MITAALA YAWASILISHWA BUNGENI, KAMATI YAIBARIKI NIHALALI SASA KUGAWIWA KWA WABUNGE


 
>MITAALA NIHALISI, KAMATI YASEMA
> Mhe.MBATIA NAE ASHIKILIA MSIMAMO WAKE, KUWA SIO HALISI



> Mhe. KWAWAMBA AZIDI KUPONDA HOJAZEKE, ASEMA AZINA MAANA
Bunge leo limepokea taarifa ya Tume iliyoundwa kuchunguza uhalisi wa mitaala iliyowasilishwa na serikali, Tume hiyo imedhibitisha kuwa  mitaala hiyowasilishwa Bungeni ni halisi na haijachakachuliwa.

Akiongea Bungeni, Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda amebainisha kwamba nakala tatu zilizowasilishwa ya mitaala wa Elimu wa awali, msingi na sekondari zote niza mwaka 2005 na ndio halisi

Kufuatia taarifa hiyo Mhe. James Mbatia ambaye aliibua sakata hilo baada ya kuwasilisha hoja binafsi juu ya udhaifu ulipo katika sekta ya Elimu nchini, Leo amesema kuwa mitaala hiyo sio halisi huku akitoa sababu za kudhibitisha kauli yake hiyo

Mitaala hii sio halisi kwani kwani imekosa sahihi husika na haina namba za utambulisho wa kimataifa, aiwezi kuwa halisiAlisema Mbatia

Mhe. Shukuru Kawambwa, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya ufundi amesema Bungeni hapo, akijibu baadhi ya hoja za Mbatia kuwa sababu anazotoa hazina msingi huku akisisitiza kuwa Siyolazima machapisho ya ndani kama mitaala yawena udhibitisho wa kimataifa
Sakata la mitaala liliibuka Bungeni baada ya Mhe. Mbatia kuwasilisha hoja binafsi ya kutaka kujadiliwa kwa udhaifu uliopo kwenye sekta ya Elimu. Miongoni mwa mambo aliyokuwa akilalamikia ni swala la mitaala ya Elimu kwa Shule za awali, msingi na sekondari 
Pia Waziri aliwai kuahidi Bungeni kuwa angewasilisha mitaala kwa Wabunge kituambacho waziri huyo wa Elimu hakikutekeleza na wabunge wengi wa upinzani kupaza sauti na kusema hakuna mitaala hiyo

WABUNGE WAMKERA  SPIKA WA BUNGE

Spika wa Bunge Mhe. Anna Makinda ameonyesha kukerwa na kukasirishwa na kitendo cha wabunge, kuhudhuria kwa uchache katika vikao vya Bunge kitendo kilicho sababisha kuahirishwa kwa kikao cha saba, Spika amewaambia wabunge kuwa wanapokuwa Bungeni Dodoma hawajipumzisha bali wako kutekeleza majukumu yao ya Kibunge

Taarifa ambazo Blog hii imepata kutoka huko Bungeni nikuwa siku hiyo ya kikao cha 7 jumla ya Wabunge 22 tu ndio walihudhuria vikao vya jioni vya Bunge


EmoticonEmoticon