MILLIONI 100 KUSAIDIA WALEMAVU 150, KUPITIA MFUMO WA MKOPO WA VICOBA




Walemavu 150 nchini wamefaidika kwa kupata mikopo midogomidogo, kwakupitia mfumo wa VICOBA yani Vilage Community Bank, ambayo ilianzishwa mwaka jana na Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dr. Reginald Mengi ambapo kiasi cha Millioni 100 zilitolewa ilikuwakopesha Walemavu

Akiongea kwenye Hafla iliyo andaliwa kwaajili ya Walemavu Msimamizi wa Vikoba Bi. Devodha Kitokola ambaye ni Mbunge wa Viti maalum Kupitia chama cha CCM, alielezea mafanikio ya Mikopo hiyo kuwa,Tayari walemavu 150 wameweza kukopeshwa, kutoka katika meneo mbalimbali nchini

Aidha Bi. Devodha alisema kuwa Wanategemea kusambaza huduma hiyo katika vijiji vingi zaidi nchini kwani walemavu niwengi na wote wanaitaji msaada huwo

"Lengo letu nikuwafikia walemavu wote nchini ilinao waweze kufaidika kwani tunapokea maombi mengi kutoka seemu nyingi nchini. Alisema Bi Devodha

Zaidi ya Milioni 100 tayari zimetolewa na Dr. Mengi ilikuendeleza Vicoba kwa walemavu, kwani  walemavu Wameonyesha juhudi na uwezo mkubwa wakutumia fursa hiyo. Alisema Bi Devodha

Walemavu wengi wameonyesha nia ya kuendeleza kipato chao, na wengi wao wameahidi kukopa kwa malengo ya baadae ilinawao waje kuwakopesha watu wasio na ulemavu. Walemavu wameonyesha nia ya kujiendeleza kimapato wao pamoja na jamii kwa ujumla. Alisema Bi Devodha


EmoticonEmoticon