GESI NI MALI YA TAIFA, AIWEZI KUWANUFAISHA MTWARA-LINDI KWA ASILIMIA MIA ASEMA WAZIRI

wananchi wa lindi wakiandamana

Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Prof. Dr Sospeter Muhongo, amesema Madai ya wananchi wa Lindi kutaka rasilimali ya Gesi iwanufaishe kwa asilimia mia na isisafirishe kwenda katika maeneo mengine ya Taifa aliwezekani.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo, Jijini Dar es salaam, Waziri amesema swala la gesi nila kitaifa na kwamba kila mmkoa inahaki ya kutumia gesi hiyo kinyume na madai ya Wananchi wa Mtwara wanavyo hitaji

"Tukisema Gesi iishie Mtwara na kuwanufaisha wao kwa asilimia zote, basi hata mikoa mingien yenye raslimali nyingi nao watumie pekeyao, mfano Maeneo ya Mara, Mwanza nao wakatalie Samaki zao au Mikoa inayo zalisha Chakula kwa wingi nayo pia ikakataa, kituambacho hakiwezekani, lazima tutumie rasilimali zetu kama taifa" Alisema Waziri Muhongo

Aidha, Gesi Asilia, Madini, Makaa ya mawe, Wanyama Pori, Misitu, Milima ya utalii, mito, maziwa, bandari vyote kwa pamoja ni mali Watanzania, Alisema Waziri Muhongo na kuongeza kuwa nilazima tutunze rasilimali zetu kwa ajili ya taiafa zima. Alisema 

Muhongo, amewataka watanzania wasikubali kuvunja mikoa na rasilimali zilizopo kwa kisingizio cha rasilimali kwani kufanya hivyo nikuvunja amani iliyopo katika Taifa letu.

Hatahivyo, Waziri alisema ajira lazima zitapatikana katika maeneo husika kutokana na mitambo ya gesi inayojengwa, na kusisitiza kuwa 


EmoticonEmoticon