VING'AMUZI BONGO BADO NI TATIZO, UCHUNGUZI WA BAINI






Baada ya uzimaji wa mitambo ya Analojia katika jiji la Dar es salaam, imebainika kwamba ni wananchi wachache sana wa Dar es salaam wana uwezo wa kuangalia TV. Hii ni kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na shirika la habari la XHUSA.

Tanzania imekuwa nchi ya kwanza Afrika Mashariki kuhamia mfumo wa kisasa wa matangazo wa Dijitali baada ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na teknolojia kutangaza kwamba jiji la Dar es salaam ndilo la kuanza kuathiriwa na mfumo huo mpya.

Hata hivyo utafiti huo unaonyesha kwamba, wananchi walio wengi bado hawana ving'amuzi nyumbani kwao na ni watu watano kati ya 20 ndio hupata huduma ya matangazo humu jijini. Hali hii inatokana na bei ya ving'amuzi kuwa juu na wananchi walio wengi hawawezi kumudu bei hizo.

Nchi za Afrika Mashariki zimeamua kuhamia mfumo mpya wa matangazo miaka mitatu kabla ya muda wa Shirikisho la Kimataifa la Mawasiliano hapo Juni 2015. Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi hajachukua uamuzi wa kuzima mitambo yao kwa sababu mbalimbali.

Kwa upande mwingine, Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Bw. Innocent Mungy  amekanusha madai kwamba ni watu 5 kati ya 20 ndio huwapata matangazo katika mfumo huu mpya jijini Dar es salaam.

Aidha Bw. Mungy amesema kwamba, ving'amuzi vimenunulika sana kabla na baada ya kuzima mtambo wa Analojia jijini Dar na kwamba madai ya Shirika la Habari la XINHUA si za kweli. Hata hivyo Bw. Mungy amesema kwamba tatizo ni kwamba walio wengi bado hawana ujuzi wa kuunganisha ving'amuzi vyao kwa sababu wanashindwa kusoma na kuelewa maelekezo yaliyoandikwa.


EmoticonEmoticon