Mhe. PINDA - WANANCHI WA MTWARA WALIPOTOSHWA

Waziri Mkuu akiwa Bungeni siku za Nyuma


WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ametoa ufafanuzi wa kile kilicho jiri Mtwara na kusababisha vurugu kubwa ambazo zilipelekea nyumba kuchomwa moto hasa za ziongozi wakati wananchi wa Mkoa huo wakipinga swala la kusafirishwa kwa bomba la Gesi kutoka Mtwara kuja Dar es salaam

Akiongea leo Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu kwa waziri Mkuu, alitoa kilekilicho sababisha vurugu kwa wakazi hao na kusema ni upotoshaji tu ulifanyika

Mhe. Pinda amesema kuwa Serikali na Viongozi hawa kutoa elimu na ufafanuzi wakutosha kwa wakazi wa Mtwara ilikujua nijinsi gana watanufaika na Mradi wa Gesi ulioko mkoani mwao

" Nakiri kuwa swala la elimu ya kutosha kwa wakazi wa Mtwara aikutolewa, na kumekuwa na upotoshaji wa taarifa huku wengine wakidai kuwa Gesi hiyo itapelekwa kwao Raisi Jakaya kitu ambacho sio kweli" Alisema 

                 Mwigulu alia chuo cha uzoefu kianzishwe

Akimuuliza swali Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba alishangwaza na kitendo cha serikali kulalamika kukosa wafanya kazi huku kukiwa na wahitimu wengi wa vyuo vikuu ambao hawajapata kazi hadi hizi sasa

"Kwanini serikali inalalamika haina wafanyakazi wakutosha katika halamashauri zake wakati kuna idadi kubwa ya wanafunzi mitaani, lakini wanakwamishwa na swala la uzoefu je kuna uwezekano wakuanzisha chuo cha Uzoefu" Aliuziza Mbunge Huyo


Mhe. Mwigulu amesema, kila mtaa kuna mwanafunzi aliye hitimu elimu ya juu tena katika vyuo vyenye hadhi ya juu na kuitaka serikali kuwatumia hao, lakini pia alisisitiza kipengele cha Uzoefu kifutwe na kumatakla waziri mkuu kutoa tamko la kufuta kipengele hicho
Aidha waziri mkuu alijibu kwakukataa kuwepo kwa upungufu wa wafanyakazi katika almashauri hizo, na kusema kuwa kama serikali hawana seemu ya kuitaji huzoefu

"Wala sisi atuitaji uzoefu kwani uzoefu ndio anaenda kuupata pale kwenye Almashauri anapoenda kufanya kazi lakini pia hatuwezi kuwaajiri wote wanao hitimu katika sekta ya umma" Alisema Waziri Mkuu


EmoticonEmoticon