WABUNGE WA UKRAINE WAZICHAPA BUNGENI


Wabunge wa Ukraine wame zichapa Bungeni, katika kikao cha kwanza cha Bunge hilo, ambapo walitakiwa kupiga kura ya kuidhinisha uteuzi wa Waziri mkuu mpya, Mykola Azaron.

Habari iliyochapishwa na mtandao wa www.Euronews.com, inasema kuwa Wabunge wa Upinzane na wale Wabunge wa chama Tawala walijikuta kwenye hali ya kupigana na kusukumana, baada ya wabunge wa upinzani kutaka kupiga kura ya kumpinga Waziri huyo

Kwa upande mwingine Wabunge wa Chama cha Upinzane walikuwa wakishutumiana, baada ya wenzao wawili kugeukia upande wa serikali, kitendo ambacho kiliwaudhi upinzania na kuzidisha zogo bungeni humo.

Chama tawala kinaitwa Party of Regions, nakile cha upinzani kinaitwa Batkivshchyna’, Lakini hayo yakiwa yanaendelea Ndani ya Bunge baina ya Wabunge wa chama tawala na kile cha upinzani

Kulikuwa na tukio jingine likiendelea nje ya Bunge Hilo.

Kundi kubwa la watu 100 lilikuwa nje ya Bunge hilo kwa maandamano, ambao ni wafuasi wa kundi la FEMEN ambao walikuwa wakijaribu kuingia ndani ya Bunge hili kwa madai ya kuchoshwa na rushwa inayofanywa na viongozi wao, na habari zinasema kuwa waandamanaji hao walikuwa nusu uchi

Hatahivyo hisio mara ya kwanza kwa wabunge hao kupigana, Mwakajana walipiga baada ya kutofautiana kwenye mabadiliko ya muswada


EmoticonEmoticon