MAPINDUZI CUP, COASTAL, AZAM NA MTIBWA NANI KUINGIA NUSU FAINALI??


TIMU mbili zitakazokamilisha idadi ya timu za kucheza hatua ya Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi, zinatarajiwa kujulikana leo, wakati mechi mbili kali zitakapopigwa kwenye viwanja viwili tofauti visiwani Zanzibar

Coastal Union ya Tanga inayoshiriki michuano hii kwa mara ya kwanza, inamenyana na Miembeni kwenye Uwanja wa Mao Dze Tung saa 10:30 jioni, kabla ya mabingwa watetezi Azam FC kupambana na mabingwa wa zamani wa michuano hii, Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Amaan, kuanzia saa 2:30 usiku wa leo.

Azam ndio inaongoza Kundi B kwa pointi zake nne, wakifuatiwa na Miembeni wenye pointi tatu, Coastal pointi mbili na Mtibwa yenye pointi moja inashika mkia.
Kwa ujumla, hadi sasa timu yoyote kati ya zote nne za Kundi B inaweza kufuzu Nusu Fainali na hii inamaanisha hili ndilo lilikuwa Kundi la kifo.

Kwa upande wa Kundi A, Hapo jana Simba ilifuzu nusu fainali na kuungana na Tusker ya Kenya baada ya kutoka Sare ya 1-1 dhidi ya Bandari. Mabingwa hao wa Tanzania Bara Kikosi cha kwanza kinatarajia kuondoka nchini kuelekea nchini Oman kwa ajili ya maandali ya mzunguko wa pili wa ligi na kuacha kikosi cha pili (Simba B) kikiendelea na mashindano hayo.

Haya ni mashindano maalum kwa ajili ya kuadhimisha miaka 49 ya mapinduzi Zanzibar sherehe zitakazo fanyika January 12 katika uwanja wa Amaan.

katika soka la kimataifa

Mwanasoka Bora wa Dunia kujulikana leo, kupitia tuzo za (BALLON D'OR) wachezaji ambao wanaupinzani mkubwa katika nafasi hiyo ni Leonel Messi ambaye anachezea Barcelona, Christiano Ronaldo anachezea timu yaReal Madrid na Andre Iniesta ambaye anachezea Barcelona FC


EmoticonEmoticon