VURUGU BADO ZINAENDELEA MOROGORO, MKUU WA MKOA ATINGA ENEO LA TUKIO



 Watu wanne wanahofiwa kufa katika vurugu zinazoendelea wilaya ya Kilosa- Dumila baada ya kuvamia kijiji kilicho sababisha vurugu hizo ambacho kilikuwa kimetengwa kwaajili ya Wakulima

Mkuu wa Mkoa huo Bwana. Joel Bendera, licha kukataa kuwa nje ya mkoa huo lakini kwa taarifa za kuaminika zilizoifikia Blog hii nikuwa mkuu wa Mkoa huo tayari amefika eneo la Tukio ilikuwatuliza Wananchi

Wananchi hao waliifunga barabara kuu ya kuelekea Dodoma kwa masaa kadhaa na kufanaya fuj, Aidha kulikuwa na msururu wa magari ya Abiria na Mizigo yakiwa upende wa kutoka Dumila kwenda Kilosa yakisubiri barabara hiyo kufunguliwa. 

Wananchi waliofunga barabara ya Dumila kwaajili ya fujihizo
Mawe maukubwa na Magogo yaliwekwa njiani ilikushinikiza serikali kuwasikiliza na kutekeleza madai yao. Madai hayo ni juu ya Wafugaji waliopewa eneo la Msowero ambalo pia wakulima wanaliitaji.


Hatahivyo Wananchi hao wa kijiji cha Mambwegwa na Msowero katika Wilaya ya Kilosa tayari walisha kutana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Halima Dendego aliyoenda kuyasikiliza madai yao.

 

Picha na Habari kwa hisani ya
www.oneloveTz.blogspot.com pamoja


EmoticonEmoticon