MIZENGWE YA MITAALA YA ELIMU SASA KUJULIKANA, KAMATI YA UNDWA KUICHUNGUZA


> JE MHESHIMIWA MBATIA ATAJIUZULU IKIWASILISHWA
> KAMATI IKIBAINI MADUDU NANI ATAWAJIBISHWA






Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi Mhe. Shukuru Kawambwa leo Bungeni amewasilisha mitaala kwa elimu ya Msingi na Sekondari wa mwaka 2005 kama ambavyo iliahidiwa na Serikali kupitia kwa Mhe.Wiliam Lukuvi ambaye ni Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu na Bunge, kuwa Mitaala hiyo ingewasilishwa kabla ya Bunge kumalizika hapo tarehe 8 mwezi huu

Baada ya Waziri wa Elimu kuwasilisha mbele ya Bunge Mitaala hiyo Naibu Spika Job Ndugai ameunda kamati yakuchunguza mitaala hiyo kama imechakachuliwa au aina mapungufu yoyote

Kuundwa kwa kamati hiyo kumetokana na maoni ya wabunge waupinzani kusema kuwa huenda ikachakachuliwa kwa haraka ilikuwafumba watanzania. 

" Siku yakuwasilishwa kwa hoja hii kulikuwa na wasiwasi kuwa hata Mitaala ikiwasilishwa hapa haitakuwa halisi na halali nahii ndio sababu ya kuteua kamati ya baadhi ya Wabunge ilikufanya ukaguzi juu yamadai hayo" alisema Naibu Spika

Miongoni mwa wabunge 5 waliochaguliwa na mheshimiwa James Mbatia alikuwemo na baadhi ya viongozi wa serikali, ambao ni Mhe. Magreth Sitta, Mhe. Benadetha.

Aidha, Mhe. James Mbatia aliwasilisha hoja binafsi kuusu udhaifu uliopo kwenye Sekata ya Elimu nchini huku akitaka ufafanuzi wa Mitaala ya kufundishia kwa elimu ya Msingi na Sekondari ambayo alidai haipo

Akiongea Bungeni Siku yatarehe 31. Feb. 2013, Mheshimiwa Mbatia alilalamika sana juu ya mitaala na kuelezea Uongo wa Waziri Wa Elimu aliye ahidi kuwasilisha mitaala hiyo kwa wabunge katika kikao kilichopita lakini hakufanya hivyo

James Mbatia pia alilalamikia makosa yaliyopo juu ya kitabu cha elimu ya Sekondary kwa kidato cha nne na cha sita, somo la hisabati na kusema nimakosa makubwa yote hayo ikiwandani ua hojayake ya Udhaifu uliopo katika sekta ya Elimu nchini
*********************************
Je mitaala hiyo ikibainika kuwa na madudu ndani yake nani atawajibishwa ikiwa sababu za kutopewa Mitaala hiyo kwa wabunge pia aijatolewa na je mhe. Mbatia atajiuzulu kama alivyo sema wakati akiwasilisha hoja yake


EmoticonEmoticon