WABUNGE WATAKA UWAZI SUALA LA MADWA YA KULEVYA, LUKUVI YEYE ASISITIZA SERIKALI ITACHUKUA HATUA MPAKA IJIRIDHISHE


BUNGE la 10 mkutano wa 12 kikao cha kwanza imeanza hii leo jijini Dodoma, katika kikao hicho ambapo hoja mbalimbali zilisomwa na maswali kadhaa yaliulizwa huku suala la Madawa ya kulevya yakiwa yameshika kasi mjengoni hapo

Baadhi ya wabunge walitishia kuwataja vigogo na watu mbalimbali ambao wanashiriki biashara hiyo haramu huku kukiwa na swali kwanini wakati wa uteketezaji wa bidhaa hiyo pamoja vyombo vya usalama kushugulikia suala hilo kwa siri kubwa bila kuwepo kwa uwazi

Swali lilielekezwa kwa Waziri wa nchi sera na uratibu wa bunge Mhe Wilium Lukuvi ambaye aliwataka wabunge kuwataja wale wote wanao wafahamu ambao wanashiriki kuendesha biashara hiyo

"kazi ya serikali sio majina tu kwani majina mengi yakitolewa sisi lazima tuyafanyie uchunguzi, tutaendelea kuwataja na kuwachukulia hatua wale tuliowakuta na vielezo nasio kila mtu kutaja tu bila vielelezo"amesema Lukuvi

Mtu yeyote mwenye majina na vielelezo aniletee hapa na nitamsaidia kutaja , wabunge tukisisitiza kutaja majina majina yetu wote yatakuwepo lakini tukiwa na vielelezo lazima tuchukue hatua za kisheria na kusisitiza kuwa ni aibu kwa serikali kupeleka kesi mahakamani kisha tunashindwa kesi na kulipa pesa. amesema 

MAUAJI YA MATAJIRI NAYO YAGUSIWA

Wimbi la mauaji yanayo endelea hapa nchini, hasa kwa wafanya biashara hasa katika mkoa wa Arusha imeelezwa kuwa inaweza kusababisha kudumaa kwa uchumi kwani walio uwawa walikuwa na mchango mkubwa wa kiuchumi hapa nchini, ambapo Naibu waziri wa nishati na madini Mhe. Stephen Julius Masele ameeleza kuwa wizara yake imejipanga kuhakikisha biashara ya madini isiyumbe.

NA FEDHA ZA RADA KUNUNUA VITABU

Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imeendelea kuandamwa baada ya maswali mfululizo kuulizwa bungeni juu ya upungufu wa walimu, vitabu vya kufundishia na mazingira magumu yakiwa ni mambo yanayolalamikiwa na watanzania wengi.

Aidha, Mhe. James Mbatia aliitaka wizara hiyo kuunda jopo la wahariri kukaguwa vitabu hivyo kabla avijafikiwa wanafunzi ambapo waziri wa elimu amesema wizara yake tayari imewapa kazi wataalamu ilikupitia zitabu kabla ya kupeleka kwa wanafunzi.


EmoticonEmoticon