Akizungumza mara baada ya kufungua kesi hiyo ya dahawa namba 24 ya mwaka 2013; mkurugenzi wa kituo hicho Bi. Hellen Kijjo-Bisima amesema hatua ya wao kufungua kesi inatokana na waziri mkuu kutofuta kauli hiyo wanayodai kuwa imevunja katiba na kukiuka kinga aliyopewa na katiba hiyo.
Kwa upande wake, mkurugenzi wa taasisi ya kiraia inayojishughulisha na kufuatilia mwenendo wa bunge ya Citizens Parliament Watch Bw. Albani Markosy, amesema wanaunga mkono hatua ya LHRC na kwamba taasisi hiyo pia inakusudia kumshitaki waziri mkuu kwa madai kuwa siku hiyohiyo alitoa kauli kuwa serikali imechoka.
Shitaka hilo lenye no. 24 la mwaka 2013 dhidi ya Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Mizengo na Mwanasheria Mkuu wa serikali Mhe. Jaji Werema, ikifuatia kauli ya waziri huyo aliyo itoa Bungeni Dodoma katika kikao cha Tarehe 20 mwezi wa 6 2013 ambapo Waziri mkuu aliwaamuru Polisi kuwapiga wale wote watakao kaidi amri kupigwa tu.
EmoticonEmoticon