SERIKALI YATAKIWA KUSHUGULIKIA UKIUKWAJI WAHAKI ZA BINADAMU NCHINI



SERIKALI ya Tanzania imekosa mfumo wa uhakika wa kushugulikia malalamiko ya matukio ya ukiukwaji wa Haki za binadamu hapa nchini, Mtandao wa watetezi wa Haki za binadamu nchini waeleza


Raisi wa Jumuhiya ya Wanasheria Tanganyika, ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao huo. Wakili Francis Stolla amesema kumekuwa hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa pale ambapo mashirika na asasi za kulinda haki za binadamu zinapopiga kelele juu ya swala hilo

“Kumekuwa na mauaji mbalimbali yanayo laaniwa na kugusa hisia za watu, tena zinazotumia nguvu kama Risasi lakini sheria za uundwaji wa Tume ambazo zinaundwa na serikali, wakati huohuo serikali ndio inatuhumiwa, aifanyi haki kutekelezwa” Alisema Wakili Francis

Uundwaji wa Tume umekuwa sio mzuri, ucheleweshwaji wa kuchukua hatua mpaka wananchi wana lalamika, kwani wahusika hawafikishwi mahakamani hata pale tume inapopeleka Ripoti na Uchunguzi wake kwa serikali lakini hatua madhubuti hazichukuliwi. Alisema Francis

“Kunachombo ambacho akiegamii upande wowote ambacho ni KORONA, chombo hiki kipochini ya Mahakama kwani mahakama ndio imepewa mamlaka ya kutenda haki pale Serikali inapokuwa kwenye mgogoro na Wananchi wake, kitu ambacho nacho hakifanyiwi kazi vizuri” Alisema Francis

Hatahivyo Wakili huyo amesema, Hatawale wanaotetea haki za binadamu nchini nao wanaitaji kulindwa kisheria ilikuwa na usalama wa maisha yao. Alisema Wakili Francis


EmoticonEmoticon