KIKOSI CHA TAIFA STARS KITAKACHO IKABILI ZAMBIA DEC.22, HIKI HAPA

Baada ya Kilimanjaro Stars na Zanzibar Heroes Kumaliza kushiriki mashindano ya Kombe la Chalenji jijini Kampala,Kocha Mkuu wa Taifa Stars,Kim Poulsen leo katika ofisi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF),ametangaza kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoingia kambini jioni ya Dec, 12, jijini Dar es Salaa kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Afrika,Zambia (Chipolopolo) itakayo fanyika Desemba 22,2012 katika Uwanja wa Taifa jijini Dra es Salaam

Kikosi hicho kinaundwa na Makipa ni Juma Kaseja, Mwadini Ally na Aishi Manula, Mabeki ni Shomari Kapombe,Erasto Nyoni, Nassoro Masoud Cholo,Agrey Marris,Samih Nuhu, Nadir Haroub Canavaro,Amir Maftah, Issa Rashid na Kelvin Yondani.
Viungo ni Frank Damoyo,Athuman Idd Chuji, Mrisho Ngasa,Shabani Nditi, Mchana Khamis,Salum Abubakar,Amri Kiemba na Mbwana Samata. Washambuliaji ni John Bosco,Simon Msuva na Thomas Ulimwengu.

Katika kikosi hicho, wachezaji walioitwa kwa mara ya kwanza ni kipa Aishi Manula anachezea kikosi cha U20 cha Azam na timu ya Taifa kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes), beki wa kushoto wa Azam, Samih Nuhu, beki wa kushoto wa Mtibwa Sugar, Issa Rashid na mshambuliaji wa Azam, Mcha Khamis.

Pia kati ya wachezaji walioitwa, sita walikuwa kwenye kikosi cha Zanzibar (Zanzibar Heroes) kilichokamata nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika Jumamosi jijini Kamapala, Uganda. Wachezaji hao ni Mwadini Ally, Nassoro Masoud Cholo, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Samih Nuhu, Aggrey Morris na Mcha Khamis.


EmoticonEmoticon