Wanafunzi wanaoishi katika Geto au nyumba za kupanga hawapati nafasi
ya kusoma kutokana na mazingira ambayo wanakumbana nayo katika nyumba
hizo hali ambayo inapelekea wanafunzi wengi kufeli, kubeba mimba au
kuacha shule.
Hayo yamesemwa na kaimu mkurugenzi wa ukuzaji rasilimali wa taasisi
ya elimu TEA Bi Sylivia Lupembe wakati akipokea msaada wa
shilingi Millioni 5 kutoka kwa kampuni ya mafuta ya GAPCO.
“Tumetembea seemu tofauti tofauti hapa nchini tumeona, mazingira
nimagumu kwani mwanafunzi analazimika kupika, kuchota maji na wakati
mwingine hakuna hata umeme wakujisomea, maitaji nayo yanakuwa shida
kuyapata kiasi kwamba mwanafunzi anachoka na kuacha shule” Alisema
Sylvia
Bi.Sylvia liongeza kuwa asilimia kubwa ya wanafunzi wanao ishi katika
nyumba hizo ni wale wanaotoka katika familia duni, kwani kwa mwaka
jana wanafunzi elfu 16 waliacha shule kwa matatizo mbalimbali kama
ujauzito na umbali mrefu.
Mchango ulipokelewa leo na mamlaka hiyo utaelekezwa katika ujenzi wa
mabweni 30 katika shule 1500 hapa nchini ili kuweza kuwawezesha
watoto wakike kupata elimu bila vikwazo, kwani tayari wameanza na
ujenzi wa bweni katika shule ya kibaigwa.
Mamlaka ya elimu pia imewataka watanzania kuwekeza katika usafiri kwa
wanafunzi ikiwa ninjia moja wapo ya kuchangia katika swala la
kuendeleza elimu hapa nchini.
********************************
MKUTANO
WA 31 WA SHIRIKISHO LA MABARAZA YA UPIMAJI NA TATHMINI YA ELIMU
AFRIKA KUFANYIKA ARUSHA AUG. 12-16 MWAKA HUU
Tanzania kuwa
mwenyeji wa mkutano wa shirikisho la mabaraza ya upimaji na tathmini
ya Elimu Barani Afrika, kwa lengo la kujadili kuwepo kwa elimu ya
uvumbuzi pamoja na kuinua kiwango cha walimu barani Afrika.
Akiongea na
waandishi wa habari hii leo jijini dar es salaam, Naibu Katibu
Mtendaji wa baraza la Mitihani nchini Tanzania Dkt. Charles E Msonde
amesema mkutano huo utafunguliwa na makamu wa pili wa Rais wa
zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi huko mkoani Arusha
Mkutano
huo utafanyika kuanzia tarehe 12 hadi 16 Augost mwaka huu ambapo
washiriki zaidi ya 400 watahudhuria mkutano huo kutoka nchi
mbalimbali ikiwemo Kenya, Uganda, Asia na marekani.
EmoticonEmoticon