TCRA - TUNASHUGULIKIA CHANGAMOTO ZINAZOTOKEA BAADA YA KUHAMIA KWENYE MFUMO WA DIGITALI


Baada ya TCRA kufanikisha shuguli ya kuhamisha mitambo ya kurushia matangazo ya Televisheni kutoka Analogia kwenda Digitali sasa mamlaka hiyo inajielekeza kwenye kutatua changamoto zinazo tokea katika mfumo huo mpya

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) Mhe. Prof John Nkoma amesema, mamlaka yake inafuatilia kwa karibu huduma zinazotolewa na makampuni yote yaliyopewa leseni ya kuuza Ving'amuzi nchini.

" Tumeagiza watoa huduma waboreshe huduma kwa kuongeza sehemu za mauzo, lengo nikukabiliana na ongezeko la wateja wanaohitaji ving'amuzi pamoja na kutatua matatizo yanayojitokeza kwa wateja mara moja" alisema Prof Nkoma.

Aidha, mamlaka imeagiza vituo vya utangazaji vya luninga ambavyo havijajiunga kwenye mfumo wa digitali kufanya hivyo mara moja ili huduma ziwafikie wananchi.

Prof. Nkoma, amesema wanaamini utangazaji wa televisheni kwenye mfumo wa digitali utaleta chachu kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi na kuwaomba wananchi kujiunga haraka na matangazo ya televisheni ya mfumo wa digitali, Alisema.  


EmoticonEmoticon