GOROFA LAANZA KUPOROMOKA HUKU LIKIENDELEA KUJENGWA DAR, AANGUKIA NYUMBA,MAJIRANI WAOFIA USALAMA WAO


Sehemu ya Nyumba ya mama mmoja mkazi wa Kinondoni karibu na Hospitali ya Dr. Mvungi jijini Dar es salaam ilioangukiwa na gorofa linaloendelea kujengwa jirani na nyumba hiyo


Blog hii ilifanya mahojiano na mama ambaye nyumba yake imeangukiwa na gorofa hilo aliyejitambulisha kwa jina la Masele Mohamed Mabula ambapo nilishuhudia chumba kimoja kilivyo haribiwa vibara na kuporomoka kwa kipande cha gorofa hilo


Gorofa hilo linalojengwa na na kampuni ya CASCO, lakini Afisa mtendaji wa kata hiyo ya mwanayamala Bi. Flora Mzanfo amesema anataarifa ya gorofa hilo ambapo amedai kuwa nyumba zilizo jengwa katika eneo hilo zimekaribiana sana kiasi kwamba kuporomoka kwa jengo hilo nilazima kungeadhiri majirani wa eneo hilo

Naye msimamizi mkuu wa majengo wa manispaa ya Kinondoni bwana Charles asema kuwa ufafanuzi zaidi wa jengo hilo alimuelekeza msaidizi wake kulifuatilia iliwaweze kujiridhisha na tukio hilo kisha wachukue hatua zaidi kwa mmiliki wa jengo hilo


Aidha bwana Charles amesema ujenzi wa gorofa hilo umekiuka utaratibu kwani ulitakiwa kujengwa gorofa 4 lakini ujenzi umefika mapaka gorofa ya 3 lakini mpaka sasa ujenzi wa gorofa ya 4 ulikuwa unaendelea mpaka tukio hilo linatokea



Kume kuwa na usalama mdogo kwa majengo marefu hapa nchini hana jijini Dar es salaam, hali inayoonyesha kuwa wahusika na wasimamizi wakuu wameshindwa kufanya kazi yao, huku serikali ikisubiri kila mara kutoa pole na matamko pale maafa yanapo tokea na watu kupoteza maosha.


EmoticonEmoticon