MJI WA KIGAMBONI SASA KUWA WILAYA RASMI







Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi mji wa Kigamboni wa jijini Dar es salaam kuwa Wilaya kamili inayojitegemea, na kufanya mkoa wa Dar es salaam kuwa na Wilaya nne

Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya makazi Prof. Anna Tibaijuka amesema kuanzia sasa mji wa Kigamboni utatoka na chini ya manispaa ya uongozi wa manispaa ya Temeke.
“ Kigamboni itajitegemea kama Wilaya kuanzia  leo, na utakuwa chini ya  Kigamboni Development Agency (KDA)”. Alisema Prof. Tibaijuka
 
Kutengwa kwa Mji mpya wa Kigamboni kuwa Wilaya, kumekuja baada ya kuundwa kwa chombo kijulikanacho kama Wakala wa Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni inayojulikana kwa Lugha ya Kiingereza kama Kigamboni Development Agency (KDA), Alisema Prof. Tibaijuka

KDA, itakuwa na jukumu la kuendeleza Kigamboni kuwa mji wa Kisasa, na kufafanua kuwa shuguli zote za kiserikali zitasimamiwa na chombo hicho kwa kushirikiana na baraza la ushauri la mji wa Kigamboni. Alisema Prof. Tibaijuka

Hatahivyo, Baraza la ushauri wa Wilaya ya Kigamboni utaundwa kwa kushirikisha wawakilishi wa wananchi pamoja na Madiwani na Wabunge wa eneo hilo.


EmoticonEmoticon