TCRA WATANGAZA NEEMA MATUMIZI YA SIMU, WAFANIKIWA KUDHIBITI MAKAMPUNI NCHINI

TCRA WATANGAZA NEEMA MATUMIZI YA SIMU, WAFANIKIWA KUDHIBITI MAKAMPUNI NCHINI


Gharama za kupiga simu kutoka mtandao wa kampuni moja ya simu ya mkononi kwenda mwingine nchini, kuanzia Machi Mosi mwaka huu zitashuka kutoka sh.115 hadi sh.34.9 kwa dakika moja.

Uamuzi huo umefanywa na mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) baada ya kufanya mapitio ya gharama za mwingiliano kwa kampuni za simu nchini kwa mwaka 2013. Pia kuanzia Januari Mosi mwakani gharama hizo zitapungua hadi sh.32.4.

Vilevile Januari 2015 gharama hizo zitashuka na kufikia sh. 30.6, Januari 2016 gharama hizo zitadhuka mpaka sh. 28.6, Januari 2017 zitashuka mpaka sh.26.9 kwa dakika moja.

Akitangaza bei uamuzi huo jijini Dsm jana, Mkurugenzi Mkuu wa TCRA, Profesa John Nkoma alisema umetolewa kwa mujibu wa sheria ya TCRA ya mwaka 2003 sura 172. Profesa Nkoma alisema viwango hivyo ni vya kikomo cha juu na pia ni bei elekezi lakini akasema kampuni za simu zina uhuru wa kukubaliana kibiashara ili mradi makubaliano yao yasizidi gharama zilizoelekezwa na TCRA.

    Baadhi ya sababu ya mabadiliko ya gharama za kupiga simu:
  • Kumpa mtumiaji uhuru wa kuongea bila kubadilisha badilisha laini
  • Kumpunguzia mtumiaji mzigo wa kubeba simu na laini nyingi
  • Gharama za simu nchini Tanzania ziko juu ukilinganisha na baadhi ya nchi barani Afrika
  • Kudhibiti ukiritimba wa gharama zinazotozwa haswa mtu ananapopigia mtandao mwingine

Mhe. PINDA - WANANCHI WA MTWARA WALIPOTOSHWA

Waziri Mkuu akiwa Bungeni siku za Nyuma


WAZIRI Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda ametoa ufafanuzi wa kile kilicho jiri Mtwara na kusababisha vurugu kubwa ambazo zilipelekea nyumba kuchomwa moto hasa za ziongozi wakati wananchi wa Mkoa huo wakipinga swala la kusafirishwa kwa bomba la Gesi kutoka Mtwara kuja Dar es salaam

Akiongea leo Bungeni katika kipindi cha maswali na majibu kwa waziri Mkuu, alitoa kilekilicho sababisha vurugu kwa wakazi hao na kusema ni upotoshaji tu ulifanyika

Mhe. Pinda amesema kuwa Serikali na Viongozi hawa kutoa elimu na ufafanuzi wakutosha kwa wakazi wa Mtwara ilikujua nijinsi gana watanufaika na Mradi wa Gesi ulioko mkoani mwao

" Nakiri kuwa swala la elimu ya kutosha kwa wakazi wa Mtwara aikutolewa, na kumekuwa na upotoshaji wa taarifa huku wengine wakidai kuwa Gesi hiyo itapelekwa kwao Raisi Jakaya kitu ambacho sio kweli" Alisema 

                 Mwigulu alia chuo cha uzoefu kianzishwe

Akimuuliza swali Waziri Mkuu, Mhe. Mwigulu Nchemba alishangwaza na kitendo cha serikali kulalamika kukosa wafanya kazi huku kukiwa na wahitimu wengi wa vyuo vikuu ambao hawajapata kazi hadi hizi sasa

"Kwanini serikali inalalamika haina wafanyakazi wakutosha katika halamashauri zake wakati kuna idadi kubwa ya wanafunzi mitaani, lakini wanakwamishwa na swala la uzoefu je kuna uwezekano wakuanzisha chuo cha Uzoefu" Aliuziza Mbunge Huyo


Mhe. Mwigulu amesema, kila mtaa kuna mwanafunzi aliye hitimu elimu ya juu tena katika vyuo vyenye hadhi ya juu na kuitaka serikali kuwatumia hao, lakini pia alisisitiza kipengele cha Uzoefu kifutwe na kumatakla waziri mkuu kutoa tamko la kufuta kipengele hicho
Aidha waziri mkuu alijibu kwakukataa kuwepo kwa upungufu wa wafanyakazi katika almashauri hizo, na kusema kuwa kama serikali hawana seemu ya kuitaji huzoefu

"Wala sisi atuitaji uzoefu kwani uzoefu ndio anaenda kuupata pale kwenye Almashauri anapoenda kufanya kazi lakini pia hatuwezi kuwaajiri wote wanao hitimu katika sekta ya umma" Alisema Waziri Mkuu

TANGA, DODOMA KUAMIA DIGITALI LEO USIKU

TANGA, DODOMA KUAMIA DIGITALI LEO USIKU


WAKAZI wa Miji ya Tanga na Dodoma wamepokea kwa hamasa kubwa zoezi la kuamia Digitali kuliko ilivyo kuwa kwa wakazi wa Jiji la Dar es salaaam, kwani wakazi wengi wa maeneo hayo tayari walisha nunua Vingamuzi

Ikiwa leo ni siku ya kuzimwa kwa Mitambo ya Analogia ifikapo saa sita usiku, Msemaji wa TCRA bwana Inocent Mungy ambaye ni msemaji wa TCRA amesema hayo hii leo kwanjia ya simu akiwa mkoani Dodoma, kuwa leo usiku kwa mikoa hiyo miwili mitambo ya Analogia itazimwa na kuwashwa ya Digitali

Aidha, amesema kwa mkoa wa Tanga tayari watu elfu 20 wameamia Digital hatakabla ya mitambo hiyo kuzimwa, Na mkoani Dodoma hali iko hivyohivyo kwani tayari watu elfu 27 wameshaamia Digitali, huku idadi ndogo ya watu wasio zidi elfu 35 wakiwa ndio bado hawajaamia lakini niwengi sana walio jiandaa kuamia kwa siku ya leo

Lakini bwana Inocent amesema, kuanzia leo asubuhi kulikuwa na msururu wa watu wasiozidi 15 wakisubiri kununua Ving'amuzi kwa mawakala mbali mbali mkoani Dodoma

“Kwa mkoa wa Dodoma tumefanya majaribio katika maeneo ya Nong'ono nyuma ya chuo cha UDOM, tayari Digital ikosawa kwa kutumiwa na kufikia muda halali tutazima mitambo ya Analogy” alisema bwana Mungy

Hatahivyo bwana Mungy, amewataka wananchi kusema aina ya Tv aliyo nayo, pamoja na eneo analo kaa kama ni bondeni au eneo la Tambarare ilikuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza, na kuongeza kuwa kuna umuhimu wa kwenda na mtaalamu wa kuunganisha king'amuzi wakati wa kuunganisha king'amuzi hicho

Kama kuna mtu anamalalamiko yoyote nimuhimu kuyafikisha mahali aliponunua king'amuzi kwani, tayari wamepokea malalamiko 180 na kuyafanyia kazi.

Pia bwana mungi amekanusha uvumi unaoenezwa na vyombo vya habari kuwa kuna ina ya Kinga'amuzi ambacho kitazimwa ifikapo June mwaka huu kuwa sio za kweli na kuwataka wanao eneza uvumi huo kuacha maramoja
WAFANYAKAZI- RIPOTINI MKINYANYASWA

WAFANYAKAZI- RIPOTINI MKINYANYASWA

 

SERIKALI IMEWATAKA WAAJIRI WANAO NYANYASA WAFANYAKAZI KUACHA MARAMOJA, HUKU IKIWASISITIZA WAFANYAKAZI KUZIJUA SHERIA ZINAZO WALINDA NA KURIPOTI KWENYE VYOMBO VYA SHERIA PINDI WANAPOPATWA NA MGOGORO NA WAAJIRIWA WAO

 Habari zaidi


Serikali imetoa onyo kwa waajiri wote hususani wale wawekezaji wanaowanyanyasa wafanyakazi kuacha maramoja kwani itawachukualia hatua stahiki na kuwataka watambue kuwa wamekuja kuleta ajiira stahiki na sio manyanyaso kwa wafanyakazi.

Akiongea leo Bungeni Naibu Waziri wa Wizara ya Kazi Mhe. Dr Milton Makongoro Mahanga wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Mariam Msabaha, ambaye alitaka kujua nihatua zipi serikali inachukua kwa waajiri ambao wanawanyanyasa wafanyakazi wao, Mahanga amesema nilazima waajiri watambue umuhimu wa haki kwa wafanyakazi wao

Aidha, amewaomba wafanyakazi kuelewa sheria zinazowalinda kazini na kuwasisitiza kutoa tarifa pale wanapokosa haki zao

Hatahivyo, tayari waajiri 13 wamefikishwa Mahakamani kwa kosa la kuwanyanyasa wafanyakazi wao, huku kukiwa na tafiti mbalimbali ambazo zinafanywa na wizara ya kazi ilikuweza kudhibiti hali hiyo, huku elimu ikitolewa kwa waajiri na wafanya kazi kuondoa tatizo hilo. Alisema Dr Milton 

MWIGULU AWAFUNGULIA MLANGO WA NEEMA WANAFUNZI ELIMU YA JUU

MUSWADA WA MAREKEBISHO YA MFUMO WA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI UMEPITISHWA HII LEO  ILIKUWEZA KUFANYIWA MAREKEBISHO .Habari zaidi

Mhe. Mwigulu Nchemba akiongea Bungeni siku za nyuma   

Mbunge wa Iramba Magaribi na Naibu katibu mkuu wa CCM- Bara, Mhe. Mwigulu Nchemba leo amewasilisha hoja binafsi yakuiomba serikali kukubali kuleta muswada wa marekebisho ya sheria ya mfuko wa Elimu ya juu (Higher Education Fund) ilkutatua matatizo ya muda mrefu ambayo hulalamikiwa juu ya mfuko huo

Akiongea Bungeni, Mhe. Mwigulu amesema endapo Serikali itakubali kufanya marekebisho, itaipunguzia mzigo wa kugarimia Elimu ya juu katika Bajeti yake (Serikali) kwani hata Wizara zitagaramia helimu ya juu, kuliko mfumo uliopo sasa ambao umekuwa na malalamiko mengi wa kutenga bajeti kwaajili ya shuguli hiyo

"Tukiweka mfumo wa kila wizara kugarimia helimu ya juu kupitia fedha zake za matumizi Mengineyo kwa asilimia 80%, itasaidia Serikali kupata kiwango cha 100% kwakila mwanafunzi, kwani itawezesha kutobagua niyupi apewe mkopo na yupi asipewe" Alisema Mwigulu

Aidha, Alieleza kuwa mfumo ambao unamlazimu mwanafunzi anaye taka mkopo kusomea fani asiyo ipenda iliapate mkopo sio mzuri, kwani wengi husoma fani wasizozipenda. Alisema Mwigulu

Hatahivyo Hoja hiyo binafsi ilipitishwa kwa kishindo na Wabunge wote ambayo ilielezea Sababu za kwanini Serikali ilete mswada wa marekebisho ya sheria hiyo Bungeni

KUTOKA BUNGENI DODOMA LEO


               HABARI
> MUSWADA WA MAREKEBISHO YA MFUMO WA MIKOPO KWA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU NCHINI UMEPITISHWA HII LEO  ILIKUWEZA KUFANYIWA MAREKEBISHO .



>  SERIKALI IMEWATAKA WAAJIRI WANAO NYANYASA WAFANYAKAZI KUACHA MARAMOJA, HUKU IKIWASISITIZA WAFANYAKAZI KUZIJUA SHERIA ZINAZO WALINDA NA KURIPOTI KWENYE VYOMBO VYA SHERIA PINDI WANAPOPATWA NA MGOGORO NA WAAJIRIWA WAO

HABARI YA BIASHARA

>  KUTOKANA NA NCHI JIRANI YA KENYA KUVUNA KIASI CHA TANI LAKI NNE (400,000) HUKU  TANZANIA IKIVUNA KIASI CHA TANI MIAMOJA TU (100), KUTOKA KATIKA RASILIMALI ZINAZO PATIKANA BAHARINI, SERIKALI IMESEMA IMEJIPANGA VYEMA KATIKA KUVUNA RASILIMALI HIZO NA KUFIKIA KIWANGO CHA JUU ZAIDI .

Muda mfupi ujao utaletewa habari zaidi kutoka Bungeni

Spika wa Bunge, Mama Anne Makinda ameahirisha Bunge mpaka kesho saa tatu asubuhi

KIMBUNGA FELLENG CHAJA, MIKOA 8 KUADHIRIKA

Picha kuonyesha kimbunga hicho (kaskazini-mashariki mwa Madagascar)


Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania, inahu tahadharisha umma juu ya uwezekano wa matukio ya mvua kubwa ya zaidi ya Milimita 50 kuanzia tarehe 30 January mpaka February 01 mwaka huu.






Taarifa hiyo, inasema kutakuwepo na Kimbunga kinatojulikana kama ' FELLENG ', kaskazini-Mashariki mwa Madagascar ambacho kinavuta upepo wenye unyevunyevu kutoka Congo kupitia maeneo mbalimbali ikiwemo Tanzania

Aidha baadhi ya maeneo yatakayo adhirika ni Mkoa wa Rukwa, Iringa,Ruvuma, Mbeya, Mtwara, Njombe na Morogorona. Mvua itanyesha kwa saa 24 mfululizo kwa tarehe zilizo tajwa hapo juu

GESI SASA KUBAKI MTWARA NA MEGAWATI 600 ZA UMEME KUZALISHWA HUKO


Waziri Mkuu Mizengo Pinda akiongea na wakazi wa Mtwara hapo Jana

Habari nilizo pata toka mtwara muda simrefu

KUPITIA, kikao kilicho kaa kwa siku mbili mfululizo katiya Wajumbe mbalimbali wanao wakilisha wanachi wa Mtwara na WAZIRI Mkuu, Hatimaye Gesi Kubaki Mtwara na itazalishwa eneo la Madimba huku kiwango kidogo cha Gesi kikisafirishwa kuja Dar, lakini Mtwara ndipo kutakuwa na Gridi kubwa ambayo ita zalisha Megawati 600 za umeme.

Mawaziri 6, hii leo wametua mkoani Mtwara kumuunga mkono Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kwaajili ya Kuongea na wakazi wa Mtwara juu ya mgogoro wa mbola la Gesi kutoka Mtwara kuja Dares salaam. Mgogoro uliodumu kwa wiki mbili sasa

Mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli), Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, - (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt. Shukuru Kawambwa).

Wajumbe wengi katika kikao hicho wamekataa swala la Bomba la Gesi kutoletwa Dar es salaa, Miongoni mwa mambo yaliyo ibuka katika kikao hicho, nipamoja na baadhi ya wajumbe kumkataa Mkuu wa Mkoa na kumwambia Waziri mkuu aondoke naye


Moja kati ya Mitambo ya kuzalishia Gesi huko Mtwara

Mengine ni pamoja na kauli ya Hawa Gasia, ya kutoa kauli za uongo kuusu MtwaraVijijini kuunga mkono suala la Gesi kwenda Dar huku Madiwani wa Mtwara nao wakidai hawakuusishwa juu ya swala hilo.






Kikao kinafanyika chini ya ulinzi mkali wa FFU, JWTZ na UWT (Usalama wa Taifa). Wananchi wa Mtwara na maneo ya Lindi wamekuwa na mgogoro wa wiki mbili juu ya Mbomba la Gesi kusafirishwa kuja Dar.

SERIKALI KUONGEZA DAWA ZA MAGONJWA NYEMELEZI YA UKIMWI

WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII MHE.
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii kupitia mpango wa Taifa wa kudhibiti Ukimwi NACP, imetenga fungu maalum kwaajili ya kununulia Dawa za kudhibiti magonjwa nyemelezi ya ugonjwa huo ilikukabiliana na uhaba wa Dawa na Vifaa tiba katika vituo vyote vya umma

Akiongea leo Bungeni leo wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mhe. Magreth Mkanga, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mhe. Dr Hussein Mwinyi amesema Serikali itahakikisha kuwa dawa hizo zinapatikana kwa wingi katika vituo vya Afya ili kudhibiti uhaba wa Dawa hizo za magonjwa nyemelezi

Aidha Dawa kama za Kifua kikuu, Kisonono na Malaria zinapatikana Bure Bila malipo kwa watu wenye Virusi vya Ukimwi katika vituo vyote vya kutolea huduma za Afya za umma na baadhi ya vituo Binafsi ambavyo vimeidhinishwa na Wizara hiyo

WATANZANIA WAKOSA MJADALA WABUNGENI LEO


Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mkutano wa 10, Limeanza leo Mkoani Dodoma, huku Watanzania wengi wakikosa mkutano huo kutokana na Shirika la Utangazaji la TBC kushindwa kurusha matangazo yanayoendelea kutokana na tatizo la Mitambo

Muda mfupi baada ya muda rasmi wa Bunge kuanza Shirika hilo lilitangaza na kuomba radhi kwakushindwa kurusha matangazo hayo ya moja kwa moja kutoka Bungeni Dodoma

Mkutano wa Bunge unatarajiwa kufanyika kwa wiki Mbili Mfululizo, ambapo maswala mbalimbali yanajadiliwa huku wengi wakisuburi kujua juu ya swala la Gesi litakavyo kwenda miongoni mwa viongozi wa Serikali.

HABARI PICHA - MTWARA


waziri wa mambo ya ndani ya nchi Mhe. Emanuel Nchimbi akitoka Masasi kuelekea Mtwara Mjini

Habari nilizo nazo hadi sasa

Mawaziri wapatao 6, wako Mkoani Mtwara kujadili matatizo ya Gesi, mawaziri hao ni pamoja na Waziri wa Ujenzi (Dkt. John P. Magufuli), Waziri wa Uchukuzi (Dkt. Harrison Mwakyembe), Waziri wa Viwanda na Biashara (Abdallah Kigoda), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, - (Dkt. Mary Nagu) na Waziri wa Elimu (Dkt. Shukuru Kawambwa).

Waziri Mkuu Mizengo Pinda bado yuko huko pamoja na Viongozi wa Kidini wa Kiislamu pamoja na wa Kikristo wakijaribu kutatua tatizo hilo. Wananchi wa Mtawara kwa wiki mbili sasa wamekuwa na mgogoro na Serikali juu ya mradi wa Bomba la Gesi.

ALIYE KWAMISHA DHAMANA YA LULU HUYU HAPA

LULU AKIRUDISHWA MAHABUSU HII LEO
WAKATI Jaji  wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Zainabu Mruke akimwachia Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael Kimemeta (Lulu) kwa dhamana yenye masharti matano ,Msajili wa Mahakama Kuu Amir Msumi amekwamisha dhamana ya msanii huyo na kumlazimu kurudi rumande mpaka kesho.

Lulu awezi kurudi nyumbani ingawa ametimiza masharti ya dhamana, kwa sababu msajili wa mahakama ambaye ndiye mwenye mamlaka kisheria ya kuidhinisha dhamana yake  ayupo ofisini, kwa hiyo Lulu atarudishwa tena Mahakamani ilikusaini dokomenti zake za dhamana mbele ya Msajili wa Mahakama hiyo

GESI YAZUA U CCM NA UCHADEMA, KISA KUWAITA WAANDAMANAJI NI WAHUNI

HUKU ziongozi wajuu wakiendelea na vikao hii leo, Mkoani Mtwara juu ya vurugu zilizojiri kwa wiki sasa kutokana na mzozo wa GESI kusafirishwa kuja Dar, Wabunge wa Chadema Wamtupia vibomu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Bwana. Nape Nnauye juu ya swala la Gesi

Wabunge hao ni Mhe. Zitto Zuberi Kabwe Mbunge wa Kigoma, na Mhe. Halima James Mdee Mbunge wa Jimbo la Kawe, wakimtupia vijembe Bwana Nape Nnauye ambaye ni Katibu wa Halmashauri kuu ya Taifa ya CCM, Itkadi na Uenezi.

Vibomu hivyo ambavyo walikuwa wakitupiana kwenye mtandao wa TWITER, Nibaada ya Bwana Nape Nnauye kusema kuwa wanaofanya Vurugu hizo ni wahuni na sio matatizo ya mzozo wa Gesi unaoendelea

Baadhi ya hizo TWEETS za ziongozi hao hizi hapa, kutoka kwa kiongozi mmoja kwende kwa mwingine

 
 





                                       ***************************
 


NEEMA KWA LULU, SASA KURUDI TENA URAIANI


Mahakama kuu Kanda ya Dar es Salaam imempatia dhamana msanii wa Filamu Elizabeth Michael (Lulu) kwa masharti ya kupata wadhamini wanaofanya kazi Serikalini wakiwa na Sh 20milioni kila mmoja, kuacha hati yake ya kusafiria mahakamani,kuripoti mahakamani na wafadhili kuweka bondi ya Shilingi mil 20

Hivi sasa yupo katika maeneo ya  Mahakama hiyo akisubiri kukamilisha taratibu ili aweze kurudi nyumbani kwake.Miongoni mwa masharti mengine ni pamoja na kutoruhusiwa kumtoka nje ya Dar es salaam, na kwamba atawajibika kuripoti kila tarehe moja ya mwenzi mahakamani hapo
Lulu Michael anayekabiliwa na tuhuma za mauaji ya kuuwa bila kukusudia ya Msanii mwenzake Steven Kanumba April 72012, Leo Lulu amepata dhamana baada ya kukamilisha masharti ya mahakama.

BREAKING NEWSSSSSSSSSSSSSS

VURUGU TENA MTWARA- KITUO CHA POLISI CHA VAMIWA, MWANDISHI WA KITUO CHA CHANEL TEN AJERUHIWA KATIKA TUKIO HILO


Habari zakuaminika  zilizo rushwa na kituo cha Television cha EATV kipindi cha Hotmix hivi sasa, zinasema Kumetokea tena vurugu Mkoani Mtwara, ambapo kituo cha Polisi kimechomwa moto pamoja na Mwaandishi wa Habari wa Chanel Ten amejeruhiwa katika Vurugu hizo hata hivyo aikuelezwa kama kuna mtu amepoteza maoisha katika tukio hilo

UP DATES

Habari zaidi kutoka kwa mashuhuda huko Mtwara, Uharibifu ni mkubwa sana kwani IKULU ndogo imevamiwa na nyumba ya Mbunge Hawa Gasia imevamiwa. JWTZ na Mahakama pia zimevamiwa na inasemekana pia zimechomwa moto huku Polisi nao wakiendelea kupiga mabomu kuwatawanya wananchi hao

Chanzo cha Habari kinasema, Vurugu hizo zimetokana na Imani za Kishirikina pamaja na Askari Jeshi aliye waita wenzake na kuvamia wananchi baada ya kupigwa.

Mwandishi wa Chanel Ten aliye jeruhiwa ni JOHN KASEMBE na tayari amefikishwa Hospitali kwa matibabu zaidi

Habari zaidi utaendelea kujuzwa juu ya Habari hii 

VURUGU BADO ZINAENDELEA MOROGORO, MKUU WA MKOA ATINGA ENEO LA TUKIO



 Watu wanne wanahofiwa kufa katika vurugu zinazoendelea wilaya ya Kilosa- Dumila baada ya kuvamia kijiji kilicho sababisha vurugu hizo ambacho kilikuwa kimetengwa kwaajili ya Wakulima

Mkuu wa Mkoa huo Bwana. Joel Bendera, licha kukataa kuwa nje ya mkoa huo lakini kwa taarifa za kuaminika zilizoifikia Blog hii nikuwa mkuu wa Mkoa huo tayari amefika eneo la Tukio ilikuwatuliza Wananchi

Wananchi hao waliifunga barabara kuu ya kuelekea Dodoma kwa masaa kadhaa na kufanaya fuj, Aidha kulikuwa na msururu wa magari ya Abiria na Mizigo yakiwa upende wa kutoka Dumila kwenda Kilosa yakisubiri barabara hiyo kufunguliwa. 

Wananchi waliofunga barabara ya Dumila kwaajili ya fujihizo
Mawe maukubwa na Magogo yaliwekwa njiani ilikushinikiza serikali kuwasikiliza na kutekeleza madai yao. Madai hayo ni juu ya Wafugaji waliopewa eneo la Msowero ambalo pia wakulima wanaliitaji.


Hatahivyo Wananchi hao wa kijiji cha Mambwegwa na Msowero katika Wilaya ya Kilosa tayari walisha kutana na Mkuu wa Wilaya hiyo, Halima Dendego aliyoenda kuyasikiliza madai yao.

 

Picha na Habari kwa hisani ya
www.oneloveTz.blogspot.com pamoja

DHAMANA YA LULU YAPIGWA KALENDA




Lulu akiwa anatoka Mahakama ya Kisutu chini ya ulinzi wa Askari Magereza. Picha na Loyce Joseph




MAHAKAMA Kuu kanda ya  Dar es Salaam imebadilisha siku ya kusilizwa kwa maombi ya dhamana ya Mwigizaji nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael, maarufu kwa jina la Lulu,kutoka  Ijumaa ya kesho hadi Juma tatu ya January 28 mwaka huu, na Kiasi cha Milioni 20 kinaitajika ili kuweza kuwekewa dhamana hiyo

 Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua aliyekuwa msanii mwenzake wa fani hiyo, Steven Kanumba, bila kukusudia.

Taarifa za ndani kutoka Mahakamani hapo zilizolifikia Blo hii na kudhibitishwa na vyanzo vya ndani kutoka Mahakamani hiyo zimedai kwamba msanii huyo anaweza kupata dhamana hiyo na kurudi uraiani huku akipangia tarehe nyingine ya kuwasilini Mahakamani hapo kwa ajili ya kesi hiyo.

Awali Lulu alikuwa akikabiliwa na kosa la kuua kwa kukusudia, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, lakini baada ya upelelezi kukamilika alibadilishiwa mashtaka na kuwa ya kuua bila kukusudia, kisha kesi hiyo ikahamishiwa Mahakakama Kuu. 
UFISADI WAIBUKIA GEITA, KAMATI YA BUNGE YABAINI

UFISADI WAIBUKIA GEITA, KAMATI YA BUNGE YABAINI

Kamati ya Bunge ya hesabu za Serikali za mitaa nchini, Leo imekataa kupokea hesabu za halmashauri ya wilaya ya Geita kutokana na mapungufu ambayo yanaviashiria vya uwepo wa ubadhirifu wa kiasi kikubwa cha Pesa

Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati hiyo, Mbunge wa Kinondoni Mhe. Idd Azan amesema kuwa mambo yanayotiliwashaka ni pamoja na fedha zaidi ya shilingi Milioni 800 zilizotumika katika ujenzi wa kituo cha mabasi cha Geita pamoja na kiasi cha shilingi Bilioni 1.9 za mradi mbalimbali ya maendeleo ya zilizotenga na jinsi zilivyotumika.

SERIKALI YATAKIWA KUSHUGULIKIA UKIUKWAJI WAHAKI ZA BINADAMU NCHINI



SERIKALI ya Tanzania imekosa mfumo wa uhakika wa kushugulikia malalamiko ya matukio ya ukiukwaji wa Haki za binadamu hapa nchini, Mtandao wa watetezi wa Haki za binadamu nchini waeleza


Raisi wa Jumuhiya ya Wanasheria Tanganyika, ambaye pia ni mwanachama wa Mtandao huo. Wakili Francis Stolla amesema kumekuwa hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa pale ambapo mashirika na asasi za kulinda haki za binadamu zinapopiga kelele juu ya swala hilo

“Kumekuwa na mauaji mbalimbali yanayo laaniwa na kugusa hisia za watu, tena zinazotumia nguvu kama Risasi lakini sheria za uundwaji wa Tume ambazo zinaundwa na serikali, wakati huohuo serikali ndio inatuhumiwa, aifanyi haki kutekelezwa” Alisema Wakili Francis

Uundwaji wa Tume umekuwa sio mzuri, ucheleweshwaji wa kuchukua hatua mpaka wananchi wana lalamika, kwani wahusika hawafikishwi mahakamani hata pale tume inapopeleka Ripoti na Uchunguzi wake kwa serikali lakini hatua madhubuti hazichukuliwi. Alisema Francis

“Kunachombo ambacho akiegamii upande wowote ambacho ni KORONA, chombo hiki kipochini ya Mahakama kwani mahakama ndio imepewa mamlaka ya kutenda haki pale Serikali inapokuwa kwenye mgogoro na Wananchi wake, kitu ambacho nacho hakifanyiwi kazi vizuri” Alisema Francis

Hatahivyo Wakili huyo amesema, Hatawale wanaotetea haki za binadamu nchini nao wanaitaji kulindwa kisheria ilikuwa na usalama wa maisha yao. Alisema Wakili Francis

NEW YORK KUAMIA TANZANIA HIVI NDIVYO KIGAMBONI ITAKAVYO KUWA BAADA YA MRADI KUKAMILIKA

           



        Hivi ndivyo maeneo makuu katika mji huo yatakavyo onekana kwa mpangilio maalum. kuna eneo la Biashara, Utalii kama ilivyo pichani Daraja na eneo la 3D pia litakuwepo

 Habari zaidi utaendelea kupata hapahapa juu ya Mji Mpya wa Kigamboni ................

MJI WA KIGAMBONI SASA KUWA WILAYA RASMI







Serikali ya Tanzania imetangaza rasmi mji wa Kigamboni wa jijini Dar es salaam kuwa Wilaya kamili inayojitegemea, na kufanya mkoa wa Dar es salaam kuwa na Wilaya nne

Akiongea na Waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam, Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya makazi Prof. Anna Tibaijuka amesema kuanzia sasa mji wa Kigamboni utatoka na chini ya manispaa ya uongozi wa manispaa ya Temeke.
“ Kigamboni itajitegemea kama Wilaya kuanzia  leo, na utakuwa chini ya  Kigamboni Development Agency (KDA)”. Alisema Prof. Tibaijuka
 
Kutengwa kwa Mji mpya wa Kigamboni kuwa Wilaya, kumekuja baada ya kuundwa kwa chombo kijulikanacho kama Wakala wa Uendelezaji wa Mji Mpya wa Kigamboni inayojulikana kwa Lugha ya Kiingereza kama Kigamboni Development Agency (KDA), Alisema Prof. Tibaijuka

KDA, itakuwa na jukumu la kuendeleza Kigamboni kuwa mji wa Kisasa, na kufafanua kuwa shuguli zote za kiserikali zitasimamiwa na chombo hicho kwa kushirikiana na baraza la ushauri la mji wa Kigamboni. Alisema Prof. Tibaijuka

Hatahivyo, Baraza la ushauri wa Wilaya ya Kigamboni utaundwa kwa kushirikisha wawakilishi wa wananchi pamoja na Madiwani na Wabunge wa eneo hilo.

IDADI YA VIJANA  WALIOJIUNGA NA ELIMU YA JUU YAONGEZEKA

IDADI YA VIJANA WALIOJIUNGA NA ELIMU YA JUU YAONGEZEKA



IDADI ya vijana wanaojiunga na mafunzo ya elimu ya juu nchini Tanzania imeongezeka na kufikia laki moja na elfu ishirini na tano, baada ya serikali kukamilisha ujenzi wa vyuo vya elimu ya mafunzo ya ufundi stadi katika mikoa mine nchini

Waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa, amesem Hayo wakati wa ziara ya naibu spika wa Bunge la Korea Kusini Park Byeong-Seug, ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi

Kwa mujibu wa Waziri Kawambwa, Ujenzi wa vyuo hivyo umetokana na mkopo wa Dola za Marekani Millioni 8, zaidi ya shilingi Billioni 10 za Tanzania ilioupata kutoka Serikali ya Korea Kusini

Waziri Kawambwa ameongeza kuwa mara baada ya kukamilika Ujenzi wake, vyuo hivyo vimefanikiwa kudahili Wanafunzi 1160,sawa na ongezeko la asilimia 1 ya uwezo wa vyuo vyote nchini. Alisema Waziri

WANAFUNZI 450 HUFARIKI KILA KWAKA NCHINI KISA, UKOSEFU WA VYOO MASHULENI






NAIBU Waziri wa Afya na ustawi wa Jamii, Mhe. Dkt Seif Rashid amekiri kuwepo kwa upungufu wa Vyoo katika Shule za msingi nchini, na kwamba tayari wanafunzi zaidi ya 450 wamefariki dunia kutokana na magonjwa ya homa ya matumbo kutokana na vyoo hivyo kuwa vichafu kinyume cha utaratibu wa kiafya

Akiongea na Waaandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Naibu waziri huyo amesema kuwa miongoni mwa wagonjwa wanaohudhuria hosibitali kwaajili ya kupata matibabu ya magonjwa ya Tumbo na kuhara ni wanafunzi, ambapo kila mwaka ni wanafunzi 45o hufariki dunia kwa maradhi hayo. Alisema Drkt Seif

“ Hali ya kukosekana kwa vyoo vyenye mazingira salama kiafya, imesababisha daadhi ya wanafunzi kuugua magonjwa ya uambukizo yakiwemo magonjwa hatari kama homa ya matumbo, kuhara damu na hata ugonjwa wa kipindupindu” Alisema Dkt. Seif

Hatahivyo, Asilimia 86 ya shule zilizopo nchini Tanzania, hazina mazingira na miundombinu rafiki kwa watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali ukiwemo wa viungo, kwani ni alisimia 4 tu ya shule nchi nzima ndio zina niundombinu ya choo kwa watu wenye ulemavu.

“Bado hatuna miundombinu ambayo ni rafiki kwa watu wenye ulemavu kutokana na asilimia ndogo sana ya shule zetu ndio zenye miundombinu hiyo, ambayo ni asilimia 4 tu kwa nchi nzima” alisema Dkt. Seif

Mojawapo katiya malengo ya Serikali ndani ya Sekta ya Elimu, ni kufanikisha matumizi ya Tundu  moja la choo kutumiwa na wanafunzi 20 kwa watoto wakike huku wakiume wakitumia tundu moja wanafunzi 25, mpango ambao haujafanikiwa hadi hivi sasa. Na kwa mkoa wa Dar es salaam ni shule 6 tu ndizo zina miundombinu ya choo kwa uwiano wa idadi ya wanafunzi.

Kategori

Kategori