TANGA, DODOMA KUAMIA DIGITALI LEO USIKU


WAKAZI wa Miji ya Tanga na Dodoma wamepokea kwa hamasa kubwa zoezi la kuamia Digitali kuliko ilivyo kuwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaaam, kwani wakazi wengi wa maeneo hayo tayari walisha nunua Vingamuzi

Ikiwa leo ni siku ya kuzimwa kwa Mitambo ya Analogia ifikapo saa sita usiku, Msemaji wa TCRA bwana Inocent Mungy ambaye ni msemaji wa TCRA amesema hayo hii leo kwanjia ya simu akiwa mkoani Dodoma, kuwa leo usiku kwa mikoa hiyo miwili mitambo ya Analogia itazimwa na kuwashwa ya Digitali

Aidha, amesema kwa mkoa wa Tanga tayari watu elfu 20 wameamia Digital hatakabla ya mitambo hiyo kuzimwa, Na mkoani Dodoma hali iko hivyohivyo kwani tayari watu elfu 27 wameshaamia Digitali, huku idadi ndogo ya watu wasio zidi elfu 35 wakiwa ndio bado hawajaamia lakini niwengi sana walio jiandaa kuamia kwa siku ya leo

Lakini bwana Inocent amesema, kuanzia leo asubuhi kulikuwa na msururu wa watu wasiozidi 15 wakisubiri kununua Ving'amuzi kwa mawakala mbali mbali mkoani Dodoma

“Kwa mkoa wa Dodoma tumefanya majaribio katika maeneo ya Nong'ono nyuma ya chuo cha UDOM, tayari Digital ikosawa kwa kutumiwa na kufikia muda halali tutazima mitambo ya Analogy” alisema bwana Mungy

Hatahivyo bwana Mungy, amewataka wananchi kusema aina ya Tv aliyo nayo, pamoja na eneo analo kaa kama ni bondeni au eneo la Tambarare ilikuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza, na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kwenda na mtaalamu wa kuunganisha king'amuzi wakati wa kuunganisha king'amuzi hicho

Kama kuna mtu anamalalamiko yoyote nimuhimu kuyafikisha mahali aliponunua king'amuzi kwani, tayari wamepokea malalamiko 180 na kuyafanyia kazi.

Pia bwana mungi amekanusha uvumi unaoenezwa na vyombo vya habari kuwa kuna ina ya Kinga'amuzi ambacho kitazimwa ifikapo June mwaka huu kuwa sio za kweli na kuwataka wanao eneza uvumi huo kuacha maramoja


EmoticonEmoticon