WATANZANIA WATAKIWA KURIPOTI MATATIZO YA EAC 

Watanzania wametakiwa kuitaarifu serikali juu ya kero na unyanyasaji wanaofanyiwa wanapoingia katika nchi nyingine wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kufanya biashara, ili serikali iweze kuchukua hatua.

Katibu Mkuu Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki nchini Tanzania, Dkt Stagomena Taxi, amesema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumzia maazimio yaliyofikiwa katika mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo ulioisha hivi karibuni.

Bi. Taxi amesema kumekuwa na malalamiko kadhaa ya wanayofanyiwa Watanzania hususani jumuiya ya wafanyabiashara, na kwamba ni jumuku la wafanyabiashara hao kuweka wazi kero hizo ili serikali iwasiliane na nchi husika kwa lengo la kuzitatua.

Katika mkutano huo, Mradi wa ujenzi wa bandari ya Dar es Salaam ulipewa kipaumbele. Ilikuongeza kina cha gati no.1-7, ujenzi wa gati mpya no.13 na 14, ikiwa nipamoja na matengenezo ya bandari za maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Bandari ya Kivu. Suala hilo litaiwezesha Tanzania kufaidika kibiashara.


EmoticonEmoticon