KESI YA LULU YAAMISHIWA MAHAKAMA KUU BAADA YA UPANDE WA JAMUHURI KUSOMA USHAHIDI WAKE LEO

 
Kesi ya Kuua bila Kukusudia inayomkabili Msanii wa Filamu, Elizabeth Michael maarufu kama LULU, imehamishiwa katika Mahakama Kuu, NA Lulu amerudishwa tena Maabusu. Lakini taree ya kusimamishwa katika mahaka kuu aikuweza kutwaja.


Lulu anakabiliwa na kesi ya Kuuwa bila kukusudia, Msanii mwenzake Mareemu Steven Kanumba, ambaye alifariki April 7, 2012 nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam, 


Upande wa jamuhuri leo, Ulisoma taarifa ya ushahidi wa Kesi hiyo, ambayo imechukuliwa kwa watu 9, Akiwemo Seth Bosco mdogo wake mareemu Steven Kanumba, Madaktari walio kuwepo kwenye uchunguzi wa mwili wa mareemu kanumba ambao waliwakilisha familia ya Mareemu, mapolisi waliofanya Upelelezi na walio andika maelezo ya awali ya Msanii LULU.


Katika Ushahidi huo, Jamuhuri ilitoa vitibitisho ambavyo ni ramani ya eneo la tukio, Ripoti ya kitaalamu ya uchunguzi wa kifo hicho, Ambayo imedhibitisha Kanumba liuwawa na mtikisiko wa ubongo yani Brain Concution. Pamoja na maelezo ya mshatakiwa yani LULU


Lulu alipopewa nafasi yakujielezea iwapo ananeno la kuongezea iliviambatanishwe kwenye ushahidi utakao tolewa katika mahakama Kuu., Lulu alisema Hana la Kuongezea.


Hii imekuwa kinyume na watu wengi walivyo sambaza kwenye mitandao ya Kijamii kuwa msanii huyo ameachiwa kwa Dhamana.


EmoticonEmoticon