NEEMA KWA LULU, SASA KURUDI TENA URAIANI


Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam imempatia dhamana msanii wa Filamu Elizabeth Michael (Lulu) kwa masharti ya kupata wadhamini wanaofanya kazi Serikalini wakiwa na Sh 20milioni kila mmoja, kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani,kuripoti mahakamani na wafadhili kuweka bondi ya Shilingi mil 20

Hivi sasa yupo katika maeneo ya  Mahakama hiyo akisubiri kukamilisha taratibu ili aweze kurudi nyumbani kwake.Miongoni mwa masharti mengine ni pamoja na kutoruhusiwa kumtoka nje ya Dar es salaam, na kwamba atawajibika kuripoti kila tarehe moja ya mwenzi mahakamani hapo
Lulu Michael anayekabiliwa na tuhuma za mauaji ya kuuwa bila kukusudia ya Msanii mwenzake Steven Kanumba April 72012, Leo Lulu amepata dhamana baada ya kukamilisha masharti ya mahakama.


EmoticonEmoticon