RAISI JK AHUDHURIA MAZISHI YA SAJUKI

Raisi akiwa katikati ya waombolezaji katika makaburi ya Kisutu
Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr Jakaya Mrisho Kikwete ni miongoni mwa mamia ya watanzania walioudhuria mazishi ya msanii Sajuki ambaye amezikwa leo katika makaburi ya Kisutu Jijini Dar es Salaam.

Sajuki alifariki Alfajiri ya taree 2, Jan 2013 katika Hospitali ya Muhimbili alipolazwa, Sajuki ambaye aliugua kwa muda mrefu akisumbuliwa na maradhi ya Saratani, ugonjwa ambao umemsumbua kwa miaka miwili mpaka anafikwa na umauti

Wasanii mbalimbali na viongozi wengine pamoja na wananchi ni miongoni mwa watu waliohudhuria mazishi ya msanii huyo. Sajuki ameacha mke Wastara Juma na mtoto mmoja wa miezi 9. Mtandao huu unatoa Pole kwa Ndugu jamaa na Familia ya Marehemu kwa kuondokewa na mpendwa wao

Mwili wa marehemu Sajuki ukiwa ume bebwa ba waombolezaji

Alichokisema Raisi kwenye mtandao wa Twitter kuusiana na msiba wa sajuki


Parents having to bury their children just doesn't seem like the natural order of things; it's heartbreaking. Rest in peace Juma Kilowoko.


EmoticonEmoticon