MATANGAZO YA BUNGE LIVE…TENA, WANANCHI KUJULISHWA KILA HATUA



Baada ya wadau wengi kulalamikia mpango wa Matangazo ya Bunge kutorushwa live kama ilivyo kaririwa na vyombo mbalimbali vya habari kwa wiki moja sasa, Mpango huo umepigwa chini tena nakuwa matangazo hayo yatarushwa live kama ilivyokuwa hapo hawali


Akitoa taarifa hiyo katibu mkuu wa Bunge Dr. Thomas Kashililah amesema kuwa ofisi ya Bunge haitositisha matangazo ya Bunge ila itafanya maboresho mawasiliano kwanjia ya kawaida kupitia Teknohama ambapo watakuwa na Television na Radio ambazo zinarusha matangazo hayo moja kwa moja

Dr, Kashililah amesema, Bunge litazindua Radio yake hivi karibuni ambapo itatmika nchini zima, pia kutakuwa na matangazo ya moja kwa moja kupitia kwenye mtandao mpya ambao utarusha matangazo hayo masaa 24. Aidha vituo vya Television vitaruhusiwa kurusha matangazo hayo moja kwa moja bila kuwekewa mipaka ya aina yoyote ikiwa ni sambamba na matngazo yatakayo tolewa na mitambo ya Bunge

Kama ilivyo hapo awali Bunge halitarusha matangazo ya aina yoyote ile isipo kuwa nakala ya majadiliano ya Bunge kwa mtu yeyote atakaye au kituo cha Television na Radio vitaruhusiwa kupitia katika mitambo yake lakini nayo iwe nakala ya majadiliano ya Bunge

Waandishi wa habari hawatapata furasa ya kuingiza kamera ndani ya ukumbi wa Bunge, bali watapata picha hizo kutoka katika mitambo ya Bunge nakurusha moja kwa moja. Alisema Dr. Kashililah

Bunge litatoa utaratibu (Code of conduct for media broadicasting) wa namana ya kunakili na 
kurusha matanngazo ya Bunge bila kujali yanarushwa kwa utaratibu upi. Hii itasaidia kuweka misingi bora ya mawasiliano na hivyo kuwapafursa wananch kujua hali halisi ya matukio yote ndani ya Bunge na kamati, bila kuegemea upande wowote (Non Partisan) alisema Dr. Kashililah

Dr. Kashililah pia amekanusha swala la Bunge kurorushwa live kuwa alinukuliwa vibaya na kusisitiza kuwa ni maboresho tu ndio yatafuata lakini matangazo y a Bunge yatarushwa live kama hapo awali. Na wanachi watajulishwa kila hatua ya mabadiliko hayo


EmoticonEmoticon