SERIKALI YAKANUSHA WANAJESHI WA KENYA/UGANDA KUTESA RAIA NCHINI

WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA MHE. SHAMSHI VUAI NAHODHA

AKIONGEA Bungeni hii leo Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Mhe Shamshi Vuai Nahodha amekanusha kuwepo kwa majeshi ya nchi jirani ya Kenya na Uganda kuingia nchini kinyemela na kutesa raia kama ambavyo iliwasilishwa Bungeni jana na Mbunge wa Ukerewe Mhe. Silvester Machemli

Akijibu hoja hiyo leo Bungeni kama ilivyo ahidiwa na Spika wa Bunge, Waziri wa ulinzi amesema kuwa siokweli kuwa Askari hao wanawatesa raia ila kunamafunzo ambayo yanaendelea eneo hilo la ukerewe baina ya nchi hizo na Tanzania

“Sikweli kwamba wanajeshi wa nchihizo wanatesa raia na wameingia kinyemela ila kuna mafunzo yanaendelea ya kudhibiti wavuvi haramu wanaotumia nyavu ndogo, na wanajeshi hao wako nchini ambao ni kutoka Kenya, Uganda na Tanzania” Alisema Waziri

Aidha Waziri alisema, Mafunzo hayo yanayoendelea yanatambulika na Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza, Ofisi ya Kata na Kitongoji cha Ukerewe na kuwa siokweli kwamba taarifa ya wanajeshi hao haijaifikia jeshi la polisi

Hatahivyo waziri wa Ulinzi alikemea vikali kitendo cha Kiongozi kutoa taarifa bilaya kukifanyia uchunguzi na ufahamu wa kina, nakumataka mtoa hoja angefanya utafiti kwanza na sio kudanganya umma wawatanzania, Alisema

Naye mtoa hoja hiyo Mhe.Silvester Machemli akikemea vikali kauli ya Waziri huyo ya kumuita kuwa ni muongo na kwamba hajafanyia uchunguzi kile alichokisema huku akisisitiza kuwa anaushahidi wakile alichokiwasilisha hiyo jana kuwa wanajeshi wanchi hizo wananyanyasa raia huku akitaja majina ya wananchi wa jimbo lake waliohadhirika na kadhia hiyo

WASANII/ WAFANYA BIASHARA WAPIGWA BITI – SARE ZA JESHI

Leo Waziri wa Ulinzi ametoa kauli nzito juu ya Wasanii na watu wanaofanya Biashara ya kuuza nguo ambazo zinafanana na sare ya Jeshi la Polisi waache mara moja kwani atakaye bainika Hatua kali za kisheria zitachukuliwa

Akijibu swali lililo ulizwa na Mariam Msabaha Mbunge wa Viti Maalum, ambaye aliuliza serikali inawadhibiti zipi watu wanaotumia sare za Jeshi kwenye uhalifu, Waziri ulinzi amesema kwa wale wasanii wanaovaa sare zinazo fananana na zakijeshi nimarufuku

“Kwa mtu yeyote asiye husika kuendelea kutumia sare zinazofanana na zakijeshi, Tutaendelea kuwasaka na hatutasita kuwachukulia hatua zakisheria kwa mujibu wa sheria” Alisema Waziri wa Ulinzi

Aidha amewataka watu wanaofanya biashara za nguo ambazo nisare za jeshi kuacha mara moja biashara hiyo kwani siruhusa kwa mtu yeyote kumiliki sare hizo au kuuza


EmoticonEmoticon