WALIO PANGISHA NYUMBA ZA NHC KIHOLELA KUTIMULIWA

Watu waliopanga nyumba za shirika la Nyumba la taifa kiolela sasa kutimuliwa bila notisi endapo hawata timiza mashariti waliopewa na shirika hilo ndani ya miezi mitatu iliobaki


Akitoa taarifa hiyo kwa umma, Mkurugenzi wa usimamizi wa rasilimali za shirika la Nuyumba Bwana Hamad Abdala amesema, wametoa miezi mitatu iliwaweze kuhalalishwa ukaaji wao kwani kukaidi agizo hili fursa yakutambuliwa haitakuwepo tena.


Baada ya Fursa hii kupita nyumba hizo zitapangishwa kwa watu wengine, kwani kukaa bila mkataba kwa sababu yoyote ile inamaana makubaliano na masharti ya upangaji na shirika hilo sio hahali. Alisema Abdala

Kama itapita mwezi mmoja bila kutimiza masharti hayo, itachukuliwa kuwa ni ukiukaji wa mashrti ya upangaji kwamaana hiyo shirika litalazimika kuwatoa kwani watakuwa wameonyesha kuwa hawaitaji upangaji. Alisema Abdala

Hivi sasa mkataba wa upangaji umebadilika nakuwa ya miaka mitatu nasiyo ya awali ambapo mpangaji alikuwa akipanga moja kwa moja

Aidha mwaka 2010 shirika la nyumba liliwatangazia watu wote waliopangishwa kwenye nyumba za shirika kinyume cha taratibu kujitokeza iliwaweze kupewa upangaji lakini hali hiyo imejirudia tena na kuilazimu shirika hilo kutoa miez mitatu kwa wale wote waliopanga kiholela kutafuta upangaji wahalali


EmoticonEmoticon