JK AZINDUA MAJENGO YA HOSPITALI  LEO JIJINI DAR ES SALAAM


Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Dr Jakaya Mrisho kikwete hii leo amezindua majengo mapya ya hospitali, maalum kwa ajili ya Huduma za akina mama na watoto katika Hospitali za Sinza, Mnazi mmoja na Mbagala rangi tatu jijini DSM yaliyojengwa kwa msaada wa shirika la kimataifa la Korea (KOICA).

Raisi Jakaya ameelezea kuwa,Nia na madhumuni ni Kupunguza matatizo ya Uzazi kwa kina mama wajawazito ikiwa pamoja na kupunguza vifo vya watoto walio chini ya miaka 5

Mbali na shughuli hiyo, Rais hii leo pia amekabidhi nyumba zilizojengwa kwa ajili ya wahanga wa mabomu ya Gongo la mboto, shughuli iliyofanyika maeneo ya Gongo la mboto jijini DSM na hapo kesho anatarajia kukwea pipa kuelekea Korea kwa ajili ya ziara ya kikazi.


EmoticonEmoticon