakati Albino waliouwawa ni watu 70. na waliokamatwa ni waganga na wale wanaotekeleza matukio ya mauaji je? kundi ambalo ni waagizaji wa hivi viungo wako wapi wakati nchi yetu inasifiwa kwa upelelezi" alisema bwana Torner

Tunaiomba serikali iwenke mikakati mipya, kwani hivi sasa wanauwa kwa mbinu zingine kiasi kwamba unaweza kuhisi mauaji hayapo lakini kuna tarifa za mauaji kwa mwaka 2001 mpaka 2001 za matukio 3 na hizo nizile zinazoripotiwa tu, alisema Touner

Aidha, Touner alilalamikia kitendo cha wanafunzi wenye ulemavu wa Ngozi katika shule ya Msingi Buhangija iliyopo manispaa ya Shinyanga ambao ni zaidi ya 139 kutorudi nyumbani wakati wa likizo kwa kuhofia usalama wao, huku aijulikani nilini watarudi kukutana na familia zao

" Wanafunzi wengi wenye ulemavu wa ngozi wamejikuta wakiwa kwenye kambi kila inapofika kipindi cha likizo kitendo ambacho kinaleta simanzi kwa familia za watoto hawa, kwani hawajui nilini watakutana na familia zao" Alisema Touner

Tangu mwaka 2006 mpaka hivi kumekuwa na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi hapa nchini licha ya serikali kuweka usalama kwa watuhao


EmoticonEmoticon