ANALOGIA KUZIMWA DAR ES SALAAM, TCRA WASISITIZA MASAA MACHACHE YALIYO BAKI, WAKAZI WA DAR NAO WAHAHA KWENYE FOLENI NDEFU KUSUBIRI HUDUMA HIYO

KAMA inavyoonekana pichani, kwenye vituo vyote ambako huduma ya ving'amuzi hupatikana kumekuwa na foleni kubwa tangu asubuhi yaleo kufuatia zoezi la kuzima mitambo ya ANALOGIA ilikuamia DIGITALI kutarajiwa kufanyika hii leo usiku saa sita kamili

Mkoa ambao utaanza kuzimwa ni JIJI LA DAR ES SALAA, Ikifuatiwa na mikoa mingine nchini. Msemaji wa TCRA Inocent Mungi amesema zoezi limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na kusisitiza kuzima mitambo hiyo ifikapo saa 12.00 kamili usiku

Aidha, amesema kuusu ubora wa huduma itakayo patika ni ya uhakika na kuwaomba wananchi wanao ishi maeneo ya mabonde kuhakikisha wana Antena mbili ya ndani na yanje ilikuweza kupata stasheni bila chenga


EmoticonEmoticon