GESI SASA KUBAKI MTWARA NA MEGAWATI 600 ZA UMEME KUZALISHWA HUKO


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na wakazi wa Mtwara hapo Jana

Habari nilizo pata toka mtwara muda simrefu

KUPITIA, kikao kilicho kaa kwa siku mbili mfululizo katiya Wajumbe mbalimbali wanao wakilisha wanachi wa Mtwara na WAZIRI Mkuu, Hatimaye Gesi Kubaki Mtwara na itazalishwa eneo la Madimba huku kiwango kidogo cha Gesi kikisafirishwa kuja Dar, lakini Mtwara ndipo kutakuwa na Gridi kubwa ambayo ita zalisha Megawati 600 za umeme.

Mawaziri 6, hii leo wametua mkoani Mtwara kumuunga mkono Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwaajili ya Kuongea na wakazi wa Mtwara juu ya mgogoro wa mbola la Gesi kutoka Mtwara kuja Dares salaam. Mgogoro uliodumu kwa wiki mbili sasa

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli), Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, - (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt. Shukuru Kawambwa).

Wajumbe wengi katika kikao hicho wamekataa swala la Bomba la Gesi kutoletwa Dar es salaa, Miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao hicho, nipamoja na baadhi ya wajumbe kumkataa Mkuu wa Mkoa na kumwambia Waziri mkuu aondoke naye


Moja kati ya Mitambo ya kuzalishia Gesi huko Mtwara

Mengine ni pamoja na kauli ya Hawa Gasia, ya kutoa kauli za uongo kuusu MtwaraVijijini kuunga mkono suala la Gesi kwenda Dar huku Madiwani wa Mtwara nao wakidai hawakuusishwa juu ya swala hilo.






Kikao kinafanyika chini ya ulinzi mkali wa FFU, JWTZ na UWT (Usalama wa Taifa). Wananchi wa Mtwara na maneo ya Lindi wamekuwa na mgogoro wa wiki mbili juu ya Mbomba la Gesi kusafirishwa kuja Dar.


EmoticonEmoticon