WATU 11 WAUWAWA TANA RIVER INCHINI KENYA



WATU 11 wameuwawa leo asubuhi na wengine kujeruhiwa vibaya katika eneo la Kibusu Tana river nchini Kenya katika Visa vya kulipiza kisasi kati ya jamii ya wa pokomo na jamii ya Orman. Na kupelekea idadi ya watu waliokufa tangu juzi kufikia 21

Watu kutoka jamii ya Orman leo majira ya saa moja asubuhi wamevamia vijiji vya Pokomo na kuuwa watu 11, kwa nia ya kulipa kisasi juu ya wenzao 10 waliyo uwawa jana asubuhi na jamii ya Pokomo hata HotMix pia ilikujuza juu ya habari hiyo

Kiongozi wa kikabila wa eneo hilo Chief Amuma Mkala na Babuya Komora ambaye ni Diwani wa eneo hilo kwa pamoja walithibitisha kutokea kwa tukio hilo,

Shirika la Msalaba mwekundu nchini Kenya limesema kuwa, miongoni mwa walio uwawa ni watoto watano, wanawake watatu na wanaume watatu kutoka jamii ya Pokomo


Hatahivyo, Licha ya Raisi wa Kenya Mwai Kibaki kutuma Askari 2, 000 katika eneo hilo bado mauaji yameendelea kutokea, na mahofisa wa Polisi wanahofia kutokea mauaji mengine zaidi

December 21 mwaka jana watu 42 waliuwawa katika eneo hilo na kupelekea idadi ya vifo vya wenyewe kwa wenyewe kuongezeka hadi 160 tangu mwzi wa nane mwaka jana.



EmoticonEmoticon