BIDHAA BANDIA TATIZO LA KUDUMU NCHINI



BIDHAA BANDIA, haitakaa itoweke kutokana na baadhi ya Watanzania kuchangia kupatika kwa bidhaa hizo hapa nchini kwa kile kilichodaiwa kuwa ni kununua bidhaa ya chini na kuacha bidhaa Halisi.

Akiongea leo, na moja wa wadau wa Campus Vision, Mkurugenzi wa Sera wa shirikisho la wenye viwanda nchini (CTI) Bwana Husein Kamote, amesema tatizo la bidhaa bandia aliwezi kumalizika mara moja, kutokana na wananchi kununu bidhaa za bei rahisi ambazo ni Feki na kuacha za bei ya juu ambazo ndio imara.

Aidha, Mkurugenzi huo aliongeza kuwa Tatizo la Bidhaa Bandia nila kimataifa hivyo kuwawia vigumu kudhibiti bidhaa hizo, kwani nyingi za bidhaa hizo huletwa na nchi ambazo nazo haziko tayari kukubali kuwa wanachagia kuwepo kwa bidhaa hizo hapa nchini.


"Hili limekuwa fumbo kwa nchi hizo hasa pale tunapofanya uchunguzi, akuna nchi inayokubali juu ya swala hilo, na sisi kubaki na ualakini kwa nchi tunazo zihisi," alisema Kamote 

Ametoa wito kwa wananchi wawe makini kuangalia bidhaa hizo, hasa zile zinazo mwagwa mitaani na kusisitiza Wananchi kutoa tarifa bindi wanapoona bidhaa bandia, na elimu kutolewa kwa walaji juu ya bidhaa hizo

Bidhaa zinazoongoza kwa kuwa bandia nizile za Electronic kama TV,Radio, Simu,  Bidhaa za Madawa na Rangi za viatuu. Hata hivyo alisema Watanania huchangia kuletwa kwa bidhaa hizo


posted by 
Samson Charles


EmoticonEmoticon