AFANYIWA UDHALILISHWAJI KATIKA KITUO CHA POLISI

Binti mmoja amemlalamikia Polisi wakituo cha Oysterbay Jijini Dar es salaam kwa madai ya kumfanyia kitendo cha unyanyaswaji wa kijinsia baada kufika kituoni hapo kupata msaada wa kiusalama juzi Jioni, Binti huyo ambaye alikuwa anaumwa baada ya kuingiliwa kinyume na maumbile alifanyiwa kitendo hicho kwamara nyingine na Polisi wakituo hicho

Blog hii inafuatilia zaidi kujua kama nipolisi ndiye aliye fanya kitendo hicho au mazingira yenye ukweli na tukio hilo, kwani binti huyo alienda kama muitaji msaada nasi mtuhumiwa wakosa lolote,

Akiongea na Blog hii dada huyo ambaye anaitwa Sara Julius Kimario alielezea kuwa tukio la kugeuzwa kinyume na maumbile na Polisi huyo, lililomkuta baada ya kutoroka kwa mama ambaye alikuwa akimtumikisha kwa shuguli za Ngono katika danguro moja huko Mwananyamala Sokoni,

Binti huyo alidai kuwa Polisi huyo alimuahidi ange mnunulia chakula na kumtafutia mahali pakulala lakini haikuwa hivyo bali alimtendea unyama huo na kuondoka zake bila kumpa msaada wowote, binafsi aliamini angeweza kumsaidia kwani alikuwa akiumwa na ananjaa sana

Nilikuwa na kaa mwananyamala sokoni ambapo nilikuwa najishugulisha nabiashara za ngono lakini skuwahi kutumika kinyume na maumbile mpaka majuzi hapa nilipo patwa na maumivu makali baada ya kuingiliwa kwanguvu nakupata maumivu ikabidi nitoroke ilikuweza kupata matibabu” Alisema Sara huku alikilia

Sara alifika kituo cha polisi Oyster-bay tarehe 13. Feb. kwaniaya kupata usalama na mahali pakulala kwani alikuwa akilala kituo cha basi Ubungo bila kupata matibabu yoyote

' Niliwahi kwenda kituo cha polisi Kinondoni ambapo nilipewa Arabii ilikuwa tarehe 7 hakuweza kusema niyamwezi wangapi.....ambapo nilienda hospitali ya Mwananyamala nakupata matibabu ambapo nilishonwa lakini sikuwa nimepona kwajinsi nilivyo umia” Alisema Sara

Hapo awali sara alikuwa akiishi Mwananyamala sokoni ambapo amesema walikuwa kwenye danguro wakifanya biashara ya ngono kwa muda wa miaka 14 sasa, nikwa mama mmoja ambaye anajishugulisha na biashara ya madini na kwa muda huo wote hawakuruhusiwa kutoka nje kabisa

Huyu mama anajishugulisha na biashara ya madini (Jina kapuni) na alinitoa kwetu kwania yakufanya kazi zandani lakini baada yakufika huku kazi ilibadilika nakuanza kufanya biashara hiyo” alisema

Sara amesema ndani ya Danguro hilo kwa gorofa yajuu wako mabinti 10 lakini gorofa yachini ajui niidadi ya wasichana wangapi wanakaa, pia jengo hilo linalindwa na walinzi wawili na huwa hawatoki zaidi yakuenda kibara zani. Alisema

POLISI AKANA

Kwakutaka ufafanuzi wa tukio hilo, Nilimpigia OCD Mtafungwa wakituo cha Oyster-bay ilikujua juu yatukio hilo. Ocd alionyesha kutojua tukio hilo nakusema kuwa hana taarifa za mtu kama huyo huku akihaidi kufanya uchunguzi watukio hilo

Sifahamu kuusu tukio hilo na kwa sasa siko ofisini, lakini nitalishugulikia na kusu swala la huyo binti kufika kituoni sina taarifa za kiofisi kujua kama niyeye unaye mtaja kwa jina ...nipigie baada ya muda nitakuwa ofisini” Alijibu OCD Mtafungwa wa Oyster-bay

Alizidi kueleza, kuna binti ambaye yuko pake kituo anatatizo kama hilo ila sina uhakika kama ndiye unaye mzungumzia, kwakuwa nitaenda ofisini nitakupa taarifa zaidi Alisema

Hatahivyo, Taarifa kutoka kwa mtu wandani wa Jeshi hilo ambaye nitahifadhi jina lake, alinielezea kuwa OCD wakituo hicho alikuwa natarifa za binti huyo pamoja na tukio alilotendewa kwani baada ya kuharifiwa juu yatukio hilo aliomba binti huyo apelekwe kituoni hapo

Huyo binti tumemrudisha kituo cha Oyster-bay, nakuna taarifa zake za awali nahata danguro hilo alilokuwa akikaa taarifa zake tayari zilishalifikia Polisi wakituo hicho muda mrefu, wanafuatilia” kilisema chanzo hicho

Jeshi la Polisi linadawati lakushugulikia matatizo ya kijinsia ambapo Blog hii ilimtafuta mmoja wapo kutoka kituo cha Polisi Kurasini ambaye sitataja jinalake na alikiri kutokea kwa tukio hilo huku akisisitiza hata kama nipolisi hayupo juu ya sheria nakuahidi kulishugulikia tatizo hilo

Kisheria kama wewe ni mtuhuiwa au sio mtuhumiwa unapofika au kufikishwa mikononi mwa Polisi jukumu la usalama wako kwao nilakwanza nasio wao kukudhuru wewe kama ambavyo Sara alivyo fanyiwa unyanyasaji wa kijinsia

Hatahivyo sara alisisitisa zaidi juu yakupata nauli nakurudi kwao, Licha ya maumivu makali anayopata hivi sasa. Sara yuko kituo cha Polisi Oyster-bay.

Bahari zaidi utaletewa hapa hapa, kwa sasa naifadhi picha ya binti huyo


EmoticonEmoticon