ASKARI WA JWTZ AFARIKI DRC. CONGO, IGP NAE AFANYA PANGA PANGUA KWA MAOFISA WAKE




Kurugenzi ya habari na mawasiliano makao makuu ya jeshi la wananchi JWTZ limetoa taarifa ya tukio la kufariki kwa afisa wa jeshi hilo akiwa katika jukumu la kulinda amani huko DRC, GOMA


Taarifa za kifo cha askari huyo aliyefariki tarehe 28 Agosti 2-13, ilitokea wakati wanajeshi wetu wakiwa katika eneo la ulinzi ambapo waliangukiwa na bomu na kusababisha majeruhi,


 wakiwa njiani kuelekea hospitalini ndipo askari mmoja ambaye ni Meja Khatibu Mshindo alifariki dunia, lakini majeruhi wengine wanaendelea na matibabu nchini humo.Mwili wa marehemu utaletwa nchini chini ya jeshi la umoja wa mataifa nchini DRC MUNUSCO kwa maziko.

KAMISHA MSAIDIZI ACP DEUSDEDIT KATO AHAMISHIWA

 MAKAO MAKUU YA POLISI
 Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema, amefanya mabadiliko kwa baadhi ya makamanda wa Mikoa na Vikosi ndani ya jeshi hilo

kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na msemaji wa jeshi hilo mrakibu mwandamizi wa polisi SSP Advera Senso, 


Mabadiliko hayo ni pamoja na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Linus Sinzumwa ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi 

Idara ya Upelelezi na nafasi yake inachukuliwa na Kamishina 
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi SACP Zelothe Stephen kutoka Makao Makuu ya Polisi.

Aliyekuwa Kamanda wa Polisi Viwanja vya ndege Kamishna Msaidizi ACP Deusdedit Kato amehamishiwa Makao Makuu ya Polisi na nafasi hiyo inachukuliwa na Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP Selemani Hamisi kutoka Makao Makuu Idara ya Upelelezi

.Wengine ni Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Hamad Hamad anayeenda kuwa Mkuu wa Upelelezi Viwanja vya ndege ambapo hapo awali nafasi hiyo ilikuwa inashikiliwa na David Mwafwimbo aliyehamishiwa mkoani Lindi kuwa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi (OCD).

Aidha SSP Senso amefafanua kuwa uhamisho huo ni wa kawaida kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.


Japo kuwa ASSP Senso amesema panga pangua hiyo ni suala la kawaida katika jeshi hilo lakini huenda Msaidizi ACP Deusdedit Kato aliye hamishiwa Makao Makuu ya Polisi ameondolewa kutokana na skendo za madawa ya kulevya kupitishwa kinyemela katika viwanja vya ndege au ni kwaajili ya kupisha uchunguzi katika eneo hilo.




EmoticonEmoticon