TAASISI YA MIFUPA (MOI) YAPOKEA VIFAA VYA UPASUAJI WA UTI WA MGONGO


Taasisi ya mifupa ya hosptali ya Taifa Muhimbili MOI, hii leo imepokea vifaa vya upasuaji wa magonjwa ya uti wa mgongo kutoka kwa kampuni moja ya nchini Corea vikiwa na garama ya shilingi Milioni 350 za kitanzania

Akiongea wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo, Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya MOI, Dr. Laurence M Museru amesema vifaa hivyo vitawawezesha kuwahudumia wagonjwa zaidi ya wawili kwa siku tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo mgonjwa mmoja hufanyiwa upasuaji 

kutokana na vifaa hivyo kuwa vichache huku garama za matibabu yake yakiwa ya juu sana. Hii itakuwa neema kwa watanzania wengi hasa wale wanao kumbwa na matatizo baada ya ajali kwani vifaa hivi vitawezesha matibabu ya haraka na pengine garama zitashuka ili kuwawezesha watanzania kupa matibabu.

MAMLAKA YA USAFIRI WA ANGA TANZANIA KUNUNUA MITAMBO YA KUONGOZEA NDEGE, MARUBANI NAO KUFUNDISHWA BURE NA KUFUNDISHA 

Mamlaka ya usafiri wa anga tanzania TCAA, imejipanga kununua mitambo miwili ya kisasa kwaajili ya kuongozea ndege jambo ambalo litaboresha hali ya usalama katika angala ya tanzania pia mamlaka hiyo imepanga kuwasomesha marubani wa 5 ili kuhakikisha nchi inakuwa na marubani wakutosha.

Akiongea na wanahabari hii leo jijini Dar es salaam, msemaji wa mamlaka hiyo Bi. Bestina Magutu amesema mitambo hiyo itaanza kutumika hapo mwaka baada ya kukamilika chini ya mpango wa matumizi wa mwaka wa fedha 2013/2014.

Bi. Bestina ameelezea kuwa, Udhamini huo kwa marubani 5 unatoka katika mfuko wa mafunzo wa Mamlaka ya Usafiri wa anga unaosimamiwa na kanuni ya mwaka 2007 inayofahamika kama Civil Aviation Contibution and Administration of Training Fund ambao umeanza kufanya kazi rasmi mwaka 2011.

Karama ambazo zitatumika kuwasomesha wanafunzi hao ni kiasi Dola za kimarekani Elfu 62 ambayo ni sawa na zaidi ya shilingi Milioni 100 za kitanzania, ambapo watasoma kwa muda wa miezi 14

Aidha, Mhandisi mkuu wa idara ya uongozaji wa ndege wa mamlaka hiyo Bi Valentina Kayombo alielezea matokeo na faida zitakazo patikana wakati mitambo hiyo itakapo anza kutumika hapa nchini kuwa

Tayari kampuni ya ujerumani ya COMSOFT imepata zabinu ya mradi huo utakaohusisha ufungwaji wa mtambo wa satelite wa kufuatilia vyombo angani (Survillence) wa ADS-B yanii Automated Data Surveillance unaogarimu Euro 959,490,000 na ule kukusanya na kutuma taarifa za usafiri wa anga wa AMHS yanii Aeronautical Massage Handling System unaogharimu kiasi cha Euro 621,345,256



EmoticonEmoticon